Unatumiaje muda wako asubuhi hadi jioni. Una ratiba au kiholela tu.
Sikia
Kuna fursa nyingi tu za biashara zipo kila siku. Usipofanya kisa bado "unajipanga" it's up to you. Richard Branson (kama humjui Google kidogo) aliwahi kusema Kama mtu akikushirikisha fursa.....👇
halafu huna hakika kama waweza kuifanya basi SEMA NDIYO KWANZA kisha utajifunza jinsi ya kuifanya huko mbele ya safari".
So fursa zipo nyingi. Usipofanya maisha hayakusubiri wewe. Life must go on. Watu lazima wasafiri, wale, wavae, watume na kupokea pesa, wasuke na kunyoa....
Hawawezi kukusubiri wewe eti unajipanga. Life MUST go on. Wewe kama unajipanga wenzako wanafanya hizo fursa.
Tunaposema nchi zingine zimeendelea KIPIMO cha haraka haraka ni MIUNDOMBINU na HUDUMA ZA JAMII. Ninapoona leo nchi hii kuna #mwendokasi. Hata kama bado iko Dar es Salaam.
Naanza kuwaza. Mimi niitumie vipi ili nifanikishe mambo yangu. Flyover zikikamilika mimi binafsi zitanifaidisha vipi kiuchumi. Au ntaishia kupiga picha kama ambavyo wengine walipiga picha daraja la Manzese mpaka lilipokuja la Kigamboni wakapiga nalo picha.......
wakati kuna watu wanapita na magari yao ya kifahari na kuendelea kuboresha maisha yao huku wewe
Maisha ndo haya haya. Mwaka juzi niliandika ujumbe LIFE BEGINS AT 40. Unaweza kuutafuta ili kujifunza jinsi ya kuepuka kupoteza muda.....
Maisha yanasonga. Hayasubiri utayari wa mtu. Wanaofanikiwa ni watu wenye uthubutu wa kujaribu KABLA YA KUWA TAYARI. Get going before you're ready coz you'll never be all ready!
Usipotumia Twitter na mitandao mingine vizuri ni wewe utakayepoteza muda siyo Twitter. Twitter haitakusubiri wewe mpaka siku ujue kutengeneza Page Utaendelea kuwa soko la wengine yani wewe unanunua vitu kila siku ila huna unachoingiza cha maana kupitia bando lako.
Watu wanayaendesha ma Jeep na ma Cadillac na ma Range nk bila shida usipopata hasira ya kupambana ni wewe. Wengine wanunue. Ukisema wewe daladala inatosha kwamba hushindani na mtu sawa. Usilalamike tu kubanwa mbavu na kuibiwaibiwa simu au pochi mlangoni. Vumilia.....
Kuna mashule mazuri ya kisasa yani watoto watatu mwalimu mmoja (siyo zile za watoto 40 mwalimu mmoja) na uangalizi wa mwanao unakuwa wa hali ya juu kweli kweli yapo. Usipopeleka mwanao kisa eti "hali ya uchumi ni ngumu" it's up to you, wenzako wanapeleka😂😂
Hahaaaa 😂😂 nilikuwa IST kufanya reaseach ada chekechea tu milioni 3 kwa mwaka kwa mtoto mmoja. Sauti iko sawa huko? Ukisomesha mtoto mmoja IST toka chekechea hadi amalize High School utalipa si chini ya milioni 800! Ukisomesha wawili je?
Yes wewe ukisema siyo lazima asome IST wenzako wanasema piga ua lazima. 🤓. It's up to you.
kuna watu wako serious sana wapo wanakuja Dm nawafundisha nimekuwa mentor wao hadi raha Nawewe muda ndio huu njoo Dm ujifunze
Weka mipango yako. FANYIA kazi ndoto zako🙏
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Unakuta mtu ameajiriwa au amejiajiri miaka inaenda hajui kwa nini hapigi hatua kipato hakikui lakini yupo tu hatafuti maarifa ya jinsi gani ya kutumia muda wake wa ziada kutengeneza kipato hata mara mbili ya mshahara wake….
Wengine wanafanya hivyo na wanapiga hatua kubwa hadi wengine wanafikiria sasa kuachana na ajira, unashituka kuacha Ajira Yes kuacha watu wanaacha ,Ni muhimu kujifunza haya mambo. Siasa hazitaisha. Angalia your life. Ukifika 40 years uwe very established.
Wakati wenzako wachache wa rika lako mtakapofika miaka 40 wakati wenzako unasikia amenunua kiwanja Kurasini kwa sh Bilioni mbili kwa ajili ya *kupaki* tu Masemitrela zake kama 20 hivi wewe wakati huo unashangaa Kama Kurasini kumbe kuna viwanja bado?
UNAPENDA KUFANYA BIASHARA #LAKINI NI MANGAPI KATIKA HAYA UNAYAJUA KUHUSU BIASHARA?
