"MAKUBALIANO YA FEDHEHA"

Julai 2019 Barrick Gold corporation ilinunua kampuni ya ACACIA Mining Plc kwa $428M. Hii ni baada ya mjadala wa muda mrefu kati ya BARRICK na ACACIA takribani miezi 5 ya mazungumzo BARRICK na ACACIA wakakubaliana thamani ya kampuni ya ACACIA ni $951M
Awali majadiliano kati ya serikali na BARRICK yaliyofanyika Tanzania yaligomewa na ACACIA na wanahisa wengine wa ACACIA ambao wanamiliki karibu 36% ya hisa zote za ACACIA. Serikali iligoma kwenda mezani na ACACIA, wakaamua kukaa na BARRICK Gold Corporation
Utaratibu wa wanahisa ndani ya ACACIA ni tofauti na kampuni nyingi, BARRICK ambaye ana hisa nyingi (74%) haingii kwenye mjadala kujadili makubaliano yake na serikali dhidi ya ACACIA. Wanahisa wengine wanayo nguvu ya kuweza kukataa mapendekezo ya BARRICK.
Mgogoro ulikuwa katika Mgodi wa Bulyanhulu na Buzwagi (ambao uzalishaji upo mwisho), CHINA walikuwa tayari kulipa gharama na fidia zote kwa BARRICK kununua mkataba wa uchimbaji (assessments tayari). BARRICK hawakuwa tayari kupoteza mgodi huo wa Bulyanhulu
Barrick Gold corporation wakaingia makubaliano na serikali ya Tanzania siku ya tarehe 19 Mei 2019 ingawa yaliwekwa wazi na kampuni ya BARRICK GOLD CORPORATION siku ya tarehe 19 Julai 2019 mara baada ya kufanikiwa kuinunua kampuni ya ACACIA Mining plc.
kanuni za masoko ya mitaji zimewalazimisha BARRICK kuweka hadharani makubaliano yao na serikali ya Tanzania. Ingawa kanuni hizo haziibani serikali katika hilo (ukizingatia, TZ sio sehemu ya OGP hivyo haitalazimika kuweka wazi Bungeni makubaliano hayo na Barrick Gold corporation)
Serikali imekubaliana na BARRICK italipwa $300M (TZS 700bn) kama sehemu ya kumaliza mgogoro wote na sio tena ile fedha ya kununua NOAH (kishika uchumba/Good faith), lakini BARRICK watalipa kwa miaka 7 ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo ACACIA inaidai Tanzania.
ACACIA GROUP ina madai ya marejesho ya VAT karibu $240M. Hivyo katika malipo ya $300M, fedha zitakazobaki baada ya kutoa madai ya VAT REFUNDS ni $60M. Hivyo serikali ya Tanzania inatoa 'bakshishi' ya $25M (wastani wa TZS 59bn) kwa Barrick Gold Corporation.
$300M italipwa kwa miaka 7 lakini BARRICK wanapewa VAT REFUNDS ya $240M na wanapewa msamaha wa capital gains $85.6M (TZS 200bn)

