Ukiwa katika changamoto nyingi na huoni wa kukusaidia kabisa... basi jua ndivyo ilivyopaswa kuwa.. yaani kuna kitu Mungu aliweka kwenye kichwa chako anataka ukitumie vizuri. Na ukitii hiyo sauti utajishangaa kuwa kumbe una solution nyingi balaa….
Kwamba kumbe wewe ni creative kuliko ulivyofikiri. Kwamba kumbe wewe una mpaka majibu ya changamoto za wengine wengi tu, na kumbe wewe mshauri na mtia moyo wa wengi waliojikatia tamaa sababu ya umasikini na magonjwa makubwa kuliko wewe sema nivile umekilemeza hicho kichwa….
Je! Una changamoto na unatamani kupata mtu wa kukutia moyo? Unatamani mtu wa kuomba na wewe ili usikate tamaa?
Vizuri Unatamani jambo jema kabisa Lakini sasa unachopaswa kufanya ni kutafuta mtu wa kumtia moyo. Kama wewe unavyohitaji basi kuna wengi zaidi wanahitaji kutiwa moyo…
Jiulize wale ndugu zetu ambao wako Hospital Wamelazwa Baadhi wapo ICU mpaka sasa na wengi hawawezi hata kuongea. Hawawezi kula.Wewe unakula vizuri, Hawawezi kumove. Hawawezi kitu. Wapo tu kitandani na maumivu. Nani anawatia moyo? …
Mtu aliyepata ajari akapoteza fahamu Anatamani kufungua macho kwa mbali. Yanafunguka kwa mbali halafu kwa maumivu. Damu zinamtoka pia usisahau. Anayafumba. Ingawa amepata moyo kidogo. Kwamba bado yupo hai angalau. Anawaza vitu vyake…..
Ndivyo mind ya mwanadamu ilivyo. Anajiuliza NITAPONA KWELI? Ana haki ya kujiuliza hivyo. Pengine anajilaumu kwa nini alipanda pikipiki ile au gari ile? Pengine anajilaumu kwa nini niliamka siku ile? Mwingine anasema ningejua ningebaki kijijini nisingeenda kuishi mjini….
Lakini shida za nyumbani ndizo zilizonipeleka mjini nikafanye kazi ya Boda Boda. Sasa nani atamsaidia mama yangu?
Analia. Kimya kimya. Akilia ndo maumivu yanazidi. Ananyamaza. Uchungu ni mwingi. Na yeye ni binadamu. Anaanza kukata tamaa ya kuishi….
Anatamani kufa. Labda anakumbuka kumwambia Mungu aichukue roho yake na kumsamehe dhambi zake. Labda mateso yamemzidi na hasira moyoni na kujilaumu kuwa sasa wanaomtegemea ndo wataishi kwa tabu na mateso zaidi na anamkasirikia Mungu. Hakuna wa kumtia moyo. Hakuna wa kuomba naye….
Hakuna wa kumwaminisha kuwa bado Mungu anampenda hata katika hilo. Labda mwingine anaweza kufungua macho kidogo na anaona watu wanapita na mavazi meupe na blue. Anajua ni madaktari na manesi. Anatamani aulize DOKTA NITAPONA KWELI lakini mdomo haufunguki…
Macho hayana pazia masikio pia hayana pamba. Pengine ameshafahamu kuwa kuna wenzake waliolazwa wote na wameondoka duniani tayari. Nani wa kumtia moyo?
Halafu wewe unaona shida yako ni kubwa zaidi. Unataka dunia nzima ikutie moyo? Kweli? Hebu TUBU na uwatie moyo wenzako. Tafuta mtu mtie moyo. Wapo. Hata njiani mama anatembeza mchicha. Msalimie tu mpe neno la faraja…..
Nikwambie hakuna kitu kinamtia mtu moyo kama kupewa neno zuri na mtu asiyemfahamu. Unapita na gari sehemu unakutana na mjasiriamali anauza viatu mkononi vingi kweli. Mikono inamuuma. Jasho linamtoka. Unapunguza mwendo unafungua kioo unamwambia RAFIKI USIKATE TAMAA….
SHIKA ELFU MBILI HII YA MAJI MWANGALIE MUNGU UTAFANIKIWA!
Humjui. Hakujui. Na wala hakuna anayekuona.
Huwezi kujua huyo mtu alikuwa anajiuliza atakavyorudi nyumbani kwa mguu. Au hajala anaona bora anywe soda na biskuti apate nguvu kidogo. Anakuona kama MALAIKA….
Anapata moyo. Anaahirisha mawazo mabaya ya kukata tamaa. Au hata ya kujiua! Cause you never know really! Na atakukumbuka for a very long time.
Nakuagiza kwa Jina lake yeye Aliye Juu. Mtafute mtu leo popote hata mtaani. Mtie moyo. Don't ignore….
Kila asomaye post hii akimtia mtu moyo leo basi siku ya leo itakuwa ni kama siku ya kutiana moyo Tanzania. Mtie mtu moyo. Mpigie simu mtu aliyefiwa siku nyingi labda aliondokewa na mwanaye au mzazi wake au mchumba au mke mume au ndugu yake au mtu wake wa muhimu mno….
