Fortunatus Buyobe Profile picture
Jan 8, 2022 18 tweets 4 min read Read on X
Hii ilikuwa ni miaka ya '90 mwanzoni, tukitokea pembezoni mwa mgodi wa Mwadui, tulifahamika kwa jina la "Wabeshi". Image
Zana zetu za kazi ilikuwa ni sululu, chepe na majembe yaliyonolewa sana, tulikabiliana na jeshi la polisi la mgodi wa Mwadui waliokuwa na kikosi cha farasi na mbwa wenye uweredi mkubwa sana na mafunzo ya hali ya juu. Image
Nakumbuka siku rafiki zangu wawili walivyouwawa kwa kuumwa na mbwa sehemu za siri na jirani yangu Jilingumika Masufulia alivyopigwa risasi ya kichwa akivuka fensi ya mgodi wa Mwadui. Image
Almasi tuliibatiza jina la "ng'ana", na ilikuwa hauwezi kwenda kuiba bila kuchanjwa chale za kwapani na matakoni. Mganga wetu mkubwa alikuwa ni Mzee maarufu sana wa Kijiji cha MWIGUMBI, Nje kidogo ya mgodi, huyu ndio mzee aliyetupa dawa na kinga wakati wa kwenda kuiba almasi, Image
Nilikuwa na miaka 16 nimemaliza darasa la saba shule ya msingi Luhumbo.Tajiri wetu mkubwa alikuwa mwarabu wa Maganzo maarufu kwa jina la Abeid,huyu alitupikia vitumbua na chai kabla ya kwenda mgodini kuiba almasi, na chote tulichokipata tulipeleka kwake kama tajili na kulipa Image
Tajiri Abeid hakuwa mtu "rahisi rahisi", yeye mganga wake alikuwa anatokea kijiji cha Idukilo, mganga hatari sana aliyekuwa na madawa ya kisukuma ambayo yaliwabadilisha watu na kuwa mbwa mwitu au nyani pindi walipoingia ndani ya mgodi kuiba,
tajiri Abeid alikuwa anaishi kijiji cha Maganzo, akiwa na duka la bidhaa la kuzugia,lakini deal zake kubwa ilikuwa ni kununua almasi na kuziuza kwa matajili wakubwa wa Mwanza na Shinyanga mjini. Image
Almasi zote tulizopeleka kwa Abaeid zilikuwa zinatunzwa na mbuzi dume, beberu mkubwa aliyekuwa anazimeza na kuzihifadhi tumboni hadi mteja atakapokuja,hata polisi wakifika na ku-search vipi,wasiongeziona almasi kwani beberu alikuwanazo tumboni,
hakuwa beberu wa kawaida maana alikuwa na chumba chake na alilala ktk godoro. Mbuzi hakula nyasi wala majani ya miti, bali vitumbua, chai na "maparage". Kipindi hicho hatukuwa na ruhusa ya kuongea juu ya mbuzi yule, tulimuogopa na kumtii zaidi hata ya kiongozi wetu.
Tajiri wa uhakika alikuwa Fantomu wa maeneo ya Mipa,huyu hakuonana na sisi wabeshi maana tulikuwa watu "wadogo" sana, bali alipitia kwa Abeid na waarabu wengine wa Maganzo.
Maisha ya kuwa "mbeshi" yalikuwa magumu sana,maana kifo na kujeruhiwa ilikuwa ni njenje,tuliuwa na kuuwawa.
Polisi, mbwa na farasi waliokuja bila tahadhari waliuwawa kwa chepe zilizonolewa na mapanga. Tukio moja nalokumbuka ni la mwenzetu Masunga kumuua mbwa wa polisi kwa kumkata na chepe mdomoni na kuutenganisha mdomo pande mbili.
Wenzetu wengi walikufa tukiwa bwawani tukiiba,wengi walizama kwenye tope liliotokana na mabaki ya kusafishwa kwa almasi ambayo sisi tulikuwa tunakwenda kuchota na kuchekecha upya,
bwawa hili la tope zito lilukuwa karibu na "sorting area" ambayo ililindwa kwa kiasi kikubwa sana. Lakini kwa imani ya chale za mganga wa MWIGUMBI na Idukilo watu wengi tulikuwa na ujasiri wa kukatiza kila mahali bila hofu.
Wengi waliojeruhiwa na kuumizwa walilazwa ktk hospitali ya Mwadui.Siku nilipoamua kuacha "kazi" hii na kurudi shule,ilikuwa ni siku hatari sana... binamu yangu kipenzi Luhende alipigwa risasi ya kichwa na ubongo kutawanyika, mbele ya macho yangu Luhende alikufa bila kuomba maji.
Askari wakiwa umbali wa kama mita 100,sisi tukiwa na makarai yetu na chekecheke tukiambaaambaa pembeni ya reli maeneo ya SONGWA ktk njia ya mzunguko kuelekea Maganzo tuliwekwa katikati yao na kuuliwa baadhi yetu.
Katika kundi la wabeshi kumi, saba walikufa hapo hapo..watatu walifia hospitali na mimi pekee nilipona baada ya kujitumbukiza kwenye bwawa la maji ya kunywea mifugo, niliogolea chinichini kwa chini na kuibukia upande wa matete, ambapo nilikaa ndani ya maji zaidi ya masaa 12
Tuendelee na wahabeshi?

