Anselmo Profile picture
Helping People Start & Grow their Brands and Businesses Online | Building @ThamaniAcademy to Digitalize Learning #ChelseaFan💙
14 Oct
UNATESEKA KUPATA MAUZO KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII?

Inawezekana una Bidhaa nzuri, una Huduma bora kabisa, una post kila siku kwenye account zako, lakini huoni ukipata faida yoyote kupitia mitandao ya kijamii unayotumia

Nina Habari njema sana kwako siku ya leo

Are you ready?🤔
Kabla haujafanya uamuzi wa kufuta post zako, au kufunga kabisa kurasa za biashara yako...

Nataka kukuonyesha Hatua 5 muhimu sana zinazoweza kukusaidia ili kupata matokeo mazuri.

Twende wote taratibu sasa...
1. Anza kwa kuweka Malengo Maalumu.

Inawezekana unafeli sehemu kubwa kwa sababu haujui ni nini unataka kutimiza kila siku, week au mwezi.

Anza kupanga Malengo maalumu kila siku. Haya yatakuwa kama...
Read 13 tweets
13 Oct
UNASHINDWA KUANDIKA CAPTION NZURI KATIKA POST ZAKO?

Kama una Brand au unaendesha biashara yako kupitia Mitandao ya kijamii...

... basi utakuwa unafahamu ni ngumu kiasi gani kuja na mawazo ya kuandika kila siku katika kila post unayoweka kwenye ukurasa wako.
Kutokana na jinsi unavyotaka watu wakutazame kupitia Brand/biashara yako...

...Unaweza kuchagua Tone ya sauti unayotaka watu wakutambue nayo.

Kupitia Caption zako, unaweza kuonekana Mcheshi, Mpole, au serious kiasi.

Sasa Social Media Entrepreneurs wengi ni WAVIVU mno...
katika uandishi wa Caption.

Unakuta mtu amepost Picha ya Viatu au Handbag, then kaandika tu

"Kiatu kama hiki ni Tsh 65,000/= Piga namba hii 0712 312XXX"

Come on! Hapo unaweza kusema umemshawishi mteja wako kununua?

Usichukulie poa, unazungumza na Mteja kupitia Caption yako!
Read 13 tweets
18 Aug
MBINU 5 ZITAKAZOKUSAIDIA KUKUZA BIASHARA YAKO KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII.

Inawezekana hapo ulipo umekwama, huoni maendeleo yoyote ya biashara yako, wakati huo huo unaona wapinzani wako wanaendelea kupiga hatua.

Upo katika hali hiyo?
Usiwe na wasiwasi, kila mfanyabiashara au mjasiriamali kama wewe, amewahi kupitia hali kama hiyo.

Kama umeshindwa leo, haina maana utaendelea kushindwa kila siku.

Au unasemaje Brother @mafolebaraka ?
Siku zote SILAHA kubwa katika biashara na MAARIFA!

Maarifa ndio silaha yako kubwa, ndio maana leo unapaswa kunisikiliza kwa makini kwa sababu ninaenda kukupa MAARIFA (Mbinu) takazokusaidia kufufua tena matumaini yako.
Read 21 tweets
16 Aug
JINSI YA KUTENGENEZA MAUDHUI (CONTENTS) YENYE KUONGEZA USHAWISHI KWA MTEJA.

Mara nyingi katika kutengeneza Maudhui, tunatumia mawazo, Ideas na ushawishi wetu binafsi...

..lakini, kuzingatia muonekano na aina ya Maudhui yanayoandikwa ni jambo muhimu mno.
Ni rahisi sana kutengeneza mawazo na topic mbalimbali kwa ajili ya wateja wako...

..Lakini, kama muuzaji, ni lazima uwe na uelewa mkubwa wa namna ya kuwasilisha mawazo hayo kwa mteja wako.
Ndio maana ni muhimu sana kufahamu namna mbalimbali ya kuandika maudhui yanayokidhi mahitaji ya mteja wako.

Kupitia mchanganyiko huu wa maudhui, itakusaidia kuongeza wafuasi wako zaidi, kufikia wateja wapya, na kutengeneza mazingira rafiki ya kuuza Bidhaa au huduma yako.
Read 13 tweets