#Covid19Tanzania: 💥 Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?

Je, COVID-19 ni nini?
COVID-19 ni maambukizi yanayosababishwa na virusi vya Corona, virusi hivi ni sawa sawa na vile vinavyosababisha mafua ya kawaida tofauti na mafua…
virusi vya corona vinaweza kuambukiza mwingine kabla hata ya huyo mtu hajaanza kuonesha dalili. Tofauti ni kwamba, watu wenye matatizo mengine ya kiafya kama matatizo ya mapafu au ugonjwa wa kisukari, wamo katika hatari kubwa ya kuhisi kuhisi matatizo makali ya mapafu.
Watu walio na virusi vya COVID-19 kwa kawaida wataonyesha dalili zifuatazo: homa kali na kikohozi au kuhisi kuishiwa na pumzi. Athari zikizidi, wanaweza kuwa na matatizo makubwa ya kupumua na watahitaji kulazwa katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi wengine hupoteza maisha.
Je, COVID-19 inaenezwa vipi?
Virusi vya COVID-19 huenezwa hasa kwa kutangamana na mtu ambaye aliyeambukizwa na kuathirika au kuguza vifaa ambavyo viliguzwa au kupigiwa chafya na mgonjwa aliye na COVID-19. Virusi hivi hupatikana kwenye chembechembe za mate au makamasi.
Vinaingia mwilini kwa kuguza au kupitia kwa kinywa, Pua au macho.
Jinsi ya kujizuia kupata ugonjwa wa COVID-19
Kunawa mikono kwa sabuni yako na kuepuka kugusa uso wako kwa mikono yako ni njia bora zaidi za kuepuka kupata magonjwa. Kujitenga kijamii (kudumisha angalau umbali wa mita 2 au futi 6 mbali na wengine)
na kukaa nyumbani kama vile iwezekanavyo pia ni njia nzuri ya kuzuia kupata huu ugonjwa. Ili kuzuia kuambukiza virusi hivi kwa wengine, watu wanapaswa kukohoa au kupiga chafya huku wakifunika mdomo wao kwa sehemu ya ndani ya visugudi na sio kwa viganja zao na kuvaa Barakoa.
COVID-19 ilianza lini?
Virusi vya Corona vimeingia Afrika Mashariki baada ya mgonjwa wa kwanza kuripotiwa nchini Kenya tarehe 13 Mar 2020 na 16 Machi 2020
Mgonjwa wa Kwanza akagundulika Nchini Tanzania. Mlipuko wa Virusi vya Korona (kwa Kiingereza: Coronavirus) ulibainika rasmi tarehe za katikati za mwezi Desemba mwaka 2019 katika mji wa Wuhan huko Nchini China.
Hadi sasa, zaidi ya Watu Milioni 3.81 wamepoteza Maisha kutokana na Ugonjwa wa COVID-19 Huku Watu zaidi ya Milioni 176 Wakiwa Wameambukizwa Duniani Marekani, India na Brazili zikiwa zinaongoza.
NINI MCHANGO WA WANASAYANSI KATIKA KUPAMBANA NA COVID-19?
Kutokana na kuenea kwa kazi kwa ugonjwa wa COVID 19 ambao hadi sasa bado dawa yake haijapatikana, Watafiti wanaendelea kufanya Jitihada Pamoja na kutafuta Chanjo ya Ugonjwa.
Baadhi ya Chanjo za COVID-19 zimeonesha ubora katika kupambana na Maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19

CHANJO YA COVID-19
Nchi nyingi sasa zinatoa Chanjo za COVID-19 bure ili kujilinda na Maambukizi.
Kutokana na Chanjo ya COVID-19 kuonesha ubora wa kupamba na COVID-19 Baadhi ya Chini sasa ni lazima kuchoma sindano ya Chanjo ili uweze kuingia Nchi hizo.
Baadhi ya Mataifa ya Afrika yanayotoa chanjo na chanjo wanazotumia ni:
Morocco (AstraZeneca na Sinopharm)
Algeria (Sputnik V)
Misri (Sinopharm)
Kusini mwa jangwa la Sahara, mataifa yanayotoa chanjo ni:
Afrika ya kati(Johnson & Johnson)
Ushelisheli (Sinopharm na AstraZeneca)
Rwanda (taarifa zinasema wanatumia Pfizer na Moderna)
Mauritius (AstraZeneca)
Zimbabwe (Sinopharm)
Mataifa mengine kama vile Senegal na Guinea ya Ikweta yamepokea chanjo za Sinopharm lakini bado hazijaanza kutoa chanjo kwa umma.