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Fortunatus Buyobe

Fortunatus Buyobe Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @fbuyobe

Jun 27
Mwaka 2012, Blandine Nyoni akiwa katibu mkuu wizara ya afya, alinukuliwa akitoa kauli tata ya kuwabeza madaktari kuwa "wanajiona bora wakati ni wachafu na hawajui kiingeleza" Image
Katibu huyu akaendelea kusema kuwa hata yeye alisoma mchepuo wa PCB na kufaulu vizuri tu lakini kwa kutambua ubovu wa Medicine mzazi wake akamsomesha Accounts so hajui madaktari wanalalamikia nini.

Kauli hii ikang'oa kilaka kwenye jeans ya bishoo! Image
Ni kwamba mwaka huo, madaktari walikuwa katikati ya mgomo wa kihistoria

Kauli hii ikawatibua madaktari wakalianzisha upyaaaaa

Uzi👇

Dr. Ulimboka and total tools down

Nisome Image
Read 76 tweets
May 9
Wiki hii tumeshuudia waliokuwa wanachama wa Chadema wakitangaza kuachana na chama hicho huku wakiahidi kuelezea hatima zao za kisiasa siku za mbeleni

Kati ya waliohama ni waliowahi kuwa viongozi waandamizi wa chama hicho

Hii inamaanisha nini? Image
Kabla sijajibu swali hilo ni vyema tukipitia kwa ufupi mtiririko wa matukio (A quick refresher)

1. Dec 12,2024, Tundu Lissu anatangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA taifa

Nia hii ya Lissu ilikuja baada ya kuwa uchokozi wa wazi dhidi yake ndani ya chama Image
Kabla ya uamuzi huu, Lissu aliyekuwa ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA, alishamwandikia barua katibu mkuu wake kumjuza nia yake ya kuendelea kugombea kubaki kwenye nafasi hiyo.

Ulikuwa ni utaratibu wa CHADEMA kwa viongozi wa juu kutoshindania nafasi moja endapo mmoja ataonesha nia Image
Read 34 tweets
Mar 12
Monday, 24th,
June 1996 10:30 AM
Central Police post, Dsm

Majira ya saa nne asubuhi, anaingia kituoni hapa mfanyabiashara mwenye asili ya Asia ndugu Walji D Ladwa

Hapa kafika ili kutoa taarifa juu ya kuibiwa kwa gari lake lenye namba za usajili TZG 50

THREAD👇👇 Image
Bwana Ladwa alidai gari lililoibiwa ni Nissan Patrol lenye namba nyeupe.

