Mzee Bakhressa anaishi Masaki lakini maji ya Uhai au lambalamba na chapati zake hauzii majirani zake. Au ulishaona vile vibaiskeli vya lambalamba za Azam vikizunguka Masaki nyumba kwa nyumba?...
Mzee Mengi toka akiwepo mpaka leo hakuwa akiuza maji ya Kilimanjaro kwa ndugu zake au wakwe zake au jirani zake.
Shigongo hauzi magazeti kwa majirani zake maana unaweza kukuta majirani zake wanasoma Daily News na The Citizen na wasijue hata sura ya gazeti la Shigongo ipoje...
Dewji hauzi vitu vyake kwa classmate wake wa zamani au jirani zake. Masanja anauzia mchele majirani?
Lakini wote hao niliowataja wamepiga hatua bila kujali jirani au ndugu au classmate zao wa zamani wananunua au la.
Hiyo ndo akili ya kibiashara....
Tatizo la watu wengi ni kudhani kuwa ukianza kitu chako mfano biashara au ujasiriamali basi ndugu zako na marafiki na majirani ndo wanapaswa kukusapoti. Wasipokusapoti unanuna na kuona hawakutakii mema....
Unawasema na kulalamika.
kuna kitu hujajua bado ukikijua hutataka kuhangaika na makundi hayo ya watu kibiashara.
Kama upo hapo unawaza kuanza biashara na unafikiria kuwauzia jirani zako au ndugu zako basi kajipange upya kwanza. Utakuwa disappointed na kuanza kulaumu watu bure.
Ndiyo maana Mungu alikuumbia ndugu na marafiki wachache kuliko idadi ya watu usiowajua dunia hii.
Ukitaka kupiga hatua kibiashara achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako.......
Masanja hauzi mchele kwa ndugu zake au majirani au marafiki. Anauza kwa watu asiojua wanakotoka. Inawezekana pilau ulilokula Pasaka huenda ni mchele wa Masanja. Wewe ndugu yake au jirani yake?
Diamond hauzi vitu vyake kwa ndugu zake au majirani zake.......
Wanaoshindana kuview nyimbo zake You Tube au kuzidownload wala wala siyo eti rafiki zake. Ni watu tofauti.
Vijana wengi huwa wananiuliza swali: SASA BRO NTAMUUZIA NANI MAANA HUKU NINAKOKAA DUH WATU NI WA HALI YA CHINI KWELI KWELI NA HATA RAFIKI ZANGU YANI BORA MIMI...
Jibu ni moja tu hapa: Ukitaka kupiga hatua katika biashara achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako
Anayezalisha tissue au toilet papers anauzia rafiki zake? Watengeneza furniture huwa wanauza kwa ndugu zao? Sasa why wewe unawaza jirani zako ndo wateja.....
Unakuta mtu anataka kuanza kufuga kuku anataka majirani zake na wafanyakazi wenzake ndo wale kuku wake!. Maana kwanza jirani ataanza kuleta ujirani kwenye biashara yako changa halafu mtaishia kugombana bila kutarajia....
So we anza tu ndugu waje wasije isikukwaze. Kwani mwenye Twitter wewe umejiunga kwa kuwa mna undugu au eti unamsapoti? Kama vipi we acha kujiunga Twitter uone kama atakufa njaa kwa kuwa hutaki kumsapoti.
Kwani hiyo simu uliyonayo unadhani mwenye hiyo kampuni hana ndugu?...
Nilipoanza biashara nilikuwa na list ya rafiki zangu ndugu zangu na majirani. Tena wenye uwezo mzuri. Kila niliyemshirikisha anakwambia tu TUPO PAMOJA 😁😁.Hawakununua. ukisubiri sapoti ya ndugu unaweza kuipata mwaka keshokutwa.
Sasa si utakufa masikini? ...
Ukiwaza kufungua biashara huku unawaza mashosti sijui washkaji utaifunga siku si nyingi afu utasema eti wateja hakuna.
Kweli?
Yani katika nchi yenye watu karibu milioni 60 unaweza kukosa wateja kabisa kweli? Ulichokosa siyo wateja ni maarifa.....
Ukitaka kufanikiwa katika biashara hasa mwanzo fanya kama vile huna ndugu wala majirani. Fanya kwa ajili ya watu wasiokujua. Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako. Wakizileta well and good wasipoleta no problem.....
Unajua marafiki nao huwa ni rahisi kwao kufikiri unawageuza ngazi ya kupandia. Wengi huanza kuona wivu kwa siri kuwa wewe utawazidi kimafanikio ,Cha msingi wewe tengeneza VALUE. Hilo ndo muhimu. Kisha wateja SAHIHI watakuja tena kutoka mbali kweli kweli....
Kitabu kinasema Nabii hupata heshima nje ya nyumbani. Ukisubiri watu wanaokuzunguka ndo wawe wateja hujajua vizuri maana ya neno MTEJA.
Huoni Bar iko Sinza lakini wadau wake ni watu wa Tabataaaa!
Majirani wanaokunywa pombe wanaoishi jirani na hiyo Bar wanaenda kunywea Kinondoni
Kwani mwenye Samaki Samaki hana majirani? Lakini hapo Samaki Samaki wanaokula na kunywa ni jirani zake? No!
