KIDUKU Profile picture
Mar 9 36 tweets 6 min read
*Tulipanda Usiku, Tunavuna Mchana.*
#UZI👇👇👇
USHOGA, ULAWITI, USAGAJI.

Tulipoamua sote kuwa wafanyakazi, wajasiriamali na watumishi (wanaume kwa wanawake) hatukutafakari vyema.
Tulipoamua kuingia mtaani na kujipotosha juu ya haki sawa bila kujua undani halisi wa *haki, fursa na wajibu* hatukutafakari ya kesho.

Imeandikwa na *Mnegro* 8, March 2023.12:20PM.

Karibu sana.
Tulipoamua kufanya hayo yote, hatukuwaza vyema juu ya familia. Hatukuwaza juu ya misingi na malezi ya watoto wetu. Hatukuwaza nani atabaki nyumbani kusimamia jukumu kuu la nyumbani.
Tukaanza kuwakebehi akina mama wa nyumbani na kuwaita majina mabaya. Tukawaita *magolikipa*, *chuma ulete*, *wajaza vyoo*, *mizigo*, *punching bags* na kila jina tuliloona linatosha kuwafanya wachukie kusimamia *jukumu lao kuu* ambalo wengi wetu mama zetu walilifanya ndiyo maana
leo tupo imara na tunawaona kama walikuwa wanawake wa chuma.

Wanawake nao walipoona imezidi, na kwamba akiwa dokta, mwanasheria, mfanyabiashara n.k ndo anaonekana bora na wa kisasa, nao wakaingia mzigoni.
Walipoelezwa kuwa maisha ni kusaidiana, bila kujua kuwa mama kusimamia jukumu la mji wake ndiyo msaada mkubwa kwa mumewe kuliko misaada yote, nao wakaingia kingi. Baba anaondoka na mama anaondoka. Mji unabaki na mtu ambaye huitwa *housegirl* au *HOUSEBOY* au ndugu wa mume au mke
ambao nao wana ndoto zao, tabia zao, changamoto na mahitaji yao ambayo sasa yakawa ndiyo msingi wa malezi ya watoto wa baba na mama watafutaji.
Haijazidi miaka 30 toka huu mchakato usambazwe zaidi kupitia mifumo yetu ya kielimu, kisiasa na kijamii, Sasa tumeanza kuvuna matunda ya *haki sawa*, matunda ya *kusaidiana*, matunda ya *mwanamke anaweza*, *matunda ya mkutano wa Beijing*, na matunda ya kila aina ya utumbo
tulioutafuna bila kuuosha. Sasa bakteria wa utumbo huo wameanza kutuozesha.

Mwelekeo huu wa matendo na matukio ya *ushoga* waweza kuwa mwanzo wa magumu mengi ambayo tutapitia kama jamii na taifa.
Wazungu na mashirika yao yaliyojificha kupitia taasisi za misaada chini ya *dini, afya, siasa, elimu na sanaa* wanajua ni kizazi gani kiliandaliwa ili kuja kuzalisha watoto ambao watapokea elements za LGBT (rejeeni haya mambo ya haki sawa yalianza kusambazwa zaidi lini nchini).
Sasa wanachofanya ni kuanza kuvuna matunda ya watoto wengi ambao hawakuelewa vyema na wazazi wao. Watoto waliokabidhiwa kwa walezi tofauti na wazazi wao kama vile wasaidizi wa kazi, walimu na wakufunzi wa dini.
Wengine ni watoto walioanza kutazama vipindi vya TV vyenye maudhui yanayoonesha ushoga wakiwa wadogo kuanzia miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni kuelekea 2010 na hata sasa kila tamthilia ya nje inayooneshwa nchini ina viashiria vya ushoga. Bado hatujashtuka.
Wazungu na washirika wao wanajua kizazi walichokiandika nao watazalisha kizazi dhaifu zaidi yao. Na ndiyo mchezo wenyewe unapoanzia.
Juzi *Waziri wa Afya* Dada *Umy Mwalimu* alisema na kuwakumbusha akina mama juu ya majukumu yao ya msingi ya kulea familia zao kuliko kujitokeza mitaani kama watafutaji na wafanyabishara zaidi. Akasema kuwa wasishindane na wanaume.
Kama Waziri ameona changamoto, tuna kila sababu ya kuona hili tatizo na kulichukulia kuwa tatizo la kitaifa.
Tulidanganywa tukadanyika. Leo tuna watoto ambao hata mzazi akiteseka, akiugua au hata akifa hawana uchungu maana wamelelewa zaidi na watu baki kuliko wazazi wao. Tuna watoto ambao wanathamini zaidi watu wa nje na marafiki kuliko walio wazaa. Na hawana mahusiano chanya na familia
Ikumbukwe ukifanikiwa kuvunja bond ya familia, umeangamiza taifa zima.