Polisi katika upelelezi wao wakatajiwa kuwa gari ile imeonekana akiwa nayo jambazi mmoja sugu sana ambaye alikuwa kwenye radar za polisi kwa muda mrefu. Image
Jambazi huyu si mwingine bali ni Ernest Joseph Sambua Mushi maarufu kwa jina la White

Taarifa zikadokeza jambazi lile lipo mkoni Kilimanjaro kwa wakati ule

Yule mfanyabiashara akajulishwa juu ya hili na akatoa gari lake na dereva ili kwenda Kilimanjaro

Gari namba TZB 7209 Image
Read 13 tweets
Mar 11
Jan 22, 2024 kwenye kikao cha baina ya CDF na makamanda kwa upande mmoja, na Amiri Jeshi mkuu kwa upande mwingine,Mkuu wa majeshi alitoa kauli iliyoibua udadisi

"Kuna wakimbizi wameteuliwa serikalini kwenye nafasi za maamuzi"

Kauli hii ilikuwa ni nzito kutoka kwa mtu mzito. Image
Nasema mtu mzito kwa kuwa, mtu aliyetoa kauli hii ni mwenye nafasi ya kupata taarifa zote za intelejensia za nchi hii

Kwanza kama mwenyekiti wa kamati ya majeshi ya ulinzi

Pili akiwa kama kiongozi kwenye taasisi yenye chombo kinachofanya "military intelligence" siku zote. Image
Kwa hiyo CDF Mkunda alikuwa anajua anachokizungumza ni sahii kutoka vyanzo sahii

Undisputed and not farfetched facts

Kauli hii kwa mtu asiyeutumia ubongo wake vizuri, ataisoma tu kwenye magazeti na kuachana nayo bila kuusumbua ubongo kuona yale yasiyoonekana. Image
Read 28 tweets
Feb 25
Kumekuwepo na taarifa za kukamatwa kwa wahusika wa kampuni ya LEO BENEATH LONDON (LBL) inayoendesha biashara ya upatu, kukusanya amana, na kutoa riba kwa wanachama wake.

Victims wengi wa kampuni hii wakiwa ni watumishi wa kada ya ualimu Image
Image
Image
Pia Benki kuu imetoa taarifa ya kutoitambua wala kuipatia leseni kampuni hiyo.

Hapa ndipo napata maswali kuhusu umakini wa taasisi zetu zinazohusika na ukusanyaji wa taarifa za kiitelejensia

Taasisi hizi huwa hazipati fununu ya uwepo wa kampuni hizi kabla watu hawajatepeliwa? Image
Sasa hivi kuna kampuni nyingine inayojiita FIC

Kampuni hii inajinadi kuwa imesajiliwa BRELA na kupata cheti No. 177461385

Imepata TIN ya TRA No. 177-461-385 na kupewa cheti cha Tax Clearance Image
Image
Image
Read 8 tweets
Feb 24
Sometimes March 2013 Wakili Fatuma Karume alisafiri kutoka Dar kwenda mkoani Kilimanjaro. Wakili huyu alikuwa amesafiri akiwa amebeba nyaraka furani ya muhimu. Nyaraka ile alikuwa anaenda kumsomea na kumkabidhi mzee fulani aliyefahamika kwa jina la Juma Image
Actually, Mzee Juma naye alikuwa ni wakili ambaye sasa amestaafu akiwa amefanikiwa kurithisha taaluma hiyo pia kwa mwanae ambaye alikuja kuwa ni wakili maarufu sana mkoni Arusha. Fatma hakujua kama nyaraka aliyobeba ingeleta taflani kubwa ndani ya familia ya Mzee Juma. Image
Fatma aliwasili nyumbani kwa ambako alikuta waombolezaji ambao walikusanyika baada ya kusambaa taarifa za msiba za mmoja wa watoto wa Mzee Juma. Fatma alitegemea kuikuta hali hii nyumbani pale na hata safari yake ilitokana na yeye kupata taarifa hizi. Image
Read 40 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(