Hapa ni Ziwa Victoria, eneo la katikati ya Musoma na Kinesi, hapa ndipo unapopita mkondo wa Mto Mara, unaoingiza maji yake Ziwa Victoria. Unaweza kuona maji yalivyokuwa rangi nyeusi. Nitaeleza baadhi ya mambo kwa kifupi sana.

Nakala kwa @SuluhuSamia na wote wanaohusika
Mto Mara unatiririsha maji yake kutoa katika milima ya Mau iliyopo nchini Kenya na baadaye kuingia Tanzania kuanzia katika Wilaya za Serengeti, kuingia wilaya ya Tarime, unakatiza katika wilaya ya Butiama na Wilaya Rorya kabla ya kuingiza maji yake katika Ziwa Victoria.
Kirumi, Ryamisanga, Kitasakwa (Butiama), Kwibuse, Kwibwe, Bisarwi, Kuruya (Rorya), Nyabichume, Matongo, Nyamongo, Bisarwi, Mrito (Tarime) ni sehemu ambazo zinatumia maji ya mto Mara na kwa namna moja ama nyingine vimeathirika kwa maji hayo kuchafuliwa kwa utando huo wa mafuta.
Mto Mara umezungukwa na wakazi mbalimbali katika vijiji hivyo nivyotaja ambao wanajihusisha na shughuli za kibinadamu za uzalishaji mali zikiwepo ukulima, uvuvi, ufugaji mifugo, na shughuli za uchimbaji madini (migodi). Tatizo hili ambalo leo limeundiwa kamati siyo Mara ya kwanza
Kamati aliyounda Waziri chini ya Mwenyekiti wake Profesa Samuel Manyele kutupia tuhuma kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto hasa mimea vamizi kama vile magugu maji na matete na kwamba mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara
Profesa Samuel Manyele anasema wamebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe zaidi ya tani 1.8 milioni na mkojo wa ng'ombe lita 1.5 bilioni uchafu uliotokana na kuwepo kwa ng'ombe zaidi ya laki 3 katika eneo oevu la mto Mara kwa kipindi cha miezi minane mwaka 2021 wakati wa kiangazi.
Kwamba mgodi hauhusiki na uchafuzi huo ni upotoshaji na wakazi wa Mkoa wa Mara hatukubaliani nao. Tunaikataa taarifa hii ya 'kamati ya michongo' na itakuwa siyo mara ya kwanza, tumewahi kukataa taarifa ya hovyo ya kamati aliyounda Profesa Sospeter Muhongo, huko Nyamongo.
Wananchi wanaoishi kuzunguka mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara gold mine, Nyamongo, Tarime, Mara, Mwaka 2016 waligoma kupokea matokeo yaliyotolewa na kamati ya Muhongo baada ya kamati kuthibisha maji yanayotiririka kutoka katika mgodi hayana madhara yoyote kwa viumbe hai
Prof Muhongo akachukua sampuli ya maji maeneo yanayotiliwa shaka, akaema kwa usimamizi wa kamati yake, sampuli zake atapewa Mbunge John Heche naye apeleke kuchunguzwa maabara yoyote ile ili naye apate majibu yake na zoezi kama hilo afanye Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga.
Baada ya taarifa ya NEMC iliyosomwa na Peres Joshua kukataliwa, wananchi wa eneo hilo walichukua sampuli ya maji hayo waliipeleka maabara ya Nairobi, Kenya na majibu yakatoka Machi 20, 2015 yaliyobaini kuwa yana sumu na hayafai kwa matumizi ya mifugo na binadamu.
Au litolewe agizo la kupimwa tena kwa maji yanayotoka katika vyanzo vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara ili kujiridhisha kuwa hayana athari kwa binadamu, mifugo na mazingira na kama yana viwango vinavyokubalika kwa matumizi ya binadamu, mifugo na mazingira
Viwango vinavyopaswa kutumika katika upimaji wa maji haya lazima viwe vya Shirika la Afya Duniani (WHO) hivyo zichukuliwe tena sampuli za maji wakati sahihi (kiangazi na masika, wataalam wanafahamu) na zipimwe tena na maabara huru. Sampuli hizo zigaiwe kwa makundi mbalimbali