Tumetikisa na tunaendelea kuvunja taasisi ya familia kwa kugeuza msingi wa majukumu kiasi kwamba kuna nyumba huwez kujua baba ni nani na mama ni nani. Utafutaji umekuwa ndo tatizo ambalo leo hii linavunja
ndoa na kupelekea mauaji kitu ambacho hakikuwepo enzi za wazazi wetu wa chuma.

Na zaidi tuna familia nyingi za mzazi mmoja (single parent) ambazo zaidi kabisa ni za wanawake na watoto wao.
Hii ni kwasababu mwanamke wa kisasa mwenye kaelimu ka darasani hususani waliofika hadi vyuoni, wengi wao huona wanaweza hata wakiwa pekee yao. Mwisho ni mwendelezo wa uzinzi na mabadiliko ya *ma-anko* kila cku.
Matokeo yake mtoto anajifunza tabia hizo na kukosa misimamo ya kimaisha. Akifikisha umri wa balehe tu mama anabak analia na hana uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya mtoto wake. Na wakati huo huenda mtoto alishaambiwa baba yako alikufa au alikukataa.
Kuna mwanamama mmoja mmiliki wa taasisi moja inajihusisha na sanaa, sitaitaja jina. Naye ni single mother. Wakati mmoja alisikia wimbo uliokuwa na maadhi ya kuwatia moyo single mothers...wimbo ule ulimtia simanzi na hata akatoa machozi.
Yeye ni single mother aliyefanikiwa, na alisema amefanikiwa akiwa single mother. Je kufanikiwa ndiko kulikomtoa machozi baada ya kusikiliza wimbo ule? Kwanini atoe machozi? Kwanini asifurahie tu ila hadi chozi linamtoka? Kuna mahusiano gani kati ya mafanikio na machozi? Nadhani
kuna mihangaiko mingi na misukosuko na mateso mengi amepitia hadi kufanikiwa kama single mother ndiko wimbo ule ulimkumbusha hadi akatoa Machozi yake.
Hakuna mtu mwenye akili timamu anayetamani kuishi pekee yake hadi uzee wake. Watoto huja kama baraka na matunda ya familia, ila wakati wao ukifika nao huondoka na kwenda kuanzisha familia zao. Wenza hubakia wawili wakiendelea kuliwazana na kushea hisia zao hadi mwisho wao.
Hakuna anayetamani kuishi peke yake na ikiwa yupo ni wachache sana na hawakuanzisha familia.

Mfano huo utufundishe kuwa tunahitaji familia ibaki kujengwa na baba na mama na siyo vinginevyo. Huu ni msingi na ni kanuni za kimaumbile. Labda changamoto nyingine zisizoepukika
ziingilie kati. Napo bado mfiwa anayo haki ya kupata mwenza mwingine ikiwa bado anahitaji.
Kama taifa tujifunze kitu na tuanze kujirekebisha kabla hatujafikia wakati ambapo kabla ya kijana wa kiume na wa kike kuoana, watalazimika kupelekwa kupimwa kama ni mwanaume kweli au kama ni mwanamke kweli.
Wakati bado hatuna sheria ya moja kwa moja juu ya ushoga, kila mtu ashike na kutunza vyema alicho nacho.
Wanawake wafanyakazi na watafutaji tengeni muda kwaajili ya watoto na waume wenu. Jueni jukumu lenu kuu na la msingi ni usimamizi wa nyumba zenu na malezi ya watoto na waume zenu. Mengine hufuata baada ya hilo. Kubwa zaidi kumbukeni kuwa na utiifu na adabu kwa waume wenu bila
kujali uwezo wenu kiuchumi.

