Zambia walichagua bilionea wao kuwa Rais. Hakainde Hichilema, HH - “Bally”, Wanamuita “cattle boy” anatajwa kuwa bilionea mkubwa Zambia. Anamiliki ranchi nambari mbili kwa ukubwa nchini Zambia. HH ana utajiri wa zaidi ya US$389M. Wengine tukomae na “watoza ushuru” wenye vilemba.
Hakainde Hichilema ni MFUGAJI mkubwa,pia anafanya shughuli za kilimo cha mahindi. Hichilema anashika nambari mbili nchini Zambia kwa kusafirisha nyama baada ya ZAMBEEF. Anasema alianza na ng’ombe 6 na sasa anao ng’ombe zaidi ya milioni 5.
July 2013 katika ranchi yake iliyopo wilaya ya Namwala, jimbo la Kusini, aliibiwa ng’ombe wake zaidi ya 500. Hii mwaka 2013 ilikuwa na thamani Kwacha Bilioni 1. Shamba hilo lipo chini ya kampuni ya HH FARMS Ltd. Huyu ni mfugaji mkubwa. Bilionea.
Hakainde HICHILEMA anatajwa kutoa ajira kwa watu zaidi ya 2,500, katika shughuli zake za ufugaji na kilimo, tofauti na kwetu ambapo watawala wanaomba nafasi wakatajirike ofisini wakati huo wakituita “wanyonge” na sisi tukishangilia kunasibishwa na unyonge katika umaskini.
Zambia wanaona kuna sababu za msingi za kuwa na kiongozi wa taifa mwenye uchumi binafsi imara, Tanzania bado tunadhani kiongozi wa nchi anatakiwa kuwa maskini ili atuite wanyonge, tufurahi. Umaskini Tanzania umefanywa kuwa sifa inayovutia. wameufanya kuwa mtaji wa kuomba kura.
Maana yangu ni kwamba katika ulimwengu huu wenye ladha za ubepari na soko huria tunahitaji watu ambao wanakwenda kwenye ofisi za umma kuongeza ubunifu na sio kujilimbikizia mali na majengo kijiji kwao. Hatuhitaji watu wenye kujenga viwanja vya ndege kijiji kwao.
Hakainde Hichilema Siku ya pili ofisini, akateua timu ya wataalam kufanya tathmini mfumo wa kodi na kufanyiwa mabadiliko ili kuondoa kasoro ambazo zimesababishwa na (utawala wa kikatili wa Edgar Lungu katika uchumi). Wakati Tanzania ndiyo kodi na tozo sasa zinamwagika kwa Raia.
Maskini hawawezi kuwa chanzo cha mapato halali ya serikali. Tena hawa maskini unawalimbikizia mzigo wa kodi, Akili za watawala wa Tanzania zinafikiria kuwapa kodi mpya watanzania. Waziri anaamini ili serikali ipate mapato, lazima iwakamue hao wanaoitwa 'maskini'
Zambia kumchagua Hakainde Hichilema, moja kati ya bilionea mkubwa Zambia kuwa Rais wa saba wa nchi yaoinaweza isiwe hoja, ya msingi sana lakini angalia uzalendo wake wa kuwekeza ndani na kuajiri wazambia. Amekataa hata kununua magari ya kifahari serikalini.
Hakainde Hichilema gawezi kwenda ofisini kuwa “mchuma fedha za umma” ambazo anazo nyingi, kwa hili wataepuka hadithi za ujenzi kama ule uliofanyika CHATO kwa maelekezo maalum. Uwanja wa ndege Chato, nani anautumia sasa?

#MMM, Martin Maranja Masese
Mtikila, August 2022

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Martin Maranja Masese

Martin Maranja Masese Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @IAMartin_