Sampuli hizo, tuzipeleke katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo France, Germany na Belgium au pengine ambako kuna maabara za kisasa na zinazoaminika duniani. Siyo lazima kujifungia ndani na kulipana posho na kamati zisizokuwa na mantiki. Tuwasaidie wananchi siyo kuwaumiza.
Vyanzo vya maji katika sehemu nyingi zenye uchimbaji mkubwa na mdogo duniani vimekuwa vikiathiriwa na shughuli za migodi Mamlaka zinazosimamia Sekta ya Maji pamoja Mgodi ziwasiliane ili kupata chanzo mbadala cha maji na hivyo kuondoa malalamiko ya wananchi wanaozunguka mgodi huo.
Maji hayo ya Mto Mara yanayoua samaki hao yalibadilika na kuwa rangi nyeusi, juu kumetanda kitu mithili ya mafuta na yanatoa uvundo. Samaki wafu walianza kuonekana 8/3/2022 na wananchi wanaotumia maji ya mto Mara wakaanza kuwaokota na kuwapeleka sokoni kuwauza.
Pia, kwanini wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini wasihakikishe kuwa kila baada ya miezi mitatu wanachukua sampuli za maji katika vyanzo vinavyozunguka mgodi huo na kuzipima ili kujiridhisha kuwa maji hayo hayana madhara kwa binadamu, mifugo na mazingira?
Tujadili hili la Mto Mara la hivi karibuni; Wavuvi waliokuwa katika shughuli zao, walikuta samaki wakielea mtoni, aina ya gogogo na sato. Na walippfikishwa sokoni au nyumbani, waliotumia, waliharisha sana na kutapika. Hali hiyo iliwakuta wakazi wa Bisarwi, Manga, Kirumi, Kembwi,
Wavuvi wakafikisha taarifa kwa uongozi wa vijiji hivyo kuwepo kwa maji yenye sumu, meusi kwa rangi, na kutanda kwa mafuta yakiashiria hatari kwa afya ya binadamu na wanyama na Mazingira yao. Viongozi wa vijiji wakachukua Jukumu la kutoa elimu kwa wanakijiji, wasiyatumie.
Hata Mbwa waliokula nyama za mifugo hiyo iliyokufa walidhurika. Binadamu waliokula samaki wanaotakana na maji hayo walipata madhara. Samaki wanaotokana na maji hayo wanapoteza ladha ua kawaida ya samaki na wanatoa harufu mbaya ya uvundo.
Lakini tayari watu wengine walishakula vyakula vinavyopatikana katika maji hayo ya mto Mara na kudhurika, ikiwepo nyama za mifugo yao iliyokunywa maji hayo na kufa pia samaki waliopatikana kutoka katika mto Mara. Ikabidi viongozi wa Kijiji wapeleke taarifa ngazi za Juu
Watu wa kwanza kutoka serikalini kufika eneo hilo ni kutoka wizara ya maji na wizara ya uvuvi, wakafika na boti zao, wakaingia mtoni, wakachukua sampuli za maji hayo, na samaki wakapeleka maabara kwa ajili ya kufanya utafiti na vipimo vya kisayansi.
Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria imeeleza wamebaini uwepo wa kiwango kikubwa cha mafuta kuliko kiwango kinachokubalika kwa mujibu wa viwango vya ubora maji Tanzania (TZs 2068:2017), na kukosekana kwa hewa ya Oksijeni kwenye maji ya mto Mara kupelekea samaki na viumbemaji kufa
Waziri wa nchi, Ofisi ya makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Seleman Jafo akaunda kamati yake maalum kuchunguza suala hilo chini ya Profesa Samuel Manyele, kamati ikaeleza, maji yalichafuka kutokana na mimea ya asili jnayozalisha sumu, kinyesi cha ng'ombe na mvua kutibua tope.
Pia viongozi wa vijiji kadhaa waliwasilisha Taarifa za mifugo yao kufa kutokana na kutumia maji ya mto Mara baada ya halo hiyo kuonekana. Katika Kipindi Cha wiki mbili pekee, kitongoji cha Burongo, Kijiji cha Bisarwi kata ya Manga, Tarime kilipoteza ng'ombe 54 na mbuzi nane.
NB: Wakati Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) Ilipaswa kutafuta mbadala wa upatikanaji wa maji kwa wananchi waliopo kandokando ya Mto Mara wakati uchunguzi ukiwa unaendelea, lakini mmezuia wasitumie maji, lakini serikali haijatoa mbadala wake. Mnataka watumie njia gani?