Serikali imetoa msamaha wa VAT kwa BARRICK zaidi ya $85M (TZS 200bn) sehemu ya 'capital gains' inayotokana na mauzo ya hisa za ACACIA kwa Barrick
Mapato hayo serikali iliyopoteza ni mapato halali. Barrick inainunua ACACIA kwa hisa ambazo Barrick hakuwa mmiliki, zenye thamani ya $428M zenye capital gains Tax ya 20% ambayo ilipaswa kulipwa bila kutoa msamaha wa kodi (waiver).
The government of TZ will receive its economic benefits shares through withholding tax, royalties, clearing fee, fuel and petrol levies, road tolls, local government levies, import duties, skills development levy and other similar fiscal levies, if any,” muhimu hapa ni "if any"..
Serikali ya Tanzania itapata hisa za bure 16% Kutoka ACACIA lakini ni hisa dhaifu kutoka daraja B, haziruhusiwi kuuzwa, hutumii kama dhamana ya mkopo, hazina 'voting point' kwenye masuala mengine ya kampuni, gawio litaifikia GoT baada ya kutoka daraja A kulipwa kwa ukamilifu.
Pia, Mwenyekiti wa bodi - 'board of directors' kwenye kampuni ambayo itaundwa baada ya mgawanyo wa hisa hizo 16% kwa GoT, atachaguliwa kutoka kwenye wanahisa wa 'daraja A' na taarifa inaeleza “… a holder of Class B shares has no such right,”
Lakini pia, kinyume na matakwa ya sera zenye kuendesha masoko ya mitaji ba hata sheria ya madini (2010) iliyotungwa na bunge, serikali imekubali BARRICK kutoorodhesha hisa zake kwenye soko lolote la hisa Tanzania. Hivyo hawatauza 30% ya hisa kwenye soko la hisa la Tanzania.
Barrick Gold Corporation wamekubaliana na GoT baada ya mkataba wao kukamilika Bunge haliwezi kutunga sheria ambayo itabadili makubaliano na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa wakati wote ambao BARRICK watakuwa wanawekeza
Maana, Bunge la Tanzania limezuiwa kwa namna yoyote kutunga kanuni au sheria nyingine yoyote hata kama itachukua miaka 100 ambayo BARRICK watakuwa wanaendesha shughuli zao (fiscal stabilisation) nchini Tanzania. Hivyo Barrick watafanya ambayo yanawafurahisha bila bunge kuingilia.
Mapendekezo ya Kamati zile mbili alizounda Rais Magufuli, kamati za makinikia zilipendekeza kuhusu mashauri yote yafanyike nchini, BARRICK wamegoma, hivyo kwenye makubaliano hayo wameruhusiwa kufungua kesi zao kwenye mahakama za usuluhishi wa migogoro ya kibiashara ughaibuni.
Kampuni za uwekezaji kwenye madini zimezuiliwa kisheria-sheria mpya za madini) kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Sheria inazitaka kampuni kushughulikia migogoro yote ya kibiashara na uendeshaji katika mahakama za ndani ya nchi. BARRICK walitoa pendekezo lao na likakubaliwa.
BARRICK Gold Corporation wametaka migogoro yao ifanyikae kwa mujibu wa kanuni za The United Nations Commission on International Trade Law (UNCITRAL) Arbitration Rules na Rais wa kituo cha usuluhishi wa migogoro ya kibiashara cha Singapore ndio ambaye atateua wasuluhishi.
"the president of the Singapore International Arbitration Centre has been given the mandate to determine the arbitral seat upon failure by both sides to agree." hivyo anaweza kuamua kuteua wajumbe kutoka pahali anapoona panafaa, habanwi kuteua wajumbe kutoka Tanzania.
BARRICK Gold corporation wataendelea kusafirisha makinikia nje ya nchi katika makubaliano hayo hakuna sehemu wamekubali kujenga "smelters" nchini kama ambavyo kamati zile mbili zilivyopendekeza. Na wamekubaliana kuendelea kutumia benki za nje kutunza fedha zao za mapato ya ndani.
Tanzania Mining Companies (TMCs) shall not at any time have any obligation to establish beneficiation-including gold refining and concentrate smelting facilities - in the country. Kwa wakati wowote TMC hawatakuwa na mamlaka ya kupunguza au kuongeza vituo vya uchenjuaji makinikia
Tangu Barrick Gold Corporation wachukue umiliki wa North Mara na Bulyanhulu September 2019, uwekezaji wao umefika $1.995 billion. Hadi kufikia Julai 2022 katika ile $300M walifanikiwa kulipa $140M (kama sehemu ya kumaliza mgogoro). Hiyo ni kwa mujibu wa CEO Mark Bristow.
Taarifa ya BARRICK GOLD CORPORATION ina makubaliano mengi iliyoingia na serikali ya Tanzania, lakini kwa kiasi kikubwa BARRICK wameondoka kwenye meza za MAZUNGUMZO wakiwa washindi, mapendekezo yote ya Kamati zile za Rais Barrick haikuyapokea, na kama yalipokekewa, yalifinyangwa.
Hayo ndiyo mambo, Profesa Palamagamba Kabudi alivyotuingiza. Rais Magufuli anafahamu, alifikishiwa haya makubaliano akiwepo ofisini. BARRICK ni washindi ndiyo maana hadithi ya NOAH kwa kila mtanzania imeyeyuka kama theluji wakati wa kiangazi.

#MMM, Martin Maranja Masese
Mtikila

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Martin Maranja Masese

Martin Maranja Masese Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @IAMartin_

Oct 10
“Letter to the president of the United Republic of Tanzania”

Dear madam president, HE. @SuluhuSamia

How are you doing? Image
These are my quarterly (4th quarter, 1 October–31 December (92 days) greetings to U & yours as well. We prayed 2022 to be a better year for all of us, the year in which we (would) refined ourselves, because it was another year of struggle for existence as always. Let’s talk now!
Today, again, I come to you with great humility, but not diffidence, as an ordinary citizen of this beloved land. I will try to use my very vertical percipience, prudence and sagacity to try speak out, and I hope you will hand-pick these writings in a very positive way.
Read 61 tweets
Oct 7
Jaji anaingia mahakamani saa 9:30 asubuhi...

Watu wote mahakamani wanasimama....

Kesi namba 36/2022, Halima James Mdee na wenzake V/s CHADEMA inasomwa leo Ijumaa October 4, 2022 hapa Mahakama kuu Mbele ya Jaji Cyprian Mkeha..

Mh Jaji: karibuni...
Anasimama Wakili wa Serikali...

