Isabel Martínez De Perón - Rais mwanamke aliyeanza uongozi kwa kuwapa watu matumaini kisha akageuka kuwa dikteta.
|THREAD|
1 July 1974 taifa la Argentina lilipatwa na mshtuko baada ya kupata habari za kifo cha Rais dikteta Juan Domingo Perón aliyefariki kwa ugonjwa wa moyo chini ya mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwake kwa muhula wa 3.

Katiba yao inaeleza kwamba kama Rais akifariki
madarakani basi mrithi wake atakua ni makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Bi Isabel Peron (Pia alikua mke wa Rais aliyefariki) akakatisha safari yake huko barani Ulaya na kurudi nyumbani haraka kisha kuapishwa kuwa Rais tarehe 2 July 1974.
Tofauti na matarajio ya wengi, Mama Isabel alianza kwa kuponya majeraha yaliyoachwa na mtangulizi wake. Waliokatishwa tamaa, kunyanyaswa na kuteswa na mtangulizi wake walianza kuona mapambazuko. Hata makundi ya upinzani yalimuunga mkono hadharani na kusema "Mama anaupiga mwingi".
Kama wasemavyo, "tabia ni kama mpira wa miguu ukitumbukiza kwenye maji, haijalishi utaushikilia kwa muda gani ukiuachia lazima upande juu".

Haikuchukua mwaka, tabia halisi ya Bi Isabel ikapanda juu, akaanza kufuata nyayo za mtangulizi wake na kwenda mbele zaidi.
Watu walitekwa, kupotezwa na wengi kuuawa, wapinzani wakakiona cha mtema kuni, makundi ya haki za binadamu yakaonja joto la jiwe. Akapitisha sheria dhidi ya ugaidi (anti-terrorism law) kwa lengo la kuwabana na kuwanyima haki za kikatiba wapinzani wake.
Katika kipindi cha miezi 15 ya kwanza zaidi ya watu 700 walipoteza maisha, mpaka mwaka 1976 idadi iliongezeka mpaka kufikia zaidi ya watu 1300.
Waliuawa viongozi wa serikali, wahadhiri wa vyuo vikuu mpaka maafisa wa polisi mf. RPC wa mji mkuu Buenos Aires Alberto Villar na mkewe.
Kwa kifupi hakuna aliyekua salama. Wanachi walipata shida zaidi, bei za bidhaa ziliongezeka mara dufu, mfumuko wa bei uliongezeka kutoka 12% mpaka 80% ndani ya kipindi kifupi. Uchumi uliporomoka kwa kasi, gharama za maisha zikapaa. Mama akaanza ufisadi, akakwapua pesa za nchi.
Akapoteza uungwaji mkono hadi kwenye chama chake. Akaanza fukuza fukuza ya viongozi ili kuwaweka watiifu wake, akafurukuta kwa kulipa jeshi madaraka makubwa bila mafanikio. Akaanza kuishi kwa wasiwasi akihofia mapinduzi, wachambuzi wakasema hafiki uchaguzi mkuu akiwa madarakani
Yaliyosemwa yakatimia, mnamo 23 March 1976 miezi 7 kabla ya uchaguzi, wakati Mama Isabel akiwa kwenye sherehe, alionywa kuwa hali ya hewa imechafuka, akaita helicopter ya Rais impeleke ikulu, badala yake ikampeleka kwenye kambi ya jeshi kisha akakamatwa na urais ukaishia hapo.
@threader_app compile

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Leviathan

Leviathan Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(