#MMM

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Martin Maranja Masese

Martin Maranja Masese Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @IAMartin_

Mar 29
Historia ya nchi yetu inaonyesha Katiba ya Uhuru ya Tanganyika mwaka 1961 haikuwa na haki za binadamu kutokana na Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) kuzipinga kwa kuwa serikali yake ilikuwa na agenda ya kuleta maendeleo ya haraka “We need accelarators no breaks”
Na hivyo mwaka 1962, 1964, 1965 na hata mwaka 1977, Katiba za Tanganyika na baadaye Muungano hazikuwahi kuwa na tamko la Haki za Binadamu (The Bill of Rights). Mabadiliko ya tano ya Katiba ya JMT 1977, mwaka 1983 yaliingiza sehemu ya Haki za Binadamu katika Katiba.
Hata hivyo ibara ya 31 inatoa mwanya kwa kuzuia baadhi ya haki wakati wa hali ya hatari na hivyo katika Ibara ya 32 kumpa uwezo Rais kutangaza hali ya hatari iwapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo vitani, kuvamiwa na kuingia vitani
Read 9 tweets
Mar 29
Ibara ya 7(1)kwa mtazamo wangu tunaweza kuibakiza, kwa kuwa inatoa sharti kwa Serikali na vyombo vyake na mamlaka za kutunga sheria au utoaji haki kuzingatia masharti yote ya sehemu hii lakini ibara ya 7(2) iondolewe ili mwananchi wa Jamhuri ya Muungano awe na uwezo kamili wa 👇
kuhakikisha utajiri wa Taifa unaendelezwa kwa manufaa ya kila mtanzania kwa kuweza kwenda Mahakamani kuishtaki Serikali pale inapovunja au inapoelekea kuvunja misingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali. (Sasa hivi hatuna haki hiyo) Ibara ya 7(2) inapunguza uzito wake.
Ibara ya 8 inaweka misingi ya demokrasia na haki ya jamii ambayo ni kuwa:-
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi ...
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
Read 9 tweets
Mar 29
Ibara ya 11 inatamka haki ya kufanya kazi, haki ya kupata hifadhi ya kijamii, ambazo ni miongoni mwa haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni (social, economic and cultural rights). Lakini kwa haki hizi kuwekwa nje ya tamko la Haki za Binadamu (The Bill of Rights) na hivyo 👇
kunaondoa kabisa maana yake katika utekelezaji kama haki zenye mashiko kwa mwananchi wa Tanzania kwa kuwa mwananchi hana uwezo wa kuidai nchi yake haki zake hizi za msingi maana zipo nje ya Haki za Binadamu (The Bill of Rights).

Tujadiliane katika eneo hili, kinagaubaga!
Kuwa haki ya kupata hifadhi ya kijamii ambazo ni haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni zijumuishwe katika tamko la Haki za Binadamu na kuwezesha wananchi kuzitekeleza na kuzidai ili kufanya maadui ujinga, umaskini na maradhi kutoendelea kutamalaki nchini
Read 4 tweets
Mar 29
Ibara ya 7(1) ya katiba ya JMT inatoa sharti kwa Serikali na vyombo vyake na mamlaka za kutunga sheria au utoaji haki kuzingatia masharti yote ya sehemu hii. Lakini Ibara ya 7(2) inapunguza uzito wa malengo muhimu na misingi ya mwelekeo wa Serikali yaliyotajwa ibara ya 7(1)
Masharti ya sehemu hii, hayatatiliwa nguvu ya kisheria na Mahakama yeyote. Mahakama yeyote nchini haitakuwa na uwezo wa kuamua juu ya suala kama kutenda au kukosa kutenda jambo kwa mtu au Mahakama yeyote, au kama sheria, au hukumu yeyote inaambatana na masharti ya sehemu hii
Ibara ya 8 inaweka misingi ya demokrasia na haki ya jamii ambayo ni kuwa:-
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi ...
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
Read 9 tweets
Mar 29
Katiba ni muafaka wa kitaifa unaoanisha namna taifa linavyohitaji kujitawala katika mambo yote na kuendesha mambo yake. Hivyo, Katiba ya nchi ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali pia huanisha haki za msingi za wananchi
Katiba ya nchi hutungwa na wananchi kama watu huru ili kupata muafaka wa taifa lao na namna gani wangependa kujitawala, umiliki wa nchi na rasilimali ya wananchi, nafasi ya wananchi katika utawala na namna gani wataweka utawala wa nchi yao kutengeneza muundo wa serikali yao.
Katiba ni Waraka na muafaka wa Kitaifa. Ni Makubaliano ya jinsi gani wangependa utaratibu wa utawala uundwe nchini kwao. Katiba ni Waraka wa kisiasa na kiutawala uliokubalika na wananchi wote ili uwe msingi na rejeo la taratibu na sheria zote zitakazo tungwa na kuwekwa.
Read 5 tweets
Mar 29
Wananchi wengi pia wanalalamikia kuhusu elimu na huduma za afya. Wengi wanasema, elimu bora na huduma za afya bora zinatolewa kwa watu wa tabaka la juu (kuna ubaguzi usio eazi sana). Wao wanabaki na shule zenye huduma hafifu na zahanati zenye kutoa huduma hafifu katika maeneo yao
Sasa tuipate katiba mpya ambayo itaweka misingi katika dira ya taifa. (nitaeleza mbeleni). Madhumuni ya kuweka Malengo Muhimu na Misingi ya Shughuli za Serikali ni kuhakikisha kuwa Serikali na mamlaka zake zinapewa mwongozo wa kisera na mwelekeo wa kiutendaji.m kuhudumia umma.
Pamoja na mambo mengine malengo yafuatayo LAZIMA tuweke kwa ajili ya wakulima, wafugaji na wavuvi (makundi ya uzalishaji mali hayo);

(i) Kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima, wafugaji na wavuvi;
Read 6 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(