KIDUKU Profile picture
Mar 8 β€’ 36 tweets β€’ 5 min read
*Unawajua WANAWAKE?* *Kama huwajui, Basi Tumia Hii Siku yao kuwajua*

*Denis Mpagaze*
#UZIπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Bwana mmoja baada ya kufunga ndoa na binti aliyemsotea kwa muda mrefu alisema, " Bebi, unajua siamini kabisaaaa kama nimekupata! Bebi akajibu, "Amini tu mume, mimi ni wako,
kikubwa omba Mungu usiishiwe hela nikaponyoka!" Hapa mwanaume unaweza kufa ghafla na wakati alikuwa anakutania tu.

Mnaweza kupanga na msichana muonane lakini muda huo ukifika yeye akapiga zake usingizi. Unaamua kumsubiri kwenye kona ya nyumba yao hadi unatamani ukagonge hodi,
lakini utasemaje? Lengo lake akupime akili tu! Wanawake, loh!

Kijana wa watu unarudi geto kulala kumsubiri apointment ya mrembo, masaa yanakimbia, mtu haji, unaamka na kwenda mpaka kwao, unasikiliza kama wanaongea, husikii sauti yake, unasema labda mmepishana njiani. Unakimbia
kurudi gheto, hapo unawauliza hata majirani hivi Fatuma hajapita mitaa hii.

Wanakwambia hawamjui. Unatoka tena mbio hadi kwao. Mara unasikia sauti ya Fatuma akipiga stori ndani, hana mpango kama unamsubiri muda. Hapo utatamani useme kwa sauti kubwa, "We Fatuma si niko hapa
nakusubiri?" Lakini unaishia kuumia kwa hasira. Wanawake bana! Sijui huwa wanajua??
Mwanamke anaweza kushinda na shost yake, wanapiga story vizuri tu, watapika, watakula, watatoka mpaka out pamoja, lakini mwenzao akiondoka tu utasikia," Gauni lake zuri kweli tatizo amekosa miguu, halafu wanaangusha kicheko..hahahahaa!
Kuna dada mmoja alipita kusafisha wigi lake saluni, alivyoondoka wadada wakaanza kuponda ati kasukia wigi utadhani kofia la askofu. Halafu ukimuangalia anayeponda sasa alivyosuka, utadhani amebeba kifaru anaelekea Ukraine. Ningekuwa Mungu ningewagawa bure hawa watu!
Mwanamke akipewa zawadi na mpenzi wake anaona ni sawa ila kaka yake akifanye hivyo kwa mpenzi wake utaskia. "Yule sio bure, karongwa." Ni wanawake wachache sana duniani wenye ujasiri wa kuvumilia mwanamke mwenzao anapo pata jambo jema!
Unaweza mpigia simu hata mara kumi asipokee kumbe kaiacha chumbani yeye yuko barazani anakula umbea na shost zake. Halafu hata akiichukua simu hajisumbua na missed calls kujua nani alikuwa anamtafuta. Akiona ulimpigia atakubeep hata kama unamnunuliaga vocha kila siku!
Yeye anachojua ni vocha ikiisha kubeep ili utume nyingine akawapigie wasiompa vocha. Ukitaka kujua hizo vocha huwa anampigia nani, atakwambia hunipendi kwa sauti ya Delila.Baharia unalegea. Wana sauti za maigizo hawa malaika, kulala njaa labda wapende wenyewe.
Usipoteza muda wako kumjua mwanamke. Mwanamke ameumbwa kupendwa tu. Hutaki acha!