Sasa kwa nini wewe unatengeneza sabuni ya maji unafikiri jirani zako ndo wateja? Wasiponunua unaona eti hawataki kukupa sapoti. Nimesema achana na hela za rafiki zako
Utafika mbali sana. Yani ndugu watakuja huko mbele ya safari. Au utashangaa hawatakuja tu milele.
Nadhani sasa umeelewa vizuri japo ndo hivyo inauma kusikia lakini ndovile! 🤔
Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako!.....
Ukifanya hivyo ndo utakuwa umeanza kuelewa shughuli hii ya biashara na ujasiriamali ilivyo. Na utaona amani wala hutakuwa na shida na mtu.
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
KUWA MAKINI NA WATU UNAOWASHIRIKISHA NDOTO ZAKO,MAONO YAKO
Wengi husema ili uweze kufanikisha Ndoto zako basi haina budi kuzizungumza Kwa watu ili ikupe deni la kutimiza
Mimi nasema sio wote wa kuwambia….
Daudi aliwambia Kaka zake juu ya kwenda kumuua Goliath wakamkatisha tamaa na kumwambia arudi nyumbani Kuwa yeye hawezi.
Kuna watu ukiwambia Maono yako watasema hayo Maono ni makubwa huwezi,hivyo watakukatisha tamaa…..
Yusufu mtoto wa mzee Yakobo alivyowambia Kaka zake juu ya Ndoto alizokuwa anaota walijenga chuki juu yake,wakamuita Bwana Ndoto na kumpangia njama ya kumuua hatimaye kumuuza Misri….
Unaanguka.
Unachubuka.
Unapata hasira zaidi.
Na kwa hasira unaamua kusonga mbele zaidi bila kugeuka nyuma.
Majanga baada ya majanga yanakukuta.
Hakuna anayekuona kwamba na wewe ni wa maana au unachofanya ni cha maana sana….
Jasho na maumivu ndo vinakuwa washirika wako wa karibu.
Ndoto zako zinaonekana kama hazitamia tena licha ya mapambano ya muda mrefu.
Unaanza kufikiria kuacha.
Wakati ndo unataka kukata tamaa tu ghafla kuna kama mafanikio kidogo yanakubeep.
Unapata moyo kidogo... unajaribu tena
Mafanikio yanaongezeka kidogo.
Ushagraduate! Akili yako ishakuwa tayari kwa mafanikio makubwa.
Then BOOM!!! Struggle zote zinakulipa pakubwa. Umefanikiwa!
Sasa rafiki...mpaka ufike hapo kwenye "BOOM!!" ujue ushapigana kwa miaka ya kutosha. ….
Naomba niseme kitu kuhusu watu waliofanikiwa huenda kikakusaidia katika safari yako ya mafanikio..✍️
Nimekuwa na kawaida ya kununua na kusoma majarida ya Forbes toka mwaka 2012 kujifunza kuhusu watu waliofanikiwa kiuchumi walianzia wapi na nimegundua Walianzia Chini Sana..
Ghafla MTU anaacha kazi akiwa top. Anaacha. Halafu anaamua kurudi kijijini kwenu halafu anaanza kuwa mchuuzi wa kalamu za wino!
Wewe utamfikiriaje mtu huyo?
Amechanganyikiwa? Amerogwa?...
Wengi wao WALIAMUA kwa makusudi kuanza chini baada ya kuwa maisha yao yamefikia mahali ambapo binadamu wa kawaida angeweza kuridhika
Kwamba mtu amezaliwa familia bora ya kitajiri badala ya kuridhika tu na "kula bata" lakini anahangaika kuliko waliomtangulia. ..
Wanaume huwafuata Wanawake kwa mambo mawili, ambayo ni MAPENZI na SEX. Lakini inapofika hatua ya Kuoa, Wanaume hawaoi kwa sababu ya SEX au MAPENZI, wanaoa kwa sababu ya kutafuta AMANI NA UTULIVU WA NAFSI (STABILITY).
Mwanaume anaweza kukupenda na asikuoe
Mwanaume anaweza kuwa anafanya mapenzi na wewe tena mkadumu kwa muda mrefu lakini asikuoe. Lakini akampata mtu mwingine akamuoa hata kama mahusiano yake na mtu huyo yalikuwa ya miezi miwili.
Wanaume wengi hutizama mbali zaidi pale wanapotaka KUOA. Huwa hawafikirii habari za suti kali za harusi na sherehe ya gharama, vitu ambavyo hufikiriwa zaidi na wanawake kila wanapoiwaza ndoa.
.
Uwezo wa kufanikiwa kimaisha Mungu aliuweka ndani ya kila mmoja wetu na upo katika kuanzia chini. Usitake kuiga uwezo wa wengine, jenga uwezo wako kidogo kidogo. Nimeona watu wengi mno badala ya kujenga uwezo wake kidogo kidogo
Sikia....
Mzee Mengi enzi za uhai wake alikuwa na gazeti linaitwa ALASIRI. Halikuleta faida. Gazeti la Dar Leo vile vile. Jingine liliitwa THIS DAY. Ushindani wa magazeti mengine ulikuwa mkali. Wasomaji wakabadilika. Internet zikaingia nk.
Pamoja na ukongwe wake wote kwenye media industry hayakumpa faida.
Akaachana nayo.
Halafu wewe eti unataka ufundishwe biashara ambayo hutaki kupoteza hela. Kaa na hela zako tu kwa kweli.
Hivi unadhani Novida ilienda wapi. Kama Coca Cola wanakosa soko la bidhaa yao wewe je?