ROSA MISTIKA!

Riwaya iliandikwa na Euphrase Kezilahabi na kuchapishwa January 1, 1971, ni kitabu SERIKALI ya Nyerere ilikipiga marufuku sababu zikitajwa maudhui yake yalikuwa ni yenye kudhalilisha (haikuthibitishwa) ukatoliki. Dhehebu ambalo Mwalimu Nyerere alikuwa muumini huko
Watu wanajiuliza, endapo katika riwaya hiyo lingetumika jina la "MwanaAsha" kubeba taswira ya binti Rosa, wakatoliki akiwepo Mwalimu Nyerere wangelikasirika na kuzuia uchapishwaji wa riwaya hiyo ya Euphrase Kezilahabi? Maswali tu, tunajiuliza!
Kanisa katoliki pia likalalamika kwamba Mistika ni moja wapo kati ya sifa za Bikira Maria Mtakatifu (mama wa Yesu). Hivyo ni udhalilishaji kumpa Rosa jina hilo katika riwaya hiyo kwa sababu ni mchafu wa matendo kiwango cha juu katika riwaya hiyo.
Wanawake wa kitanzania nao wakaja juu kwa madai kuwa wamedhalilishwa kupitia matendo ya Rosa yaliyoandikwa kitabuni, inadaiwa kuwa mama mmoja aliwahi kuzimia baada ya kumkuta binti yake akisoma kitabu hicho.
SERIKALI ya Nyerere ikadai kuwa kitabu hicho kinaharibu maadili ya mtanzania kwa kuanika hadharani mambo machafu yasiyoendana na maadili ya mtanzania... Wakapata sababu ya msingi ya kuzuia riwaya hiyo..
Ajabu kabisa, baada ya muda kupita, riwaya hii ya ROSA MISTIKA, inasomwa na wanazuoni na kufundishwa katika vyuo vikuu, Kezilahabi akaendelea kutunga makala ngumu za kiswahili
Riwaya ya Rosa mistika iliandikwa kwa mara ya kwanza mwaka 1971, ilipochapishwa kwa mara ya kwanza, ilipigwa marufuku na wakuu wa chama tawala. Riwaya inamuonesha binti wa Kutoka visiwa vya Ukerewe, katika sura mbali mbali.
Rosa Mistika anaonekana katika riwaya kwa mara ya kwanza akiwa chini ya ulinzi wa bana yake. Baadae anaonekana katika shule ya 'misheni' ambayo ilikuwa ikisimamiwa na watawa wakikatoliki. Baadae akiwa tena chuo cha ualimu akiwa na vituko
Huko akiwa chuo cha ualimu akizunguka miji ya Tanzania, anakutana na ukatili wa maisha ya kisasa. Anashindwa kustahimili vishindo vya maisha hayo kwa sababu awali hakulelewa katika aina hiyo ya maisha. Baadae anaamua kujiua..
Tupate 'summary' kidogo!

Huko kisiwa cha Ukerewe kulikuwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Regina. Regina na jamaa yake waliishi pamoja katika kijiji cha Namagondo. Regina alikuwa mzuri sana lakini alikuwa na bwana aliyemtesa.
Regina alikuwa na binti watano; Rosa Mistika, Flora, Honorata, Stella, na Sperantia. Mume wa Regina aliitwa Zakaria na alitaka sana kupata mtoto wa kiume. Regina alikuwa na mimba sasa na alimwomba Mungu ampe mtoto wa kiume.
Usiku mmoja, Regina alikuwa akila chakula cha jioni pamoja na watoto wake. Alizungumza nao juu ya mambo ya malezi. Baadaye walikwenda kulala. Wakati huo huo, Zakaria alikuwa akirudi kutoka mahali pa kunywa pombe.
Alilewa sana na alimwambia Regina kwamba alitaka kuwaona watoto wake. Watoto waliitwa isipokuwa Rosa kwa sababu Rosa alikuwa ameanza kuwa mtu mzima. Zakaria aliwaambia waimbe na kufanya mazoezi ya kijeshi.
Mara Stella alimwambia baba yake kwamba Rosa alipokea barua pamoja na pesa. Zakaria alikasirika. Hakutaka binti zake watembee na mvulana ye yote. Rosa aliitwa na Zakaria na aliulizwa juu ya barua hiyo.
Rosa hakumtaka babake asome barua yake. Alijaribu kuila, lakini Zakaria alimshika Rosa shingo. Zakaria aliipata barua, akaisoma. Barua ilizungumzia mapenzi na Zakaria alikasirika zaidi.

