February 2018, Kampuni za umeme, Australia zilitakiwa kulipa fidia kwa wakazi wa jimbo la Victoria, nchini Australia waliothirika kwa kukosa umeme, malipo ya $180 kutegemeana na muda ambao 'nyumba ilikosa umeme'. Zilitengwa $5M. Umeme ulikatika kati ya saa 3-20.
Huku kwetu, umeme unakatwa bila taarifa, hakuna anaejali, ni wewe mwananchi kujitetea tena ukibembeleza waurudishe. Vinyozi, wachomelea vyuma, mafundi aluminum, wachapaji, banks etc hasara ni zao sio vinginevyo, nani wa kuwatetea? Nani wa kuwalipa fidia kwa hasara yao?
Serikali iruhusu uwekezaji wa kampuni binafsi za kutoa huduma za umeme, TANESCO ni kama wameshindwa hii kazi kabisa. Nchi inakosa umeme tangu asubuhi hadi usiku? Mnajichekesha tu.. Nchi yetu tumekabidhi kwa watu wasiokuwa na sera, mikakati na blueprint za kuendesha nchi.
Tufanye kama Singapore. Sekta ya umeme ipo chini ya Singapore Power. Wanatoa huduma za umeme na gesi, wanasambaza huduma, kwa wateja wake. Ni moja kati ya shirika kubwa Singapore. Sasa hawa SP wako na 'mashirika tanzu' ambao wanawasaidia kufanya huduma zao.
Mfano; PowerGas, AusNet Services, SP PowerGrid, SP powerAssets, SP Telecom, SP service, Nje ya hapo kuna SP anbao wanafanya kazi zao kwa ushirikiano na kampuni nyingine, mfano; Power Automation hawa wanahusika kutoa msaada wa huduma za uhandisi katika ulinzi wa Mifumo
Katika vituo poozo vya umeme na usimamizi wa nishati na mfumo wa Taarifa nchi nzima. Pia wapo Singapore District Cooling (SDC). Wanajihusisha na uzalishaji na usambazaji wa maji baridi kwa Majengo ya biashara. Serikali yenu ikajifunze vitu hivi kutoka Singapore na Malaysia.
November 2011, Singapore waliunganisha zaidi ya 80% ya huduma ya gesi katika kampuni za uzalishaji nguvu ambayo iliingizwa na kubadilisha gesi kwenda katika umeme na kujaza katika gridi ya taifa. 20% inayobaki inatoka kwenye mafuta na vyanzo vingine kama taka na nishati mbadala.
Mtasema Singapore ni wakongwe, basi tutumie mfano wa Malaysia. Nchi ambayo tunalingana nayo umri. Kwa mujibu wa 'tume ya nishati' kuna zaidi ya watoa huduma na wazalishaji wakubwa 18, ingawa wasambazaji wa nishati Malaysia wapo chini ya Udhibiti wa Serikali
Idara ya gesi na umeme inahusika na masuala ya kupanga na kuratibu bei na kanuni. Fedha ya mmtej inaendesha shirika la umeme Tanzania na nyingine inatumika kwenye REA na TRA huko. Tena mteja anatoa fedha ya malipo kabla ya matumizi (prepaid). Kwanini mteja adhulumiwe haki yake?
Umeme unakatika siku nzima wakati mteja amelipia huduma kwa ajili ya matumizi yake? Ofisi za serikali na hata Ikulu ni wateja wa TANESCO wa Post-paid, hawana shuruba hizi wanazokutana nazo wateja wa kawaida wa TANESCO wa Pre-paid. Umeme kwao haukatiki kwa sababu ya LUKU.
Miaka 60 baada ya uhuru bado kuna zaidi ya nyumba milioni 37 hazina umeme. 32% ya watanzania ndio pekee yenye kutumia umeme wa TANESCO. Vijijini 17% na mjini 65%. Zingatia, vijijini ndio kuna wakazi wengi kuliko mjini. Rural population 64.05% (taarifa ya benki ya Dunia, 2021)
Bajeti wizara ya Nishati 2022/23, waziri January Makamba anasema vitongoji 37,610 kati ya vitongoji 64,760 Tanzania havijafikiwa na umeme na watahitaji Sh6.50 trilioni na miaka 15 kuvifikia. Fikiria kuna watanzania wataishi bila umeme kwa miaka 15 mingine, Makamba akiwa wizarani!
Mfumo wa manunuzi ya umeme hauna backup? TANESCO wanapokea kodi kutoka kila transaction ya kununua umeme, waboreshe sasa mfumo huo. Hizi hasara za siku 3-4 nani atafidia kwa wananchi? Mtumiaji analipa VAT, EWURA, REA katika fedha anayonunua umeme. Sio hisani. Tunataka huduma bora
Mfano, ukinunua umeme kwa njia ya mitandao ya simu, umeme wa Tsh 1,000/- Cost (gharama) 819.68, VAT (kodi ya ongezeko la thamani) 18%—147.53, EWURA (Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji) 1%—8.20, REA (wakala wa umeme vijijini) 3%—24.59, TOTAL 1,000.00
Kwa miaka zaidi ya 60, tumetoka UTUMWANI kimwili, kiakili bado tupo UTUMWANI kwa wakoloni WEUSI. Wananchi sisi MZIGO. Tunawekwa gizani, tunakosa kununua LUKU lakini tunashindwa kuiwajibisha serikali kwa uzembe wake. Leo watu walipaswa kuwajibishwa.

