Learn, Earn and Grow
Jifunze kujifunza(Learn to learn)
Niliwahi kusema kwamba Katika dunia hii ya teknolojia kuna watu wa aina mbili.
1.Makers(Design, Product and Engineering )
2.Hustler(Management, Marketing and sales)
Sasa twende kwenye kujifunza kujifunza...
Jambo la kwanza katika kujifunza ni kujifunza juu ya wewe. Jua ni wapi wewe unafit kwa kuangalia internal traits zako na skills sets zako. . Jua strength zako, ni vitu gani unavifanya kwa urahisi zaidi na kuona matokeo makubwa zaidi.
Ni vitu gani ukivifanya unaenjoy na kupata flow nzuri. Kisha angalia jamii inahitaji nini kwenye vitu hivyo na develop skills katika vitu hivyo.
Pata ujuzi pata ujuzi
Ni rahisi sana kucommit muda mwingi katika kujifunza kitu unachokipenda. Utaona muda unakimbia sanaa. Angalia vitu unavyovipenda kuvifanya, vitu ambavyo ukiweka jitahada kidogo unapata matokeo na unafurahia kuvifanya na wekeza kua bora kwenye hivyo.
Sasa tuchambue wale watu wawili niliowataja pale juu.
Hustlers
•Marketing. Marketing is all about helping other people communicate and how the solution you are providing is the best. Katika dunia ya leo kama unayo simu na unaweza kuconnect na mtandao basi unaweza kufanya mambo mengi makubwa
Unaweza kujifunza marketing skills za karne ya 21 na unaweza kupata Kazi. Unaweza kujifunza marketing kutoka katika communities mbali mbali moja wapo zipo katika magroup ya facebook, magroup ya makampuni mbali mbali mfano hubspot wanayo wafunzo mazuri na community nzuri
•Angalia product unayoipenda au website au huduma flani. Kisha angalia improvement unazoweza kushauri zifanyike, tengeneza sample kama unaweza kisha watumie email.
Lakini pia unaweza kushiriki kama scout wa kampuni husika. Hakuna mmliki wa biashara ambaye atakataa wateja. Andaa plan/proposal ya jinsi gani unaweza kuwaleta wateja katika huduma au kampuni unayoipenda kisha muandike decision maker mmoja wapo katika hiyo kampuni
Kisha watafute hao wateja kwanza na walete kwao kisha unaweza kuomba employemet au hata comission katika kila mteja utakaye mleta.
•Unaweza kuniuliza nitapata vipi hizo products. Zipo njia nyingi sana za kupata products za kuuza moja wapo ni website inatwa clickbank.com lakini pia mtandao umejaa maelfu kwa maelfu ya product nzuri zinazotafuta water.
Builders
Kuna nguvu kubwa sana katika kujenga vitu. Kama wewe ni Developer team up na developer wengine na tengenezeni vitu kama softwares zinazo tatua matatizo halisi yanayowakumba nyinyi au marafiki kisha iterate kuhakikisha kwamba unagusa watu wengine pia(scale it).
Hakikisha unashare na watu wengine progress zako katika mtandao. Ipo mitandao mingi na community nyingi unazo weza kushare product yako na ukapata watumiaji mfano twitter, linkedin, facebook niche groups, indie hackers, product hunt etc.
Bill Gates aliwahi kusema “If you spend 10,000 hours doing something you will be super good at it” Ni masaa 10,000 ya kuchagua kufanya kitu tena na tena na tena hivyo ndio kujifunza kwa hakika.
Earning
Unaweza kutengeneza kipato kwa njia zifuatazo
•Kumiriki hisa za kampuni ambayo mwanzoni haikua na thamani na kupata capital gain pale itakapo kua na thamani kubwa. Kampuni hii inaweza kua yakwako au ya mtu mwingine.
•Lakini pia unaweza kutengeneza fedha kama mshahara au ujira unao upata kutokana na kutumia ujuzi wako kutatua changamoto za watu wengine.
If you are learning you are good but if you are learning and earning you will be unstoppable
#SwahiliCyryptos Part 1
Watu wengi wamekua wakiniuliza kwa habari ya Cryptocurrency nikaona sio vibaya mimi kushare notse zangu kwa mfumo wa thread.
Bila kuchelewa #Cryptocurrency ni nini?
Neno cryptocurrency ni muunganiko wa maneno mawili cryptography na currency.
Katika cryptography, tunatumia Mahesabu ya hali ya juu kulinda fedha na kuhakikisha hakuna mtu anatumia kiasi cha fedha zaidi ya kile kiasi halali alichonacho. Na neno currency ni fedha.
Cryptocurrency ni aina ya fedha za kidigitali unazoweza kuzitumia kulipa nauli ya basi, kuwalipia marafiki vinywaji bar, kununua chakula sokoni na kadharika. Kwakua Cryptocurrency ni fedha ya kidigitali inaweza kutumwa popote pale duniani.