Msisahau kuwa mwanamke mtumishi ni daraja la 3 katika ubora wa mke. Hivyo pamoja na hilo jitahidini sana kuweka uzito kwenye familia zenu maana utumishi una mwisho, ila familia ni mwendelezo wa maisha na vizazi vyenu.
Nanyi wanaume jitahidini kuwapenda, kuwafundisha, kuwahurumia na kuwahakikishia usalama wake na watoto wenu. Msiwachokoze ili wasiwe na uchungu nanyi. Mtakosa baraka. Mkumbuke kutoa sadaka kwa watoto wenu ili milango yenu ifunguliwe.
Pia tambueni kuwa jukumu la kwanza kuhakikisha usalama na ustawi wa familia ni lenu bila kujali mke ana kipato au hana kipato. Na ikiwa wake wenu wanawasaidia iwe ni katika utafutaji ambao mnaufahamu na kuusimamia. Na kama ni watumishi, watieni moyo na kusimamia vipato vyao
visitawanyike na mwisho wakatawanya na familia zao kwa kiburi.

Na zaidi muwe na muda wa kukaa na familia ili kujua wapi kuna tatizo na kurekebisha mapema. Kumbukeni kuwa mwanaume mtumishi naye pia ni daraja la tatu la ubora wa mume. Hivyo ule udhaifu utaokuwa unajitokeza kwenye
familia ni lazima kutafuta namna ya kuupunguza ili watoto wenu waje kuwa imara zaidi yenu.

Pia wanafamilia tianeni moyo katika changamoto zenu kwa kuvumiliana na kuhurumiana.

*Tanbihi...*

Uimara wako ni matokeo ya yule mama ambaye sasa ni mzee. Ikiwa alikuwa mtumishi,
ubora wako unauona, ikiwa alikuwa mfanyabiashara pia vilevile na ikiwa alikuwa golikipa bado ubora wako ni matokeo ya muda na jitihada zake.

Amua aina ya familia yako kulingana na malezi bora uliyopewa na siyo unayoona kwenye TV na kuambiwa na wengine.
*Tunavuna matunda ya tulichopanda usiku na sasa tunashangaa kuona matunda hayana mbegu kama zile tulizopanda usiku.*

Ahsanteni.🙏 RT Ujumbe Huu Ufike Mbali Ili Kuponya Jamii Yetu.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with KIDUKU

KIDUKU Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @TanzaniaOneJezi

Mar 8
TUSIMLAUMU RAIS SAMIA; TUKUMBUKE TULIKOTOKA.
Anaandika Askofu BAGONZA ( PhD )
Rais Samia ameweka rekodi. Tutasahau barabara, madaraja, madarasa na teuzi anazofanya. Lakini hili la kukutana na Chadema katika maadhimisho ya BAWACHA hatutalisahau kirahisi.
Wapo walionuna pande zote mbili za CCM na Upinzani. Ni budi wawepo ili watukumbushe tulikotoka. Hata kuku wa pande mbili hizo hawakuruhusiwa kujamiiana. Leo twakumbatiana!
Mwaka jana 2022 nilihutubia Bawacha Kitaifa kule Iringa. Nilisema tunahitaji Tanzania mpya siyo CCM mpya wala Chadema mpya.

Niliporudi DSM nilikutana na kiongozi wa CCM kitaifa nikamwambia; "Awamu ya Tano imeimarisha upinzani kwa namna ambayo ni vigumu kuubomoa bali kuuruhusu
Read 13 tweets
Mar 8
*Unawajua WANAWAKE?* *Kama huwajui, Basi Tumia Hii Siku yao kuwajua*

*Denis Mpagaze*
#UZI👇👇👇👇
Bwana mmoja baada ya kufunga ndoa na binti aliyemsotea kwa muda mrefu alisema, " Bebi, unajua siamini kabisaaaa kama nimekupata! Bebi akajibu, "Amini tu mume, mimi ni wako,
kikubwa omba Mungu usiishiwe hela nikaponyoka!" Hapa mwanaume unaweza kufa ghafla na wakati alikuwa anakutania tu.

Mnaweza kupanga na msichana muonane lakini muda huo ukifika yeye akapiga zake usingizi. Unaamua kumsubiri kwenye kona ya nyumba yao hadi unatamani ukagonge hodi,
lakini utasemaje? Lengo lake akupime akili tu! Wanawake, loh!

Kijana wa watu unarudi geto kulala kumsubiri apointment ya mrembo, masaa yanakimbia, mtu haji, unaamka na kwenda mpaka kwao, unasikiliza kama wanaongea, husikii sauti yake, unasema labda mmepishana njiani. Unakimbia
Read 36 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(