Alikwenda pamoja na Rosa nyumbani kwa mvulana aliyemwandikia Rosa barua.
Mvulana huyo, aliitwa Charles. Zakaria alimtupia Charles shilingi, akamwambia kwamba hakutaka kumwona tena pamoja na binti yake.

Itaendelea....

Leo baada ya kuleta habari za Mwl, J.K Nyerere, nikakumbuka hii riwaya ya Rosa-Mistika na ubabe wa serikali ya Nyerere kuifungia

#MMM

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Martin Maranja Masese

Martin Maranja Masese Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @IAMartin_

May 23
SINOHYDRO Corporation LTD wamepewa zabuni kujenga mradi wa mwendokadi BRT-3 Gongo la Mboto-Kariakoo (23.6km) kwa $148.1M na wamepewa zabuni hiyo bila ushindani (single source), wakati ujenzi wa BRT 2 (Gerezani -Mbagala) 20.3km wamejenga chini ya kiwango. Hawa wachina wameturoga?
Zingatia, huo ni mkopo kutoka benki ya Dunia (WB). Na serikali ya Tanzania imekopeshwa $246.7 million kwa ajili ya ujenzi wa BRT-3 ($148.1 million) na BRT-4 ($99.9 million). Wanazo. Wakati huo DART wametumia $2.46 million to 77 kulipa wakazi kupisha ujenzi wa 23.6km kwa BRT-3
BRT-1 ni 21km ilijengwa na STRABAG international GmbH, Kimara kwenda Kivukoni, Morocco, Gerezani kupitia Ubungo, ulikuwa mkopo wa AfDB na WB na $154M. Lakini sasa BRT-2 na BRT-3 wamepewa SINOHYDRO ambao BRT-2 wamejenga chini ya kiwango na baadhi ya sehemu barabara imeharibika.
Read 10 tweets
May 21
Katiba yetu hakuna cheo cha “baba wa taifa”. Hakuna kanuni/sheria yeyote imetungwa wananchi kutambua cheo hicho. Sifikirii kama mtakuwa sahihi mkitaka Mwl. Julius Nyerere atambuliwe na wote kwa jina la ‘baba wa Taifa’. Ni Rais wa 1 wa TZ. Historia ya taifa letu ipo kabla yake!
Ni kizazi dhalimu tu ndiyo kinaweza kupewa kila kitu na kukubali bila kuhoji. Neno “kwanini” linaonyesha ustawi wa ubongo. Hili siyo dola la kijeshi, kifalme au kisultani. Hatupokei kila neno na kumeza. Ndiyo, hakuna sheria inayotutaka tumtambue kwa cheo cha “baba wa taifa”. Ipo?
Mwl, kaikuta TAA chini ya Abdulwahid Sykes. AA ineundwa 1929. Nyerere amezaliwa 1922. Anawezaje kuwa baba wa taifa? AA imebadilika kuwa TAA mwaka 1948 na kuwa TANU 1954. Historia ya kudai uhuru wa Tanganyika ineanza miaka mingi kabla ya Nyerere. Katikati ya miaka ya 1920.
Read 14 tweets
May 21
Ukumbi wa Msekwa imefanyika semina, wabunge wamelipwa Shs. 440,000 (Shs. 172.9M). Kuipitisha bajeti ya miundombinu (ujenzi wa lot Na. 6 ya Tabora - Kigoma (411km). Na gharama za ujenzi ni (Sh.11.1bn) kwa kila 1km. 411km mkandarasi atatumia Shs. 4.6T. Kapewa tender bila ushindani.
Mnakumbuka niliwapa simulizi, wizara ya fedha wameingia makubaliano na China Civil Engineering construction corporation kwa utaratibu wa single source (tenda bila ushindani) thamani ya Shs. 6.7 trilioni kwa utaratibu wa manunuzi wa moja kwa moja ‘single source’ bila ushindani?
Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alipewa ujenzi wa lot Na. 5, Isaka – Mwanza (249 km). Miezi 16 amejenga 4.4% pekee na HAKUNA hata kipande kimoja cha reli ameweka katika miezi 16. Mwigulu anasema bungeni kwamba haukuwepo ufadhili wa kifedha. Ni mzaha.
Read 11 tweets
May 19
Tupige kidogo ‘mastori’ ya Mchungaji Christopher Mtikila

