Naam! Kazi muhimu ya chama cha upinzani katika nchi ya kidemokrasia yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa ni kuikosoa serikali iliyopo madarakani. Jukumu la kumwaga pongezi lifanywe na tabaka dola na wafuasi wao. Wapinzani wafanye kazi ya kunadi sera zao mbadala kwa umma. #MMM
Hoja za wapinzani zijibiwe kwa hoja. Viongozi wasitoke kuwatishia au kutoa maagizo ya kuwakamata wapinzani wao kwa sababu wanaikosoa serikali iliyopo madarakani. Huo ni wajibu wa upinzani timamu. Hoja zijibiwe kwa hoja. Kiongozi huwezi kujibu hoja za wapinzani, jikaushe #MMM
Baada ya serikali kukusanya kodi, inatakiwa maendeleo ya kijamii yaonekane kwa macho. Wapinzani wa watawala mtapaswa kuhoji kwanini hakuna maendeleo? Mkianza kuwasifu watawala mnapoteza uhalali mbele ya umma na mtaadhibiwa kihalali katika uchaguzi kama sehemu ya dola. #MMM
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
. @JMakamba Tatizo ni kanuni za EWURA, Sheria ya mafuta, EWURA au Wizara?
Kituo cha Mafuta Mvumi Mission, Chamwino, Dodoma, leo asubuhi bei ya Mafuta ni Sh.3,475 kwa lita ya petroli.
@EwuraTanzania wametoa bei kikomo lita ya Petroli ni Sh.3,023 Chamwino, Dodoma kuanzia 7/9/2022
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei
za bidhaa za mafuta ya petroli zinapangwa na soko lenyewe. EWURA Jukumu lao litakuwa ni kuhahamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa
za mafuta kwa kampuni za mafuta ambazo zipo 39.
Lakini kampuni hizo (39) za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (price cap) au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa (floor price) kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na Kanuni za EWURA.
Bashungwa anasema vituo vya afya 234 vimejengwa kwa tozo. April 4,2019 walitueleza Magufuli amejenga 352. Hotuba ya Magufuli bungeni 2020 walisema wamejenga vituo 487. Sept 2021 wakasema Samia wamejenga vituo 220 kwa tozo. Mkopo IMF kwa ajili ya COVID-19 $567.25M mlipeleka wapi?
Ukiacha kwamba kukopa ili kutengeneza madawati ni jambo la hovyo. Fedha za IMF mlizipeleka kwenye jukumu ambalo siyo lake. Madawati na Madarasa sio kazi ya mikopo ya IMF. Hizo ni kazi kimaendeleo chini ya WB. Tanzania iliomba fedha IMF kukabiliana na dharura ya COVID-19.
IMF ni short term interventions nchi inapokabiliwa na changamoto za balance of payments; au ku' boost matumizi ya serikali linapotokea janga la kuathiri vyanzo vya mapato nchi husika; au zinapotokea emergencies (natural/human disasters) na kuathiri uzalishaji na uchumi kwa ujumla
February 2018, Kampuni za umeme, Australia zilitakiwa kulipa fidia kwa wakazi wa jimbo la Victoria, nchini Australia waliothirika kwa kukosa umeme, malipo ya $180 kutegemeana na muda ambao 'nyumba ilikosa umeme'. Zilitengwa $5M. Umeme ulikatika kati ya saa 3-20.
Huku kwetu, umeme unakatwa bila taarifa, hakuna anaejali, ni wewe mwananchi kujitetea tena ukibembeleza waurudishe. Vinyozi, wachomelea vyuma, mafundi aluminum, wachapaji, banks etc hasara ni zao sio vinginevyo, nani wa kuwatetea? Nani wa kuwalipa fidia kwa hasara yao?
Serikali iruhusu uwekezaji wa kampuni binafsi za kutoa huduma za umeme, TANESCO ni kama wameshindwa hii kazi kabisa. Nchi inakosa umeme tangu asubuhi hadi usiku? Mnajichekesha tu.. Nchi yetu tumekabidhi kwa watu wasiokuwa na sera, mikakati na blueprint za kuendesha nchi.
Zambia walichagua bilionea wao kuwa Rais. Hakainde Hichilema, HH - “Bally”, Wanamuita “cattle boy” anatajwa kuwa bilionea mkubwa Zambia. Anamiliki ranchi nambari mbili kwa ukubwa nchini Zambia. HH ana utajiri wa zaidi ya US$389M. Wengine tukomae na “watoza ushuru” wenye vilemba.
Hakainde Hichilema ni MFUGAJI mkubwa,pia anafanya shughuli za kilimo cha mahindi. Hichilema anashika nambari mbili nchini Zambia kwa kusafirisha nyama baada ya ZAMBEEF. Anasema alianza na ng’ombe 6 na sasa anao ng’ombe zaidi ya milioni 5.
July 2013 katika ranchi yake iliyopo wilaya ya Namwala, jimbo la Kusini, aliibiwa ng’ombe wake zaidi ya 500. Hii mwaka 2013 ilikuwa na thamani Kwacha Bilioni 1. Shamba hilo lipo chini ya kampuni ya HH FARMS Ltd. Huyu ni mfugaji mkubwa. Bilionea.
Mzee @MsigwaPeter anasema Maasai siyo wazawa. Tukubaliane naye. Msigwa ni mhehe wa Iringa, Je wahehe ni wazawa wa Iringa au tumpe darasa mchungaji? Hawa ni wabantu. Shina la Wahehe linaanzia kwa mtu aliyeitwa Mufwimi (yaani Mwindaji), simulizi zinaeleza alitokea Ethiopia.
Mufwimi alipita akiwinda kutoka Ethiopia, Kenya kabla ya kuingia Tanganyika na kujikuta yupo Usagara na hatimaye eneo la Nguluhe-Dabaga akipitia Ikombagulu, himaya ya Chifu Mwamududa ambaye alikuwa akitawala kabila la Wakombagulu, lililokuwa na watu wachache.
Simulizi zinaeleza, wengi walimfananisha Mufwimi na mtu wa kabila la Wakamba kutoka Kenya kutokana na umbile lake kubwa. Wakati huo eneo ambalo sasa linaitwa Iringa lilikuwa na makabila mbalimbali kama; Walikuwepo: Wahafiwa, Vanyategeta, Vanyakilwa, Vasavila, Vadongwe
Siku nilikamatwa na polisi mahakama ya mwanzo Tarime. Nikapelekwa mahabusu. Nikatunzwa siku 12. Nikasafirishwa DSM nilipotunzwa siku 11. Tarime mahakamani siku nakamatwa, hakuna aliyejitikisa kunipambania. Moyoni nikajisemea “ni kiherehere changu kujifanya Ernesto ‘Che’ Guevara”
Baada ya kupewa dhamana nikatakiwa kufika kituo cha polisi mara 2 kwa kila siku 7 miezi 3 mfululizo. Mara zote nikiwa njiani naona watu wapo bizee na biashara zao. Nikawa najisemea “kujifanya Stokely Carmichael kunaniponza, walimwengu hawana habari wanaendelea na shughuli zao tu”
Hilo pia nimeliona wakati wa kesi ya Freeman Mbowe. FAM amebebwa kwenye karandinga saa 11 jioni ile, ijumaa jioni kuna bar pale Sinza imeshona, watu wengi wanakula bia na muziki. FAM anatikisa kichwa nadhani na kujisemea “tunaowapambania wao wanapambana kufungua vizibo kwa mdomo”