Mwanamke anaweza kukupenda bila sababu na akakuchukia bila sababu pia kwa sababu kupenda na kuchukia siyo wajibu wao!
Mwanamke ni kama askari, hana muda na watu waliotulia, yeye na majitu pasua kichwa. Akipata bwana tajiri atalalamika hampi mapenzi, akipata lofa mwenye bidii atalalamika hampi pesa.
Wanasaikolojia wanasema kama utaamua kuishi na mwanamke itakuchukua miaka 25 kumuelewa. Kwa lugha rahisi utakuja kumuelewa mwanamke tayari mmeishazeeka, sasa ya nini kujisumbua?
We mpende tu ili siku zako za kuishi hapa duniani ziwe nyingi, mchunguze zipungue. Unaweza mnunulia gari la thamani lakini akamthamini atakayemnunulia mafuta ya elfu kumi gari likizimikia barabarani! Mungu ni fundi nyie!!!!
Unaweza kumpa pesa ya kununua kilo hamsini za nyama asikushukuru lakini akamshukuru muuza nyama kwa kumpimia minofu mitupu!
Unaweza msomesha hadi chuo kikuu, ukamtafutia na ajira halafu akamthamini aliyemlipia chai na chapatti tatu pale kazini. Unajua ni kwa nini? Iko hivi; kama huwezi kumsaidia mwanamke leo, atakuona humpendi haijalishi umemsaidia mangapi huko nyuma.
Anadaiwa kodi laki mbili wewe ukampa laki na tisini, atakayemalizia hiyo ten kwake ndo mwanaume, atampa zawadi ya ushindi.
Kwahiyo kuanzia leo mtu wako akiwa na shida usianze drama za nimekufanyia mengi lakini huna shukurani. Hizi utajua mwenyewe. Mwanamke ni kama treni, hairudi nyuma. Unataka ageuke nyuma awe jiwe la chumvi kama mke wa Luthu? Thubutu!
Ni wajibu wa mwanaume kumpenda lakini wakati mwingine jinsi unavyozidi kumpenda ndivyo anavyozidi kujiweka mbali na wewe. Inakuwa kama vile unamvuruga.

Hawa ni watu wanaoamini katika vitu vidogovidogo ili wavifanye kuwa vikubwa. Ukimpenda kidogo atakupenda sana, ukimfokea
kidogo atayakuza balaa, ukimpiga kibao atasema ulitaka kumuua.

Jamaa mmoja akasema mwanamke katika mwezi mzima huwa anakuwa na akili siku mbili tu. Mie nikamwambia si kweli. Hawa wana akili nyingi siku zote za mwezi.
Wangekuwa hawana akili wasingetulaza nje. Sasa kwani kurudi nyumbani usiku wa manane kuogopa kelele za mke wako kuna tofauti gani na kulala nje?
Unaweza kuanzisha mahusiano leo na mwanamke halafu kesho kodi ya nyumba ikaisha, ada ya watoto ikaisha, umeme ukaisha, mama yake akaugua, chakula ndani kikaisha na siku ya kwenda saluni ikafika. Hapo sijui unafanyaje!
Hawa ndio wanawake Mura! Nawapenda kwa sababu ndio wanaochangamsha dunia. Hata pesa bila wanawake hupungua ladha. Hata Aristotle aliwahi kusema, "If women didn't exist, all the money in the world would have no meaning."
Akikutumia meseji ya Honey nikwambie kitu, katika ya mwezi unaweza usiifungue! Najua umenielewa. Sifafanui! A woman is like a tea bag, you can't tell how strong she is until you put her in hot water. Eti unaniandikia Kingereza ulinisomesha?
Unaweza kuzoeana na mwanamke kabisa lakini siku ukimwambia nataka nikuoe, akaruka mita mia na kusema "unajua nilikuwa nakuheshimu ujue?" Umeniboa sana leo. Hapa utabaki unajiuliza kwahiyo wanawake wanaolewa na watu wanaowadharau?
Halafu anaweza kuwa online lakini akiona umeanza kutype akazima data hadi kesho maana anakujua. Utaishia kusema wanakutenga. Brother hakuna anayekutenga. jipange!
Mwanamke akivurugwa utamkuta anajipepea kwa kiganjΓ  hata kama hakuna joto. Ukimuuliza atakwambia niache, naishiwa pumzi. Hawa watu ni burudani sana.
Anaweza kunyoa nyusi zote halafu akapaka rangi nyeusi.Very very funny. Sijui wakoje. Anaweza kuvaa nguo fupi inayoonesha hadi vya ndani halafu akifika mbele za watu akaanza kuishusha!
Sasa bora hao, je yule anayechomekea dela upande mmoja? Sijui ile huwa ni kamba au bikini? Ukimuuliza atakwambia hayakuhusu. Kengine ukikakuta kalivyotulia kanisani huwezi amini ndio kanatembea na wame za watu!
Unaweza mpa hela ya kodi halafu nusu akaenda saluni na nyingine akalipa vikoba.Siku vyombo vikitupwa nje ndio utaelewa kwanini hakuna baba mwenye gari, kuna baba mwenye nyumba.
Mkitoka naye out hata kama anamiliki dolali atategea kulipa. Ukisubiri alipe yatakutokea yaleee ya Adam kufukuzwa Bustani ya Eden.
Lakini pia mwanamke anaweza kujiremba ili apendeze, apendwe. Ukimwambia nakupenda, akakutukana. Loh! Unaweza kumpendezesha mwanamke akamshukuru aliyemkumbatia kwa sababu ya kupendeza.
Wanasaikolojia wanasema ukimkumbatia mwanamke walau kwa sekunde kumi na tano anatokea kukuamini sanaa!