Kesi ya kutoa maneno ya uchochezi ambayo ilifunguliwa na Jamhuri dhidi ya Mtikila Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam. Katika Kesi hiyo upande wa jamhuri Ulidai Mtikila alienda kosa Hilo kufuati ImageImage
Kauli aliyoitoa hadharani siku chache baada ya Muasisi wa Taifa la Tanzania, Julius Nyerere kufariki Oktoba 14, 1999 ambapo Mtikila alitamka maneno yafutatayo:

“Marehemu Rais Julius Nyerere alifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi, ni mzoga, nyamafu na ameenda jehanamu” alisema Mtikila.
Mtikila amekuwa akisema maneno hayo siku zote za Maisha yake na mwisho wa siku Kesi hiyo ilifutwa.

Kesi nyingine ya kutoa maneno ya uchochezi alivyoshitakiwa nayo Mtikila Enzi za Uhai wake ni Jamhuri dhidi ya Christopher Mtikila .
Read 113 tweets
Apr 15
Mwigulu Nchemba, mmeingia makubaliano ya awali na kampuni ya China Civil Engineering construction corporation kwa utaratibu wa single source (bila ushindani) yenye thamani ya Shs. 6,698,935,255,040.00 kwa utaratibu wa manunuzi wa moja kwa moja ‘single source’ bila ushindani.
Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alipewa ujenzi wa lot Na. 5, Isaka – Mwanza (249 km). Miezi 16 amejenga 4.4% pekee na HAKUNA hata kipande kimoja cha reli ameweka katika miezi 16. Mwigulu anasema bungeni kwamba haukuwepo ufadhili wa kifedha. Ni mzaha.
Utaratibu wa ‘single source’ ni LAZIMA mkandarasi awe amekidhi vigezo na uwezo. Huyu mkandarasi wa Mwigulu hana sifa hizo. Miezi 16 ameshindwa kupeleka hata ambulance, hakuna usala kwa wafanyakazi, na amefanya kazi kwa 4.4%. Mkandarasi huyu hajakidhi vigezo vya single source.
Read 19 tweets
Apr 14
Upatikanaji pembejeo
Teknolojia duni za Kilimo
Utekelezaji bajeti ya kilimo
Kilimo cha kutegemea Mvua
Ukosefu wa Huduma za Mikopo
Unafuu upatikanaji zana za kilimo
Uhaba wa mafunzo ya kilimo bora
Ukosefu wa masoko kwa shughuli za Kilimo

Malizeni hayo, ndiyo mwage sifa kwa Bashe.
Pia, ambao mnasema Bashe anaupiga mwingi, mtuonyeshe matumizi ya teknolojia katika kupambana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na ukosefu wa masoko. Mnatakiwa mtuonyeshe jinsi mradi wa kilimo utakavyokuwa na mnyororo wa thamani kwa kuweza kuuza bidhaa hata nje ya nchi.
Sekta ya kilimo ya Tanzania - ambayo inachangia karibu theluthi ya Pato la Taifa la nchi na kuajiri asilimia 75 ya idadi ya watu - ina fursa ya kuongeza mapato na kuboresha maisha. Mmekubalianaje? Mnafungamanisha sekta ya kilimo na viwanda na miradi mikubwa iliyopo nchini?
Read 5 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(