UNAPENDA KUFANYA BIASHARA #LAKINI NI MANGAPI KATIKA HAYA UNAYAJUA KUHUSU BIASHARA?
Makala yangu mojawapo ilieleza AINA za biashara kuwa kuna biashara za aina mbili:
1. Zile zenye uwezo wa kukupa fedha tu 2. Zile zenye uwezo wa kukufanikisha kiuchumi ...
Nilifundisha tena kuhusu MITAJI. Nikasema hakuna mtaji mkubwa wala mdogo yaani hakuna biashara ya mtaji mdogo. Kila biashara ina mtaji kulingana na mahitaji yake na nature ya hiyo biashara. Na pia mtaji wa kwanza siyo pesa bali mawazo yako kichwani.
Nikazumgumzia kuhusu WATEJA nikasema ukitaka kupiga hatua hasa mwanzoni unapokuwa umeanzisha biashara basi epuka pesa na majirani na marafiki na ndugu. Yaani usilazimishe kuuza kwa hao na sababu nyingi nikatoa.
Then nikaongelea BIDHAA au HUDUMA kwamba unatakiwa kuhangaika na UBORA wa bidhaa zako. Yes. Usihangike na washindani wako au wanaokucopy au wanaokucheka.
Hayo na mengine mengi yamewasaidia wengi mno. Lakini mafunzo ya sasa yanalenga kukupa ufahamu wa vitu kadhaa
mfano mawazo sahihi ya biashara. Maana halisi ya kuwa mfanyabiashara. Tofauti ya mfanyabiashara na mjasiriamali na mwekezaje. Na elimu ya mambo ya fedha katika ulimwengu wa biashara maana kuna wengi tu wanaingiza pesa nzuri lakini hawajui kupangilia matumizi yake.
Kujifunza haya na mengi mengine tuma neno #MAFUNZO DM IKO WAZI
Karibu! SANA
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Unakuta mtu ameajiriwa au amejiajiri miaka inaenda hajui kwa nini hapigi hatua kipato hakikui lakini yupo tu hatafuti maarifa ya jinsi gani ya kutumia muda wake wa ziada kutengeneza kipato hata mara mbili ya mshahara wake….
Wengine wanafanya hivyo na wanapiga hatua kubwa hadi wengine wanafikiria sasa kuachana na ajira, unashituka kuacha Ajira Yes kuacha watu wanaacha ,Ni muhimu kujifunza haya mambo. Siasa hazitaisha. Angalia your life. Ukifika 40 years uwe very established.
Wakati wenzako wachache wa rika lako mtakapofika miaka 40 wakati wenzako unasikia amenunua kiwanja Kurasini kwa sh Bilioni mbili kwa ajili ya *kupaki* tu Masemitrela zake kama 20 hivi wewe wakati huo unashangaa Kama Kurasini kumbe kuna viwanja bado?
Unatumiaje muda wako asubuhi hadi jioni. Una ratiba au kiholela tu.
Sikia
Kuna fursa nyingi tu za biashara zipo kila siku. Usipofanya kisa bado "unajipanga" it's up to you. Richard Branson (kama humjui Google kidogo) aliwahi kusema Kama mtu akikushirikisha fursa.....👇
halafu huna hakika kama waweza kuifanya basi SEMA NDIYO KWANZA kisha utajifunza jinsi ya kuifanya huko mbele ya safari".
So fursa zipo nyingi. Usipofanya maisha hayakusubiri wewe. Life must go on. Watu lazima wasafiri, wale, wavae, watume na kupokea pesa, wasuke na kunyoa....
Hawawezi kukusubiri wewe eti unajipanga. Life MUST go on. Wewe kama unajipanga wenzako wanafanya hizo fursa.
Tunaposema nchi zingine zimeendelea KIPIMO cha haraka haraka ni MIUNDOMBINU na HUDUMA ZA JAMII. Ninapoona leo nchi hii kuna #mwendokasi. Hata kama bado iko Dar es Salaam.
