Anselmo Profile picture
Mar 28 15 tweets 2 min read
MBINU zitakazokusaidia KUUZA Huduma zako kwa urahisi zaidi.

Siku zote, wateja huangalia ubora wa huduma wanayoipata bila kujali sekta ya biashara uliyopo.

Ndio maana, ni muhimu sana kufahamu ni kwa namna gani unaweza kuwafikia na kufikisha huduma zako kwa haraka.

#UZI
Hizi ni Mbinu 5 zitakazokusaidia KUUZA huduma zako kwa urahisi, kupitia mitandao ya kijamii.

1. Hakikisha WANAKUTAMBUA mapema.

Ni rahisi kuuza huduma zako kama tu Audience watakuelewa mapema, na kufahamu THAMANI ya kile unachowapatia.
Jaribu kutumia LUGHA rahisi, itakayowasaidia Audience wako kufahamu kuhusu huduma zako na namna unavyoweza kutatua changamoto zao.
Muhimu zaidi, jitahidi kuongea lugha wanayoongea audience wako.

Kama ni watu wenye changamoto za uzazi, basi zungumza lugha yao. Gusa maumivu yao, ili wakuelewe kwa haraka na kuwa tayari kununua huduma zako.
2. Onyesha UPEKEE wa Huduma zako.

Ili unielewe vizuri, soma mfano huu.

Fikiria mteja A, anahitaji kupata Mshauri na Huduma juu ya kupunguza uzito ili awe na Afya nzuri zaidi.

Bahati mbaya, baada ya kupita katika kurasa kadhaa zinazohusika na huduma hiyo ...
hakuridhika. Mwisho wa siku, akafanya uamuzi ya kuanza kufanya mazoezi peke yake...

Kwa sababu, hakuona UTOFAUTI katika page zote alizotembelea.
Hali aliyopitia Mteja A, ndio wanayopitia wateja wengi pale wanapotafuta huduma kwa ajili ya kutatua changamoto zao.

Kuna kurasa nyingi sana mtandaoni, zinazofanana almost kila kitu.

Ndio maana, wewe kama mfanyabiashara, ni muhimu kufanyia uchunguzi washindani wako ...
Ili kufahamu uzuri na udhaifu wao. Hii inaitwa Competitors Analysis.

Kuwa na taarifa kuhusu washindani wako (kibiashara) ili uje na mbinu mpya zitakazokupa utofauti na upekee katika huduma zako.
3. Fikiria kuhusu THAMANI (Value) utakayompa Mteja wako.

Moja kati ya kitu muhimu sana unachopaswa kukumbuka wewe kama mfanyabiashara, ni kwamba...

... Ubora wa huduma zako upo katika THAMANI unayoitoa, na si GHARAMA za huduma zako.
Weka focus yako kubwa katika kuongeza THAMANI ya huduma zako, kuliko kupandisha au kushusha Gharama zako.

Ili kukusaidia kuongeza THAMANI zaidi katika huduma yako, ninakupa mbinu hii...
Weka huduma zako katika mfumo wa PACKAGE.

Tengeneza Package zenye gharama tofauti tofauti, ili kumpa mteja uhuru wa kuchagua kulingana na THAMANI anayoipata katika Package husika.
4. Dumisha MAHUSIANO yako na wateja wako.

Furaha na mafanikio makubwa katika huduma zako, haipo pale mteja anapolipia huduma zako.

Bali, ni namna utakavyodumisha uhusiano wako na kila mteja anaenunua huduma zako.
Nikuibie siri moja...

Ni rahisi sana kumshawishi Mteja aliyewahi kununua huduma zako, kuliko yule ambae bado hajanunua kabisa.

Mafanikio yamejificha katika kujenga mahusiano ya MUDA mrefu na wateja wako. Wekeza hapo!
5. Usikubali kuwa JIWE!

Kuwa huru katika kufanya mabadiliko, kulingana na mahitaji ya soko.

Wakati wowote, mabadiko yanaweza kutokea katika sekta yako ya biashara au tabia za wanunuaji wako.
Weka room ya mabadiliko, ili kuendana na mahitaji ya soko kwa wakati husika.

Umenielewa? Umeongeza kitu?

Usiache kuRETWEET ili Maarifa haya yawafikie watu wengi zaidi.

Your friend
Ansey.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Anselmo

Anselmo Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @CoachAnsey

Oct 26, 2021
MUHIMU: KAMA UNA ACCOUNT YA BIASHARA.

Huwa unajisikiaje pale unapowekeza juhudi & muda wako katika jambo flani, halafu usione matokeo?

Au

Umepanda mbegu zako vizuri, ukiwa na matumaini muda si mrefu zitaanza kuzaa matunda. Halafu gafla unaaza kuona zinanyauka/kufa?
Enhee, sasa hiyo hali ndio utakayoipata pale unapoanza kuona followers wako wanapungua siku hadi siku katika Ukurasa wako wa Biashara.