Ipo siku nitakuletea faida kumi za kukumbatiwa. Binadamu ili awe salama kiakili na kimwili anatakiwa kukumbatiwa walau mara nane kwa siku! Vinginevyo visilani, hasira za karibu
na presha vitakuua. Nitaleta makala hiyo Januari 21, siku ya kukumbatiana duniani!

Unanaweza kustuka usingizini usiku wa manane ukakuta mwanamke wako amesimama anakumulika na tochi ya simu.hahaha...

Tutumie siku hii kujisomea vitabu vyangu 10 kwa ofa ya
Sh 20,000 tu. Mpesa 0753665484!

1. Mbinu 16 Alizotumia Yesu Kutoboa!

2. Viongozo Walioandika Majina Yao Vibaya 3. Fungua Ubongo

4. Fahamu ya Ndoa Kabla ya Ndoa

5. Miamba ya Afrika

6. Viongozi Wanaoishi Baada ya Kufa

7. Maisha ni Kutafuta Siyo Kutafutana
8. Ukombozi wa Fikra

9. Wasomi Huru Gerezani
10. Ukombozi wa Fikra za Mwafrika

Hardcopy ni no mpaka 10. Piga +255753690907

*Wako

*Mwl. Denis Mpagaze* *Muhenga wa Karne va 21!*

β€’ β€’ β€’

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
γ€€

Keep Current with KIDUKU

KIDUKU Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @TanzaniaOneJezi

Mar 9
*Tulipanda Usiku, Tunavuna Mchana.*
#UZIπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
USHOGA, ULAWITI, USAGAJI.

Tulipoamua sote kuwa wafanyakazi, wajasiriamali na watumishi (wanaume kwa wanawake) hatukutafakari vyema. ImageImage
Tulipoamua kuingia mtaani na kujipotosha juu ya haki sawa bila kujua undani halisi wa *haki, fursa na wajibu* hatukutafakari ya kesho.

Imeandikwa na *Mnegro* 8, March 2023.12:20PM.

Karibu sana.
Tulipoamua kufanya hayo yote, hatukuwaza vyema juu ya familia. Hatukuwaza juu ya misingi na malezi ya watoto wetu. Hatukuwaza nani atabaki nyumbani kusimamia jukumu kuu la nyumbani.
Read 36 tweets
Mar 8
TUSIMLAUMU RAIS SAMIA; TUKUMBUKE TULIKOTOKA.
Anaandika Askofu BAGONZA ( PhD )
Rais Samia ameweka rekodi. Tutasahau barabara, madaraja, madarasa na teuzi anazofanya. Lakini hili la kukutana na Chadema katika maadhimisho ya BAWACHA hatutalisahau kirahisi. ImageImage
Wapo walionuna pande zote mbili za CCM na Upinzani. Ni budi wawepo ili watukumbushe tulikotoka. Hata kuku wa pande mbili hizo hawakuruhusiwa kujamiiana. Leo twakumbatiana!
Mwaka jana 2022 nilihutubia Bawacha Kitaifa kule Iringa. Nilisema tunahitaji Tanzania mpya siyo CCM mpya wala Chadema mpya.

Niliporudi DSM nilikutana na kiongozi wa CCM kitaifa nikamwambia; "Awamu ya Tano imeimarisha upinzani kwa namna ambayo ni vigumu kuubomoa bali kuuruhusu
Read 13 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(