Guinea ilitoa chanjo 60 za Sputnik V kutoka Urusi kwa watu kwa majaribio.
JE, KUNA UMUHIMU WA TANZANIA KUKUBALI KULETEWA CHANJO? MTIZAMO WAKO NI UPI?
Hivi karibuni Kamati maalum ya wanasayansi iliyoundwa na rais wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan kutoa thathmini kuhusu hali ya ugonjwa Corona nchini, imeonya kuwa nchi ipo katika hatari ya kukabiliwa na wimbi la tatu iwapo hatua hazitochukuliwa.

Ripoti ya Kamati hiyo, ilitaka Serikali kuanza kuchukua hatua za kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo,
kuanza kutangaza watu walioambukizwa virusi vya corona, na kuagiza chanjo. Kamati hiyo ilishauri serikali kupitia vyombo vyake kulishughulikia suala la chanjo kwa kujiunga na mpango wa COVAX ulio chini ya mwamvuli wa GAVI.
Mpango wa COVAX unalenga kuhakikisha nchi masikini kote duniani zinapata mgao sawa wa chanjo licha ya ufinyu wa uwezo wao wa kiuchumi.
Wakati hayo yakiendelea, Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar, amewataka Wananchi wanaotaka kwenda Kuhijji, Wajiandae kuchanjwa kwani huwezi kuingia Maka Saudi Arabia bila kuchanjwa.
Hivi Sasa Serikali imeanzisha utaratibu wa kupima COVID -19 tena mara msafiri anapowasili kutokana na kuwepo vyeti vya COVID-19 vya kughushi huku wengine wakipata maambukizi wakiwa safarini na kuingiza Ugonjwa nchini.
“Kipimo tunachotumia sasa kinaonyesha majibu kwa muda mfupi na hata kama Mtu amepata maambukizi ndani ya saa mbili au tatu zilizopita tunambaini. Hii ndiyo namna ya kudhibiti maambukizi yasiingie nchini,”alisema Mkurugenzi wa huduma za kinga, Dk. Leonard Subi.
GHARAMA ZA KUPIMA UNAPOWASILI UWANJA WA NDEGE

Kwa mujibu wa utaratibu wa sasa msafiri yeyote anatakiwa kujaza fomu ya kuomba kupima Corona mtandaoni, kisha kwenda kwenye hospitali au kituo husika na kupima.
Gharama za malipo ni Dola za Marekani 100 (sawa na Sh. 230,000 ), Sh. 10,000 ya Hospitali au kituo ulichopimiwa na siku ya kurudi au kuingia nchini unatakiwa kulipa Dola 25 (sawa na Sh. 57,750)
MAMBO UNAYOHITAJI KUFAHAMU KUHUSU CHANJO YA COVID-19

Usalama wa chanjo za COVID-19 ni kipaumbele cha juu. Chanjo ya COVID-19 imethibitishwa kuwa salama na yenye ufanisi.
Nchini Marekani, hatua nyingi zimewekwa ili kuhakikisha kuwa chanjo ni salama na zenye ufanisi. Hatua hizi zinajumuisha waliojitolea kutoka makundi mbalimbali ya rangi, kabila na umri wanaoshiriki katika majaribio ya
kitabibu ili kuhakikisha kuwa chanjo ni salama kwa jamii mbalimbali. Taarifa na takwimu kutoka kwenye majaribio zinakaguliwa kwa kujitegemea na wanasayansi, wataalamu wa tiba, na wataalam wa afya ya umma kabla ya wewe kupewa chanjo.
Vituo vya Kudhibiti Magonjwa (CDC) vimeunda zana mpya ya kugundua haraka maswala yoyote ya usalama kuhusiana na chanjo za COVID-19. "V-safe" ni zana mpya inayotumika kwenye simu mahiri, ya kukagua afya baada ya chanjo.
Itatolewa kwa watu wakati watakapokuwa wanapokea chanjo ya COVID-19.
Chanjo ya COVID 19 itakusaidia kujikinga kutokana na kupata COVID-19. Dozi mbili zinahitajika
Unahitaji dozi 2 za chanjo ya sasa ya COVID-19 ili kupata kinga kubwa zaidi dhidi ya ugonjwa huu mbaya.
Hivi sasa kuna usambazaji mdogo wa chanjo ya COVID-19 nchini Marekani, lakini usambazaji utaongezeka katika wiki na miezi ijayo
Kila mtu ataweza kupata chanjo dhidi ya COVID-19 mara tu idadi kubwa ya kutosha ya chanjo itakapopatikana. Chanjo ikishapatikana kwa wingi, kutakuwa na watoaji wa chanjo maelfu kadhaa.
Mnamo tarehe 13 Disemba 2020, ACIP ilitoa mapendekezo ya matumizi ya chanjo ya COVID-19 ya Pfizer-Biotech ili kuzuia COVID-19.