Kama utagundua idadi ya followers wako inapungua, ni lazima uchunguze na kutafuta suluhu haraka sana!
Lazima kuna sababu inayowafanya waondoke kwenye ukurasa wako.

Ni kweli hautaweza kuwarudisha, lakini utapunguza uwezekano wa kuendelea kuwapoteza zaidi.

Sasa, ni sababu zipi zinasababisha Followers wako kukukimbia?

Ready??

Let's Walk kidogo sasa🚶‍♂️
Read 17 tweets
Oct 14, 2021
UNATESEKA KUPATA MAUZO KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII?

Inawezekana una Bidhaa nzuri, una Huduma bora kabisa, una post kila siku kwenye account zako, lakini huoni ukipata faida yoyote kupitia mitandao ya kijamii unayotumia

Nina Habari njema sana kwako siku ya leo

Are you ready?🤔
Kabla haujafanya uamuzi wa kufuta post zako, au kufunga kabisa kurasa za biashara yako...

Nataka kukuonyesha Hatua 5 muhimu sana zinazoweza kukusaidia ili kupata matokeo mazuri.

Twende wote taratibu sasa...
1. Anza kwa kuweka Malengo Maalumu.

Inawezekana unafeli sehemu kubwa kwa sababu haujui ni nini unataka kutimiza kila siku, week au mwezi.

Anza kupanga Malengo maalumu kila siku. Haya yatakuwa kama...
Read 13 tweets
Oct 13, 2021
UNASHINDWA KUANDIKA CAPTION NZURI KATIKA POST ZAKO?

Kama una Brand au unaendesha biashara yako kupitia Mitandao ya kijamii...

... basi utakuwa unafahamu ni ngumu kiasi gani kuja na mawazo ya kuandika kila siku katika kila post unayoweka kwenye ukurasa wako.
Kutokana na jinsi unavyotaka watu wakutazame kupitia Brand/biashara yako...

...Unaweza kuchagua Tone ya sauti unayotaka watu wakutambue nayo.

Kupitia Caption zako, unaweza kuonekana Mcheshi, Mpole, au serious kiasi.

Sasa Social Media Entrepreneurs wengi ni WAVIVU mno...
katika uandishi wa Caption.

Unakuta mtu amepost Picha ya Viatu au Handbag, then kaandika tu

"Kiatu kama hiki ni Tsh 65,000/= Piga namba hii 0712 312XXX"

Come on! Hapo unaweza kusema umemshawishi mteja wako kununua?

Usichukulie poa, unazungumza na Mteja kupitia Caption yako!
Read 13 tweets
Aug 18, 2021
MBINU 5 ZITAKAZOKUSAIDIA KUKUZA BIASHARA YAKO KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII.

Inawezekana hapo ulipo umekwama, huoni maendeleo yoyote ya biashara yako, wakati huo huo unaona wapinzani wako wanaendelea kupiga hatua.

Upo katika hali hiyo?
Usiwe na wasiwasi, kila mfanyabiashara au mjasiriamali kama wewe, amewahi kupitia hali kama hiyo.

Kama umeshindwa leo, haina maana utaendelea kushindwa kila siku.

Au unasemaje Brother @mafolebaraka ?
Siku zote SILAHA kubwa katika biashara na MAARIFA!

Maarifa ndio silaha yako kubwa, ndio maana leo unapaswa kunisikiliza kwa makini kwa sababu ninaenda kukupa MAARIFA (Mbinu) takazokusaidia kufufua tena matumaini yako.
Read 21 tweets
Aug 16, 2021
JINSI YA KUTENGENEZA MAUDHUI (CONTENTS) YENYE KUONGEZA USHAWISHI KWA MTEJA.

Mara nyingi katika kutengeneza Maudhui, tunatumia mawazo, Ideas na ushawishi wetu binafsi...

..lakini, kuzingatia muonekano na aina ya Maudhui yanayoandikwa ni jambo muhimu mno.
Ni rahisi sana kutengeneza mawazo na topic mbalimbali kwa ajili ya wateja wako...

..Lakini, kama muuzaji, ni lazima uwe na uelewa mkubwa wa namna ya kuwasilisha mawazo hayo kwa mteja wako.
Ndio maana ni muhimu sana kufahamu namna mbalimbali ya kuandika maudhui yanayokidhi mahitaji ya mteja wako.

Kupitia mchanganyiko huu wa maudhui, itakusaidia kuongeza wafuasi wako zaidi, kufikia wateja wapya, na kutengeneza mazingira rafiki ya kuuza Bidhaa au huduma yako.
Read 13 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(