MAFANIKIO NI SAFARI NDEFU.
Miaka minane iliyopita siku moja Nikiwa ndani ya Ofisi fulani nikiwa kama mfanyakazi wa muda tu (kwani nilikuwa na mkataba wa miezi sita tu) alikuja kijana mmoja kutafuta Kazi mahala pale lakini Kwa Bahati mbaya hakupata nafasi.
Sikufahamu kabisa! Lakini baadae nilikuja kufahamu baada ya kutoka nje ili kupata breakfast ndio nikamkuta mlinzi akimtoa Kijana yule Kwa nguvu maana alikuwa amekaa kwenye parking za gari (sehemu ambayo haruhusiwi mtu kukaa)
Jun 20, 2022 • 12 tweets • 3 min read
KIJANA MWENYE NDOTO KUBWA,JIFUNZE HAYA;
1.Jifunze kuwa Mbunifu. Hakuna kitu kipya sana,vitu ni vilevile,lakini kama kijana mwenye ndoto kubwa jifunze kuwa mbunifu,Usiendelee kufanya vitu kwa mazoea,Kuwa mbunifu katika kila jambo unalofanya ili ulete utofauti katika eneo husika. 2. Jifunze stadi za Maisha (Life skills),Duniani kuna watu zaidi ya bilioni 7 na kila mtu anatabia zake na ana mitazamo yake,hivyo ni vizuri kila mara ujifunze stadi za maisha,namna gani ya kuishi na watu wa aina tofauti tofauti,
Kuna wakati kwenye maisha unaweza kujiuliza “Mbona mambo hayabadiliki kwa haraka kama ninavyotaka?”
Unakumbuka kitu kinaitwa “GESTATION PERIOD!?” Yaani ule muda tangu ujauzito umetokea hadi mtoto amezaliwa.
Usisahau, kwenye maisha kuna vitu ni MATOKEO YA MUDA.
Yaani ni kama mama mjamzito, haijalishi ana hamu ya mtoto kiasi gani ni lazima asubirie miezi tisa.
Changamoto kubwa utakayokutana nayo utakapotaka kulazimisha, ni kuishia kuharibu kile kizuri ambacho ulipaswa kukipata.
May 8, 2022 • 6 tweets • 1 min read
~Mkumbushe mwanao kuwa WIVU utamfanya amchukie Mtu ambaye alipaswa ajifunze kutoka kwake...
~Mkumbushe Mwanao kuwa Msaada sio Haki yake asipopewa Asinung'unike atafute Chake...
~Mkumbushe Mwanao kuwa Tumeona mazuri kwa watu waliokuwa wakiitwa wabaya na Tumeona mabaya kwa watu waliokuwa wakiitwa wazuri kwahiyo Aishi na kila mtu kwa akili...