Mnamo tarehe 20 Disemba 2020, ACIP ilitoa mapendekezo ya matumizi ya chanjo ya COVID-19 ya Moderna ili kuzuia COVID-19.
Ukosefu wa fedha za kulipa, hali ya uhamiaji, au ukosefu wa bima havitakuzuia kupata chanjo dhidi ya COVID-19
Dozi za chanjo zitatolewa kwa watu bila malipo bila kujali hali ya uhamiaji au ikiwa wana bima au la. Watoaji wa chanjo wanaweza kutoza ada za usimamizi wa kutoa chanjo.
Watoaji wa chanjo wanaweza kulipwa ada hii na kampuni ya bima ya umma au ya binafsi ya anayepokea chanjo.
Baada ya chanjo ya COVID-19, unaweza kupatwa na athari za kawaida. Hii ni ishara kwamba mwili wako unajenga kinga
Athari ni dalili kwamba chanjo inafanya kazi, athari zinaweza kuwa kama homa na zinaweza hata kuathiri uwezo wako wa kufanya shughuli za kila siku, lakini zinapaswa kuondoka baada ya siku chache.
Kama Mwananchi, upi mtizamo wako juu ya Chanjo ya Corona na njia zinazotumika kupambana na Covid - 19 hapa nchini Tanzania?

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Magna Carta 自由憲章

Magna Carta 自由憲章 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @RealHauleGluck

10 Aug
Je, Kuna uwezekano kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA @freemanmbowetz kuoneshwa Mubashara kwenye vituo vya TV?

Mhe. Rais @SuluhuSamia katika mahojiano na @BBCNews umesema kesi ya Bw. Mbowe ni nafasi nzuri kwa mahakama zetu, kuionyesha dunia kuwa haki inatendeka kwa usawa na uwazi.
Kutokana na ukweli kwamba tangu mwalimu Julius Nyerere apewe kesi ya aina hiyo ‘UGAIDI’ na wakoloni wa Uingereza hakuna kiongozi wa kisiasa amshafunguliwa mashtaka ya aina hiyo tangu Uhuru. Basi itakuwa vema @judiciarytz ikimpa Bw. Mbowe ‘open, fair and transparent trial’
Kesi ya Bw. @freemanmbowetz ina ‘public interest’ kubwa sana. Ili kujenga imani na @judiciarytz uendeshaji mzima wa jaribio ‘trial’ ufanyike mubashara. Watanzania na dunia iweze kufuatia shauri hili lenye maslahi makubwa kwa demokrasia, haki na utawala wa Sheria. Ni ushauri wetu.
Read 4 tweets
10 Aug
RAIS HAKUZUNGUMZA NA CHADEMA BALI DUNIA

Ni maajabu kuona CHADEMA wanamjibu Rais @SuluhuSamia katika masuala mbalimbali ambayo ametoa maoni yake Kikatiba.
Swala la @freemanmbowetz Rais SSH amesema wazi tuache @judiciarytz wafanye kazi yao na kuhakikisha Haki inatendeka.
UKWELI MCHUNGU, hakuna utulivu ndani ya CHADEMA, tulitegemea wachukue MUDA kutafakari na kuyafanyia kazi yale aliyosema Rais @SuluhuSamia sio kukurupuka kuita ’Press’ eti wanamjibu. Watakuwa wanamjibu kila akifanya mazungumzo?
KWAMBA RAIS KAINGILIA UHURU WA MAHAKAMA