WS: Mh Jaji Naitwa Kipilinga Panya nipo pamoja mawakili wasomi..
Aliko Mwamanenge
Emanuel Ukashu
Edson Kilatu
Matinde Wankashu

Kwa pamoja tuwawakilisha waleta maombi Halima James Mdee na wenzake kumi nane..
Anasimama Wakili Peter Kibatala..

Kibatala: Ikupendeze Mh jaji Naitwa Peter Kibatala nipo wenzangu.

Hekima Mwasipu
Dickson Matata
Faraji Mangula
Deogratias Mahinyila
Selemani Matauka
Pamoja tunamwakilisha mjibu Maombi wa kwanza.

Badae pia tutaungana na Wakili Jeremiah Mtobesya
Read 66 tweets
Sep 7
. @JMakamba Tatizo ni kanuni za EWURA, Sheria ya mafuta, EWURA au Wizara?

Kituo cha Mafuta Mvumi Mission, Chamwino, Dodoma, leo asubuhi bei ya Mafuta ni Sh.3,475 kwa lita ya petroli.

@EwuraTanzania wametoa bei kikomo lita ya Petroli ni Sh.3,023 Chamwino, Dodoma kuanzia 7/9/2022
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei
za bidhaa za mafuta ya petroli zinapangwa na soko lenyewe. EWURA Jukumu lao litakuwa ni kuhahamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa
za mafuta kwa kampuni za mafuta ambazo zipo 39.
Lakini kampuni hizo (39) za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (price cap) au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa (floor price) kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na Kanuni za EWURA.
Read 6 tweets
Sep 5
Bashungwa anasema vituo vya afya 234 vimejengwa kwa tozo. April 4,2019 walitueleza Magufuli amejenga 352. Hotuba ya Magufuli bungeni 2020 walisema wamejenga vituo 487. Sept 2021 wakasema Samia wamejenga vituo 220 kwa tozo. Mkopo IMF kwa ajili ya COVID-19 $567.25M mlipeleka wapi?
Ukiacha kwamba kukopa ili kutengeneza madawati ni jambo la hovyo. Fedha za IMF mlizipeleka kwenye jukumu ambalo siyo lake. Madawati na Madarasa sio kazi ya mikopo ya IMF. Hizo ni kazi kimaendeleo chini ya WB. Tanzania iliomba fedha IMF kukabiliana na dharura ya COVID-19.
IMF ni short term interventions nchi inapokabiliwa na changamoto za balance of payments; au ku' boost matumizi ya serikali linapotokea janga la kuathiri vyanzo vya mapato nchi husika; au zinapotokea emergencies (natural/human disasters) na kuathiri uzalishaji na uchumi kwa ujumla
Read 4 tweets
Sep 1
February 2018, Kampuni za umeme, Australia zilitakiwa kulipa fidia kwa wakazi wa jimbo la Victoria, nchini Australia waliothirika kwa kukosa umeme, malipo ya $180 kutegemeana na muda ambao 'nyumba ilikosa umeme'. Zilitengwa $5M. Umeme ulikatika kati ya saa 3-20.
Huku kwetu, umeme unakatwa bila taarifa, hakuna anaejali, ni wewe mwananchi kujitetea tena ukibembeleza waurudishe. Vinyozi, wachomelea vyuma, mafundi aluminum, wachapaji, banks etc hasara ni zao sio vinginevyo, nani wa kuwatetea? Nani wa kuwalipa fidia kwa hasara yao?
Serikali iruhusu uwekezaji wa kampuni binafsi za kutoa huduma za umeme, TANESCO ni kama wameshindwa hii kazi kabisa. Nchi inakosa umeme tangu asubuhi hadi usiku? Mnajichekesha tu.. Nchi yetu tumekabidhi kwa watu wasiokuwa na sera, mikakati na blueprint za kuendesha nchi.
Read 15 tweets
Aug 17
Zambia walichagua bilionea wao kuwa Rais. Hakainde Hichilema, HH - “Bally”, Wanamuita “cattle boy” anatajwa kuwa bilionea mkubwa Zambia. Anamiliki ranchi nambari mbili kwa ukubwa nchini Zambia. HH ana utajiri wa zaidi ya US$389M. Wengine tukomae na “watoza ushuru” wenye vilemba.
Hakainde Hichilema ni MFUGAJI mkubwa,pia anafanya shughuli za kilimo cha mahindi. Hichilema anashika nambari mbili nchini Zambia kwa kusafirisha nyama baada ya ZAMBEEF. Anasema alianza na ng’ombe 6 na sasa anao ng’ombe zaidi ya milioni 5.
July 2013 katika ranchi yake iliyopo wilaya ya Namwala, jimbo la Kusini, aliibiwa ng’ombe wake zaidi ya 500. Hii mwaka 2013 ilikuwa na thamani Kwacha Bilioni 1. Shamba hilo lipo chini ya kampuni ya HH FARMS Ltd. Huyu ni mfugaji mkubwa. Bilionea.
Read 10 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(