Mwambie umeona umsalimie tu. I am telling you you will make a big difference.
Pia usisahau kuwaombea . Na wengine wote walio karibu sana na kukata tamaa.
Na ni maombi yangu Mungu akukumbuke na wewe katika shida zako. Asikupungukie.
Leo ukibahatika kushika baadhi ya simu za wapendwa wako utakuta wengi wao wana picha zako nyingi kwenye simu zao lakini hutawaona wakizitumia picha hizo mahali popote pa wazi kukusifu,kukupongeza wala kukutia moyo. ……
Ila wamezitunza tu ili siku moja ambayo wewe hutakuwa unaweza kuona wala kusikia waadike mengi kuhusu wewe ambayo wewe kwa wakati huo hutaweza kuyasoma wala kuyaona wakikusifu.
Kwa Jina la Yesu yeyote ambaye hatakusifia wakati ambao unaona anasubiri kukusifia wakati ambao…
utakuwa huoni asuburi sana kwa Jina la Yesu.
Lolote baya analokuombea aliye adui yako wa siri halitakupata wewe kwa Jina la Yesu.
Ni maombi yangu ya kwamba kabla ya Mwaka huu kuisha Mungu akakutendee mema hata asiyependa kusema kuwa anakufahamu ….
Mzee Bakhressa anaishi Masaki lakini maji ya Uhai au lambalamba na chapati zake hauzii majirani zake. Au ulishaona vile vibaiskeli vya lambalamba za Azam vikizunguka Masaki nyumba kwa nyumba?...
Mzee Mengi toka akiwepo mpaka leo hakuwa akiuza maji ya Kilimanjaro kwa ndugu zake au wakwe zake au jirani zake.
Shigongo hauzi magazeti kwa majirani zake maana unaweza kukuta majirani zake wanasoma Daily News na The Citizen na wasijue hata sura ya gazeti la Shigongo ipoje...
Dewji hauzi vitu vyake kwa classmate wake wa zamani au jirani zake. Masanja anauzia mchele majirani?
Lakini wote hao niliowataja wamepiga hatua bila kujali jirani au ndugu au classmate zao wa zamani wananunua au la.
Hiyo ndo akili ya kibiashara....
KUWA MAKINI NA WATU UNAOWASHIRIKISHA NDOTO ZAKO,MAONO YAKO
Wengi husema ili uweze kufanikisha Ndoto zako basi haina budi kuzizungumza Kwa watu ili ikupe deni la kutimiza
Mimi nasema sio wote wa kuwambia….
Daudi aliwambia Kaka zake juu ya kwenda kumuua Goliath wakamkatisha tamaa na kumwambia arudi nyumbani Kuwa yeye hawezi.
Kuna watu ukiwambia Maono yako watasema hayo Maono ni makubwa huwezi,hivyo watakukatisha tamaa…..
Yusufu mtoto wa mzee Yakobo alivyowambia Kaka zake juu ya Ndoto alizokuwa anaota walijenga chuki juu yake,wakamuita Bwana Ndoto na kumpangia njama ya kumuua hatimaye kumuuza Misri….
Unaanguka.
Unachubuka.
Unapata hasira zaidi.
Na kwa hasira unaamua kusonga mbele zaidi bila kugeuka nyuma.
Majanga baada ya majanga yanakukuta.
Hakuna anayekuona kwamba na wewe ni wa maana au unachofanya ni cha maana sana….
Jasho na maumivu ndo vinakuwa washirika wako wa karibu.
Ndoto zako zinaonekana kama hazitamia tena licha ya mapambano ya muda mrefu.
Unaanza kufikiria kuacha.
Wakati ndo unataka kukata tamaa tu ghafla kuna kama mafanikio kidogo yanakubeep.
Unapata moyo kidogo... unajaribu tena
Mafanikio yanaongezeka kidogo.
Ushagraduate! Akili yako ishakuwa tayari kwa mafanikio makubwa.
Then BOOM!!! Struggle zote zinakulipa pakubwa. Umefanikiwa!
Sasa rafiki...mpaka ufike hapo kwenye "BOOM!!" ujue ushapigana kwa miaka ya kutosha. ….
Naomba niseme kitu kuhusu watu waliofanikiwa huenda kikakusaidia katika safari yako ya mafanikio..✍️
Nimekuwa na kawaida ya kununua na kusoma majarida ya Forbes toka mwaka 2012 kujifunza kuhusu watu waliofanikiwa kiuchumi walianzia wapi na nimegundua Walianzia Chini Sana..
Ghafla MTU anaacha kazi akiwa top. Anaacha. Halafu anaamua kurudi kijijini kwenu halafu anaanza kuwa mchuuzi wa kalamu za wino!
Wewe utamfikiriaje mtu huyo?
Amechanganyikiwa? Amerogwa?...
Wengi wao WALIAMUA kwa makusudi kuanza chini baada ya kuwa maisha yao yamefikia mahali ambapo binadamu wa kawaida angeweza kuridhika
Kwamba mtu amezaliwa familia bora ya kitajiri badala ya kuridhika tu na "kula bata" lakini anahangaika kuliko waliomtangulia. ..