Makala yangu mojawapo ilieleza AINA za biashara kuwa kuna biashara za aina mbili:
1. Zile zenye uwezo wa kukupa fedha tu 2. Zile zenye uwezo wa kukufanikisha kiuchumi ...
Nilifundisha tena kuhusu MITAJI. Nikasema hakuna mtaji mkubwa wala mdogo yaani hakuna biashara ya mtaji mdogo. Kila biashara ina mtaji kulingana na mahitaji yake na nature ya hiyo biashara. Na pia mtaji wa kwanza siyo pesa bali mawazo yako kichwani.
Nikazumgumzia kuhusu WATEJA nikasema ukitaka kupiga hatua hasa mwanzoni unapokuwa umeanzisha biashara basi epuka pesa na majirani na marafiki na ndugu. Yaani usilazimishe kuuza kwa hao na sababu nyingi nikatoa.
Nimeandika makala hii Ina elimu ambayo Hautafundishwa darasani
Miezi kadhaa imepita nilifuatwa na binti mmoja na kaka mmoja. Ni watu Wenye ushawishi mkubwa kwa vijana hapa TWITTER "celebrities". Wote walikuwa na mawazo ya biashara na walitaka niwe "mentors" wao. Nikawaambia sawa
Lakini kabla sijaanza "mentorship" program hii, naomba kila mmoja wenu aandike hilo wazo katika "business plan" na atengeneze mfano au "demo" itokanayo na hilo wazo, kisha atafute angalau wateja 2 ndio tuanze "mentorship". Waliondoka moja kwa moja hawakurudi tena.
Sikuwaambia wale vijana wafanye yote hayo kwa sababu nilikuwa siwezi kuwatengenezea "business plan" au kuwatafutia wateja. Masaa 12 tu kwangu yangetosha kuwapa "business plan" yenye mashiko na ningepiga simu chache tu kwenye "network" yangu kuwaunganisha na wateja.
Kuna mahali huwezi kufika kiuchumi kwa kufanya kazi tu kwa bidii. Bidii yako ni muhimu lakini siyo ticket PEKEE ya kukupeleka katika mafanikio makubwa kiuchumi. Kuna vingine vingi nje ya bidii. Unyenyekevu na kujishusha….
Kujifunza vitu vipya ili ujae maarifa...
Ku-take risks mapema..
Kujifungamanisha kiroho (success is spiritual)... Kuwa na washauri (mentors)... nk.
Hebu jipime kama umeshaanza kuwa na hivyo vitu in your life…..
Kuna siku nimewahi kuwaambia hapa Henry Ford. Ford Motors. Alianza biashara ya kutengeneza magari kwa mtaji wa $28,000. Na pesa zote ALIKOPA. Unaelewa ukubwa wa kampuni ya Ford leo? Leo kampuni ina thamani ya $56 billion na mapato ya $158 billion kwa mwaka.
Kuna dada mmoja kutoka MOSHI (Kilimanjaro) alikuja DM akasema anataka kuanzisha mgahawa wa vyakula mbali mbali vya asili. Wazo zuri kabisa. Dr Badi Nahitaji Ushauri Mzee Wangu,Kwanza swali la kwanza kumuuliza lilikuwa UNAJUA KUPIKA?.....
Akasema ndiyo lakini sitaweza kupika peke yangu vyakula vyote hivyo wakati nafungua biashara.
Ushauri kwake ukawa: nafikiri usianze na kufungua mgahawa huko naona ni mbali sana. Kwa nini usianze kupika kidogo tu nyumbani kwako ambapo...
hutakuwa na gharama ya kodi ya huo mgahawa mpya kwanza. Wala hutakuwa na mishahara ya kulipa. Wala hutakuwa na gharama za kununua viti vya kisasa. Anzia nyumbani ulipopanga. Pika ambia vijana mtaani waje kula..
Katika vitu nilivyojenga tabia ya kufanya kila asubuhi kimojawapo ni kawaida ya kuliangalia jua wakati linapochomoza. Sunrise! Na kuvuta pumzi ndefu katika mapafu yangu na kushukuru kuwa I'M ALIVE TO SEE ANOTHER SUNRISE…….
Na utakubaliana na mimi kuwa hakuna siku jua #limegoma kuchomoza. Every morning jua lina show up kazini. Halitegi wala halichelewi wala halilalamiki kwa nini sehemu nyingine limezibwa na mawingu na sehemu zingine limezibwa na milima mirefu mpaka linachelewa kuonekana…..
Haijalishi nani atakayeliona na nani ambaye hataliona siku hiyo. Haijalishi nani atasikia joto lake na nani hatasikia joto lake nk. Lenyewe litachomoza na kuwaka na kutoa nuru na joto na uhai. Jua linajua influence yake haipo kwenye kuonekana. Kila kiumbe "kinafeel" uwepo wake.