Majaliwa Jackson (Maja Munyama), mvuvi wa dagaa anasema alipoona ndege imetua ndani ya maji (kutoka upande wa Kyaka) isivyo kawaida, kwa kuwa ilikuwa asubuhi, saa 8:53 EAT, aliwasanua wenzake waliokuwa na mtumbwi mdogo, walipiga kasia hadi kwenye ndege.
Majaliwa anasema alipofika kwenye ndege, alikuta watu wakijadili jinsi ya kuingia ndani kutoa msaada, lakini mlango umejifunga (locked). Majaliwa akatumia kasia yake, akapiga, mlango ukafunguka, watu wakaanza kuokolewa kupitia mlango huo. Majaliwa akahamia upande wa rubani.
Majaliwa akazama hadi kwa rubani, captain Baruhani Rubaga akaonyesha ishara, abomoe kioo, akafuata shoka, walinzi wakampa, sauti ya mamlaka kutoka katika kipaza sauti, kikamzuia, asithubutu. Kwanini? kwamba rubani wanawasiliana kwenye simu zao, yupo salama, maji hayajafika kwake.
Majaliwa Jackson anasema alibishana nao kwa dakika kadhaa watu hao waliokuwa wakitangaza kwa kipaza sauti bila kutoa msaada wa vitendo, walimkatalia, akawaeleza kwamba maji yanaingia kwa the kasi ndani na rubani ametoa maelekezo kioo cha upande wake kivunjwe, walimkatalia.
Majaliwa akazama tena chini akampungia mkono wa kwaheri captain Baruhani Rubaga. Rubani akamuonyesha ishara aingie mlango wa dharura (emergency). Majaliwa akazama alivyoelekezwa, akachukua kamba, akafunga ili wavuvi wenzake waanze kuvuta, kamba ikavutika kwa kasi, ikamchapa usoni
Majaliwa Jackson akazirai pale pale, ameshtuka yupo hospitali ya rufaa - kanda ya mkoa wa Kagera. Ndiye ametoa hii simulizi. Huyu anaweza kuwa amefanya kazi ngumu na kubwa ya kuhatarisha maisha yake kuliko Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyeletwa kwa Airbus H225 kutoka Mwanza #MMM
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
These are my quarterly (4th quarter, 1 October–31 December (92 days) greetings to U & yours as well. We prayed 2022 to be a better year for all of us, the year in which we (would) refined ourselves, because it was another year of struggle for existence as always. Let’s talk now!
Today, again, I come to you with great humility, but not diffidence, as an ordinary citizen of this beloved land. I will try to use my very vertical percipience, prudence and sagacity to try speak out, and I hope you will hand-pick these writings in a very positive way.
Julai 2019 Barrick Gold corporation ilinunua kampuni ya ACACIA Mining Plc kwa $428M. Hii ni baada ya mjadala wa muda mrefu kati ya BARRICK na ACACIA takribani miezi 5 ya mazungumzo BARRICK na ACACIA wakakubaliana thamani ya kampuni ya ACACIA ni $951M
Awali majadiliano kati ya serikali na BARRICK yaliyofanyika Tanzania yaligomewa na ACACIA na wanahisa wengine wa ACACIA ambao wanamiliki karibu 36% ya hisa zote za ACACIA. Serikali iligoma kwenda mezani na ACACIA, wakaamua kukaa na BARRICK Gold Corporation
Utaratibu wa wanahisa ndani ya ACACIA ni tofauti na kampuni nyingi, BARRICK ambaye ana hisa nyingi (74%) haingii kwenye mjadala kujadili makubaliano yake na serikali dhidi ya ACACIA. Wanahisa wengine wanayo nguvu ya kuweza kukataa mapendekezo ya BARRICK.
. @JMakamba Tatizo ni kanuni za EWURA, Sheria ya mafuta, EWURA au Wizara?
Kituo cha Mafuta Mvumi Mission, Chamwino, Dodoma, leo asubuhi bei ya Mafuta ni Sh.3,475 kwa lita ya petroli.
@EwuraTanzania wametoa bei kikomo lita ya Petroli ni Sh.3,023 Chamwino, Dodoma kuanzia 7/9/2022
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei
za bidhaa za mafuta ya petroli zinapangwa na soko lenyewe. EWURA Jukumu lao litakuwa ni kuhahamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa
za mafuta kwa kampuni za mafuta ambazo zipo 39.
Lakini kampuni hizo (39) za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (price cap) au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa (floor price) kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na Kanuni za EWURA.
Bashungwa anasema vituo vya afya 234 vimejengwa kwa tozo. April 4,2019 walitueleza Magufuli amejenga 352. Hotuba ya Magufuli bungeni 2020 walisema wamejenga vituo 487. Sept 2021 wakasema Samia wamejenga vituo 220 kwa tozo. Mkopo IMF kwa ajili ya COVID-19 $567.25M mlipeleka wapi?
Ukiacha kwamba kukopa ili kutengeneza madawati ni jambo la hovyo. Fedha za IMF mlizipeleka kwenye jukumu ambalo siyo lake. Madawati na Madarasa sio kazi ya mikopo ya IMF. Hizo ni kazi kimaendeleo chini ya WB. Tanzania iliomba fedha IMF kukabiliana na dharura ya COVID-19.
IMF ni short term interventions nchi inapokabiliwa na changamoto za balance of payments; au ku' boost matumizi ya serikali linapotokea janga la kuathiri vyanzo vya mapato nchi husika; au zinapotokea emergencies (natural/human disasters) na kuathiri uzalishaji na uchumi kwa ujumla
February 2018, Kampuni za umeme, Australia zilitakiwa kulipa fidia kwa wakazi wa jimbo la Victoria, nchini Australia waliothirika kwa kukosa umeme, malipo ya $180 kutegemeana na muda ambao 'nyumba ilikosa umeme'. Zilitengwa $5M. Umeme ulikatika kati ya saa 3-20.
Huku kwetu, umeme unakatwa bila taarifa, hakuna anaejali, ni wewe mwananchi kujitetea tena ukibembeleza waurudishe. Vinyozi, wachomelea vyuma, mafundi aluminum, wachapaji, banks etc hasara ni zao sio vinginevyo, nani wa kuwatetea? Nani wa kuwalipa fidia kwa hasara yao?
Serikali iruhusu uwekezaji wa kampuni binafsi za kutoa huduma za umeme, TANESCO ni kama wameshindwa hii kazi kabisa. Nchi inakosa umeme tangu asubuhi hadi usiku? Mnajichekesha tu.. Nchi yetu tumekabidhi kwa watu wasiokuwa na sera, mikakati na blueprint za kuendesha nchi.