Ni dai lenye akili ambalo halijazingatia ’logic na facts’. Rais @SuluhuSamia amejibu swali la @Salym na kupitiliza kidogo kuzungumzia kesi ya Mbowe kitendo ambacho hata Chadema wamekuwa wakisema kuwa Mbowe kafunguliwa mashtaka ya kisiasa.
Read 12 tweets
10 Aug
CHADEMA wanakutana kujadili mahojiano ya Rais @SuluhuSamia na @bbcswahili ili kujibu nini?
Tumeona mahali @godbless_lema ameandika kwamba @ChademaTz kitakutana kujibu mahojiano ya Rais SSH na @Salym, wanataka kukutana kujibu nini?
Chama kinaendeshwa kwa matukio? 🧐 Image
Tunashauri CHADEMA waache kukurupuka na kuparamia kila jambo. Tunashauri kwa mapenzi yetu kwa CHADEMA, Rais Samia kasema kuna Uhuru wa Habari, Baada ya Uchaguzi tujenge Nchi, Kesi ya Mbowe ilikuwepo lakini upelelezi haukuwa umekamilika, tuache Mahakama itafsiri sheria.
Ukweli Mchungu, wote humu tunajua kwamba ni kweli kesi ya @freemanmbowetz ilikuwepo, sio ya sasa, Rais amesema uongo? Kuhusu swala la kujenga CHADEMA wanatakiwa kujitathimini, kuanzisha na kuendeleza migogoro isiyoisha hakutatupa mwanya kushiriki katika Ujenzi wa nchi.
Read 4 tweets
10 Aug
Mahojiano Maalum ya Rais ⁦@SuluhuSamia⁩ aliyofanya na ⁦@bbcswahili⁩ na mwandishi nguli ⁦@Salym⁩ yamegusa mambo mengi kwa mfano;
• Demokrasia
• Uhuru wa Habari na Vyombo vya Habari
• Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni
• Siasa bbc.com/swahili/habari…
• Uhuru wa vyama vya siasa kufanya siasa
• Uchumi
• Hali ya maisha ya watanzania
• Tozo Mpya za Miamala
• Kesi ya UGAIDI inayomkabili Bw. @freemanmbowetz
• Uhuru wa Mahakama @judiciarytz kutoa Haki.

Mwandishi @Salym ameuliza maswali mazuri ambayo yana tija kwa sasa.
Mwandishi @Salym amegusa kila eneo ambalo alipaswa kugusa kwa weledi kabisa. Kwa wale waliotazama mahojiano hayo watagundua kuwa Rais @SuluhuSamia amejitahidi kujibu kila swali aliloulizwa. Mwandishi amefanya kazi yake vema sana na amegusa maeneo yote muhimu aliyopaswa kugusa.
Read 10 tweets
9 Aug
Tofauti ya uwekezaji wa hati fungani na masoko mengine ya mitaji kama Hisa

Hatifungani ni tofauti kabisa na masoko mengine ya mitaji kwa mfumo wake na hata faida zake.
Kwenye hatifungani unapata faida bila ya kujali uchumi unakwendaje. Kwa sababu unaponunua hati fungani unajua kabisa ni riba kiasi gani unapata kwa mwaka. Lakini kwenye hisa hujui ni faida kiasi gani unapata kwenye uwekezaji wako.
Faida inategemea na hali ya uchumi, uimara wa Soko.

Kwenye hisa unapata faida pale hisa zinapofanya vizuri na unapata hasara pale hisa zinapofanya vizuri. Kwenye hatifungani unapewa riba uliyoambiwa bila ya kujali fedha ulizowekeza zimezalisha au la.
Read 7 tweets
9 Aug
I think there can be a collective activism. Maybe some symbolize the struggle for human's rights and Equality a little more than others, but I think it's absolutely necessary for the activists to be united in order to make the struggle effective, Image
instilling hatred and blocking other activists for personal reasons kills the power of struggle and helps the oppressor. No struggle for justice has ever been won anywhere in the world without unity and solidarity of the frontline defenders.
I think if we, say, if all of the major activists in this struggle for human's rights, equality, rule of Law are at, at war with each other, then I think it would be very difficult to make this social revolution the kind of powerful revolution that we wish to be.
Read 5 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(