#MMM, Martin Maranja Masese

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Martin Maranja Masese

Martin Maranja Masese Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @IAMartin_

Aug 17
Zambia walichagua bilionea wao kuwa Rais. Hakainde Hichilema, HH - “Bally”, Wanamuita “cattle boy” anatajwa kuwa bilionea mkubwa Zambia. Anamiliki ranchi nambari mbili kwa ukubwa nchini Zambia. HH ana utajiri wa zaidi ya US$389M. Wengine tukomae na “watoza ushuru” wenye vilemba.
Hakainde Hichilema ni MFUGAJI mkubwa,pia anafanya shughuli za kilimo cha mahindi. Hichilema anashika nambari mbili nchini Zambia kwa kusafirisha nyama baada ya ZAMBEEF. Anasema alianza na ng’ombe 6 na sasa anao ng’ombe zaidi ya milioni 5.
July 2013 katika ranchi yake iliyopo wilaya ya Namwala, jimbo la Kusini, aliibiwa ng’ombe wake zaidi ya 500. Hii mwaka 2013 ilikuwa na thamani Kwacha Bilioni 1. Shamba hilo lipo chini ya kampuni ya HH FARMS Ltd. Huyu ni mfugaji mkubwa. Bilionea.
Read 10 tweets
Jun 14
Mzee @MsigwaPeter anasema Maasai siyo wazawa. Tukubaliane naye. Msigwa ni mhehe wa Iringa, Je wahehe ni wazawa wa Iringa au tumpe darasa mchungaji? Hawa ni wabantu. Shina la Wahehe linaanzia kwa mtu aliyeitwa Mufwimi (yaani Mwindaji), simulizi zinaeleza alitokea Ethiopia.
Mufwimi alipita akiwinda kutoka Ethiopia, Kenya kabla ya kuingia Tanganyika na kujikuta yupo Usagara na hatimaye eneo la Nguluhe-Dabaga akipitia Ikombagulu, himaya ya Chifu Mwamududa ambaye alikuwa akitawala kabila la Wakombagulu, lililokuwa na watu wachache.
Simulizi zinaeleza, wengi walimfananisha Mufwimi na mtu wa kabila la Wakamba kutoka Kenya kutokana na umbile lake kubwa. Wakati huo eneo ambalo sasa linaitwa Iringa lilikuwa na makabila mbalimbali kama; Walikuwepo: Wahafiwa, Vanyategeta, Vanyakilwa, Vasavila, Vadongwe
Read 7 tweets
Jun 5
Siku nilikamatwa na polisi mahakama ya mwanzo Tarime. Nikapelekwa mahabusu. Nikatunzwa siku 12. Nikasafirishwa DSM nilipotunzwa siku 11. Tarime mahakamani siku nakamatwa, hakuna aliyejitikisa kunipambania. Moyoni nikajisemea “ni kiherehere changu kujifanya Ernesto ‘Che’ Guevara”
Baada ya kupewa dhamana nikatakiwa kufika kituo cha polisi mara 2 kwa kila siku 7 miezi 3 mfululizo. Mara zote nikiwa njiani naona watu wapo bizee na biashara zao. Nikawa najisemea “kujifanya Stokely Carmichael kunaniponza, walimwengu hawana habari wanaendelea na shughuli zao tu”
Hilo pia nimeliona wakati wa kesi ya Freeman Mbowe. FAM amebebwa kwenye karandinga saa 11 jioni ile, ijumaa jioni kuna bar pale Sinza imeshona, watu wengi wanakula bia na muziki. FAM anatikisa kichwa nadhani na kujisemea “tunaowapambania wao wanapambana kufungua vizibo kwa mdomo”
Read 5 tweets
Jun 1
JPM pamoja na uharibifu na ukatili wake alikuwa ni fursa. Wakati wote nasema, JPM alichelewa kutawala ardhi yetu. Nimeeleza. Alitusaidia mambo mengi kwa kutumia udikteta wake. Tulishughulikiwa na kuimarika sana. Tukashikamana na kuwa imara. Tuliwafahamu hadi matapeli ndani yetu.
Ni ukweli dhahiri. Ni tabia za binadamu wote. Kadiri anapoumizwa ndivyo anavyochukizwa. Ni kama alivyo mnyama Paka. Ni kiumbe mpole sana. Huwezi kumuona akigombana na wenzake hovyo. Lakini ukimfungia chumbani, ukampiga, utaona upande wake wa pili. Wataalam wanaita “Apathy spirit”
Wakati wa SSH, tunacheka pamoja ikulu, tunakutana Serena, wakati huo CHADEMA hawaruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara, CCM wanakusanya wanachama mikoani viongozi wake wakuu wanazunguka. Utashiriki vipi uchaguzi wakati ulikuwa likizo miaka 5 yote ukicheka na mwenyekiti wa CCM?
Read 17 tweets
Jun 1
Nimekumbuka makala ya “Collective Imbecilization” Profesa Chachage imeandikwa na Jenerali Twaha Ulimwengu….

