~Mkumbushe mwanao kuwa WIVU utamfanya amchukie Mtu ambaye alipaswa ajifunze kutoka kwake...
~Mkumbushe Mwanao kuwa Msaada sio Haki yake asipopewa Asinung'unike atafute Chake...
~Mkumbushe Mwanao kuwa Tumeona mazuri kwa watu waliokuwa wakiitwa wabaya na Tumeona mabaya kwa watu waliokuwa wakiitwa wazuri kwahiyo Aishi na kila mtu kwa akili...
~Mkumbushe Mwanao kuwa bila Mungu hatofika popote
~Mkumbushe Mwanao kuwa Tunakosa Usingizi ili wanaotutegemea wapate kulala Vizuri..
~Mkumbushe Mwanao kuwa Akiwa baba hata akiumwa hatotamani watoto wajue maana tumaini lao pekee ni yeye...
~Mkumbushe Mwanao kuwa Kilicho bora kwake hakiwezi kuwa bora kwa watu wengine...
~Mkumbushe Mwanao kuwa Alipoamka leo kuna Mwenzake amevuta Pumzi ya Mwisho, inabidi amshukuru Mungu kwa hii zawadi ya Siku Nyingine...
~Mkumbushe Mwanao kuwa Njia yake ikishanyooka Asithubutu kuwanyooshea vidole ambao Njia zao bado zina KONA...
~Mkumbushe Mwanao kuwa Mtu atakae mpatia Bega wakati analia basi Asimsahau wakati amenyamaza...
~Mkumbushe Mwanao kuwa Wengine hatuna Mtu wa kumtegemea au Ndugu wa kumlilia Shida, Ukimtoa MUNGU Tunaamini sana kwenye Nguvu, Juhudi na Maarifa Yetu. ZAIDI Aishi Vizuri na Watu ila asijipe umuhimu kwenye maisha ya WATU... #Tuishi
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Kuna wakati kwenye maisha unaweza kujiuliza “Mbona mambo hayabadiliki kwa haraka kama ninavyotaka?”
Unakumbuka kitu kinaitwa “GESTATION PERIOD!?” Yaani ule muda tangu ujauzito umetokea hadi mtoto amezaliwa.
Usisahau, kwenye maisha kuna vitu ni MATOKEO YA MUDA.
Yaani ni kama mama mjamzito, haijalishi ana hamu ya mtoto kiasi gani ni lazima asubirie miezi tisa.
Changamoto kubwa utakayokutana nayo utakapotaka kulazimisha, ni kuishia kuharibu kile kizuri ambacho ulipaswa kukipata.
Kila unachokitamani kwenye maisha huwa kina “gestation period”.
Siku umepata wazo hadi litakapokuwa halisi, kuna muda wa kusubiri.
Siku umeanza kusoma hadi utakapomaliza, kuna muda wa kusubiri.
Siku umekutana na umpendaye hadi mfanikiwe kuishi pamoja, kuna muda wa kusubiri.