Jun 14
Mzee @MsigwaPeter anasema Maasai siyo wazawa. Tukubaliane naye. Msigwa ni mhehe wa Iringa, Je wahehe ni wazawa wa Iringa au tumpe darasa mchungaji? Hawa ni wabantu. Shina la Wahehe linaanzia kwa mtu aliyeitwa Mufwimi (yaani Mwindaji), simulizi zinaeleza alitokea Ethiopia.
Mufwimi alipita akiwinda kutoka Ethiopia, Kenya kabla ya kuingia Tanganyika na kujikuta yupo Usagara na hatimaye eneo la Nguluhe-Dabaga akipitia Ikombagulu, himaya ya Chifu Mwamududa ambaye alikuwa akitawala kabila la Wakombagulu, lililokuwa na watu wachache.
Simulizi zinaeleza, wengi walimfananisha Mufwimi na mtu wa kabila la Wakamba kutoka Kenya kutokana na umbile lake kubwa. Wakati huo eneo ambalo sasa linaitwa Iringa lilikuwa na makabila mbalimbali kama; Walikuwepo: Wahafiwa, Vanyategeta, Vanyakilwa, Vasavila, Vadongwe
Read 7 tweets
Jun 5
Siku nilikamatwa na polisi mahakama ya mwanzo Tarime. Nikapelekwa mahabusu. Nikatunzwa siku 12. Nikasafirishwa DSM nilipotunzwa siku 11. Tarime mahakamani siku nakamatwa, hakuna aliyejitikisa kunipambania. Moyoni nikajisemea “ni kiherehere changu kujifanya Ernesto ‘Che’ Guevara”
Baada ya kupewa dhamana nikatakiwa kufika kituo cha polisi mara 2 kwa kila siku 7 miezi 3 mfululizo. Mara zote nikiwa njiani naona watu wapo bizee na biashara zao. Nikawa najisemea “kujifanya Stokely Carmichael kunaniponza, walimwengu hawana habari wanaendelea na shughuli zao tu”
Hilo pia nimeliona wakati wa kesi ya Freeman Mbowe. FAM amebebwa kwenye karandinga saa 11 jioni ile, ijumaa jioni kuna bar pale Sinza imeshona, watu wengi wanakula bia na muziki. FAM anatikisa kichwa nadhani na kujisemea “tunaowapambania wao wanapambana kufungua vizibo kwa mdomo”
Read 5 tweets
Jun 1
JPM pamoja na uharibifu na ukatili wake alikuwa ni fursa. Wakati wote nasema, JPM alichelewa kutawala ardhi yetu. Nimeeleza. Alitusaidia mambo mengi kwa kutumia udikteta wake. Tulishughulikiwa na kuimarika sana. Tukashikamana na kuwa imara. Tuliwafahamu hadi matapeli ndani yetu.
Ni ukweli dhahiri. Ni tabia za binadamu wote. Kadiri anapoumizwa ndivyo anavyochukizwa. Ni kama alivyo mnyama Paka. Ni kiumbe mpole sana. Huwezi kumuona akigombana na wenzake hovyo. Lakini ukimfungia chumbani, ukampiga, utaona upande wake wa pili. Wataalam wanaita “Apathy spirit”
Wakati wa SSH, tunacheka pamoja ikulu, tunakutana Serena, wakati huo CHADEMA hawaruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara, CCM wanakusanya wanachama mikoani viongozi wake wakuu wanazunguka. Utashiriki vipi uchaguzi wakati ulikuwa likizo miaka 5 yote ukicheka na mwenyekiti wa CCM?
Read 17 tweets
Jun 1
Nimekumbuka makala ya “Collective Imbecilization” Profesa Chachage imeandikwa na Jenerali Twaha Ulimwengu….

Neno “Imbecilization” usilitafute katika kamusi ya kiingereza kwa kuwa hilo ni neno alilotengeneza Profesa Seithy Chachage mwenyewe. Alikuwa binadamu akili nyingi.
Hili jaribio la kuwapumbaza watu mamilioni kwa mpigo. Ni kama vile ingewezekana kuwakusanya watu milioni 50, ukawaweka ndani ya ukumbi mmoja kwa ukubwa huo, ukafunga madirisha na milango, kisha ukawanyunyizia dawa ya uzuzu, ubwege na ufala, ikawakolea sawasawa,
kabla hujawaachia waende Duniani waendelee shughuli zao. Hiyo ndiyo Chachage aliita “collective imbecilization”

Dhahiri hiyo haiwezekani katika mazingira ya kawaida. Isipokuwa inawezekana watu wakapumbazwa kwa pamoja, wakafanywa mazuzu kwa pamoja, wakageuzwa mabwege kwa pamoja
Read 7 tweets
May 31
Mwaka 2013 Club Billicanas ilifunguliwa baada ya ukarabati wa gharama kufanyika. Ilikuwa ni uwezo wako wa kunywa/kula siku hiyo. Freeman Mbowe alilipa bili zote. 2015 anaingia mwendazake madarakani, anaanza vibweka, 2017 BILLZ inavunjwa kwa unyama. Mwendazake alikuwa katili sana.
Picha ya kwanza Club BILLZ ikiwa na uhai wake. Show kubwa za wasanii wa ‘bongo fleva’ zilifanyika hapo. Frame ya pili ni baada ya Club Billicanas kubomolewa kwa hila tu, sababu nyingi zikiwa za kisiasa. Watu wengi wakakosa ajira. Eneo hilo sasa ni parking tu ya magari. Roho mbaya
Mbowe Hotels ambao walikuwa wapangaji wa muda mrefu kwenye jengo hilo ambapo mbali ya kuendesha Club Bilicanas pia kulikuwa na ofisi za gazeti la Tanzania Daima. Mwendazake alibomoa na hakujali mali na samani zilizokuwa ndani. Ilikuwa ni mbaya sana. Uharibifu ulikuwa mkubwa.
Read 10 tweets
May 23
SINOHYDRO Corporation LTD wamepewa zabuni kujenga mradi wa mwendokadi BRT-3 Gongo la Mboto-Kariakoo (23.6km) kwa $148.1M na wamepewa zabuni hiyo bila ushindani (single source), wakati ujenzi wa BRT 2 (Gerezani -Mbagala) 20.3km wamejenga chini ya kiwango. Hawa wachina wameturoga?
Zingatia, huo ni mkopo kutoka benki ya Dunia (WB). Na serikali ya Tanzania imekopeshwa $246.7 million kwa ajili ya ujenzi wa BRT-3 ($148.1 million) na BRT-4 ($99.9 million). Wanazo. Wakati huo DART wametumia $2.46 million to 77 kulipa wakazi kupisha ujenzi wa 23.6km kwa BRT-3
BRT-1 ni 21km ilijengwa na STRABAG international GmbH, Kimara kwenda Kivukoni, Morocco, Gerezani kupitia Ubungo, ulikuwa mkopo wa AfDB na WB na $154M. Lakini sasa BRT-2 na BRT-3 wamepewa SINOHYDRO ambao BRT-2 wamejenga chini ya kiwango na baadhi ya sehemu barabara imeharibika.
Read 10 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(