Neno “Imbecilization” usilitafute katika kamusi ya kiingereza kwa kuwa hilo ni neno alilotengeneza Profesa Seithy Chachage mwenyewe. Alikuwa binadamu akili nyingi.
Hili jaribio la kuwapumbaza watu mamilioni kwa mpigo. Ni kama vile ingewezekana kuwakusanya watu milioni 50, ukawaweka ndani ya ukumbi mmoja kwa ukubwa huo, ukafunga madirisha na milango, kisha ukawanyunyizia dawa ya uzuzu, ubwege na ufala, ikawakolea sawasawa,
kabla hujawaachia waende Duniani waendelee shughuli zao. Hiyo ndiyo Chachage aliita “collective imbecilization”

Dhahiri hiyo haiwezekani katika mazingira ya kawaida. Isipokuwa inawezekana watu wakapumbazwa kwa pamoja, wakafanywa mazuzu kwa pamoja, wakageuzwa mabwege kwa pamoja
Read 7 tweets
May 31
Mwaka 2013 Club Billicanas ilifunguliwa baada ya ukarabati wa gharama kufanyika. Ilikuwa ni uwezo wako wa kunywa/kula siku hiyo. Freeman Mbowe alilipa bili zote. 2015 anaingia mwendazake madarakani, anaanza vibweka, 2017 BILLZ inavunjwa kwa unyama. Mwendazake alikuwa katili sana.
Picha ya kwanza Club BILLZ ikiwa na uhai wake. Show kubwa za wasanii wa ‘bongo fleva’ zilifanyika hapo. Frame ya pili ni baada ya Club Billicanas kubomolewa kwa hila tu, sababu nyingi zikiwa za kisiasa. Watu wengi wakakosa ajira. Eneo hilo sasa ni parking tu ya magari. Roho mbaya
Mbowe Hotels ambao walikuwa wapangaji wa muda mrefu kwenye jengo hilo ambapo mbali ya kuendesha Club Bilicanas pia kulikuwa na ofisi za gazeti la Tanzania Daima. Mwendazake alibomoa na hakujali mali na samani zilizokuwa ndani. Ilikuwa ni mbaya sana. Uharibifu ulikuwa mkubwa.
Read 10 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(