Nimeandika makala hii Ina elimu ambayo Hautafundishwa darasani
Miezi kadhaa imepita nilifuatwa na binti mmoja na kaka mmoja. Ni watu Wenye ushawishi mkubwa kwa vijana hapa TWITTER "celebrities". Wote walikuwa na mawazo ya biashara na walitaka niwe "mentors" wao. Nikawaambia sawa
Lakini kabla sijaanza "mentorship" program hii, naomba kila mmoja wenu aandike hilo wazo katika "business plan" na atengeneze mfano au "demo" itokanayo na hilo wazo, kisha atafute angalau wateja 2 ndio tuanze "mentorship". Waliondoka moja kwa moja hawakurudi tena.
Sikuwaambia wale vijana wafanye yote hayo kwa sababu nilikuwa siwezi kuwatengenezea "business plan" au kuwatafutia wateja. Masaa 12 tu kwangu yangetosha kuwapa "business plan" yenye mashiko na ningepiga simu chache tu kwenye "network" yangu kuwaunganisha na wateja.
Kuna mahali huwezi kufika kiuchumi kwa kufanya kazi tu kwa bidii. Bidii yako ni muhimu lakini siyo ticket PEKEE ya kukupeleka katika mafanikio makubwa kiuchumi. Kuna vingine vingi nje ya bidii. Unyenyekevu na kujishusha….
Kujifunza vitu vipya ili ujae maarifa...
Ku-take risks mapema..
Kujifungamanisha kiroho (success is spiritual)... Kuwa na washauri (mentors)... nk.
Hebu jipime kama umeshaanza kuwa na hivyo vitu in your life…..
Kuna siku nimewahi kuwaambia hapa Henry Ford. Ford Motors. Alianza biashara ya kutengeneza magari kwa mtaji wa $28,000. Na pesa zote ALIKOPA. Unaelewa ukubwa wa kampuni ya Ford leo? Leo kampuni ina thamani ya $56 billion na mapato ya $158 billion kwa mwaka.
Kuna dada mmoja kutoka MOSHI (Kilimanjaro) alikuja DM akasema anataka kuanzisha mgahawa wa vyakula mbali mbali vya asili. Wazo zuri kabisa. Dr Badi Nahitaji Ushauri Mzee Wangu,Kwanza swali la kwanza kumuuliza lilikuwa UNAJUA KUPIKA?.....
Akasema ndiyo lakini sitaweza kupika peke yangu vyakula vyote hivyo wakati nafungua biashara.
Ushauri kwake ukawa: nafikiri usianze na kufungua mgahawa huko naona ni mbali sana. Kwa nini usianze kupika kidogo tu nyumbani kwako ambapo...
hutakuwa na gharama ya kodi ya huo mgahawa mpya kwanza. Wala hutakuwa na mishahara ya kulipa. Wala hutakuwa na gharama za kununua viti vya kisasa. Anzia nyumbani ulipopanga. Pika ambia vijana mtaani waje kula..
Katika vitu nilivyojenga tabia ya kufanya kila asubuhi kimojawapo ni kawaida ya kuliangalia jua wakati linapochomoza. Sunrise! Na kuvuta pumzi ndefu katika mapafu yangu na kushukuru kuwa I'M ALIVE TO SEE ANOTHER SUNRISE…….
Na utakubaliana na mimi kuwa hakuna siku jua #limegoma kuchomoza. Every morning jua lina show up kazini. Halitegi wala halichelewi wala halilalamiki kwa nini sehemu nyingine limezibwa na mawingu na sehemu zingine limezibwa na milima mirefu mpaka linachelewa kuonekana…..
Haijalishi nani atakayeliona na nani ambaye hataliona siku hiyo. Haijalishi nani atasikia joto lake na nani hatasikia joto lake nk. Lenyewe litachomoza na kuwaka na kutoa nuru na joto na uhai. Jua linajua influence yake haipo kwenye kuonekana. Kila kiumbe "kinafeel" uwepo wake.