Jamaa fulani anaona pikipiki mbili zinampita kwa mwendo wa kasi sana.
Kila pikipiki imebeba abiria wawili(mshikaki)
Hii ni baada ya kusikika milio mitano ya risasi
Yes A Dark day indeed
Baadae zikasambaa habari pale kisiwani kuwa Mlinzi mmoja wa mpaka wa shamba alikuwa “kalambwa vyuma” vitano na majambazi.
Naam!
It was a news tailored for journalists digest
Lakini nyuma ya pazia walinzi wa mipaka walikuwa wamegombana na bwana shamba two years back.
Kwanza walimchukia bwana shamba kwa kumleta kijana mdogo tu ndio awe kilanja wao lindoni.
Kijana huyo hakuwa na elimu dunia ya kutosha zaidi yao.
Yeye elimu dunia yake iliishia tu shule ya upili.
Elimu pekee aliyokuwa amebobea ni maswala ya mipaka.
Hakutegemewa kuwa Kilanja
Wakulima waliendelea kula ubwabwa na maharage na kwenda kulala.
Bila kujua mpakani mwa shamba kuna chess inachezwa.
Sasa Bwana shamba kuna maelekezo alitoa kwa kilanja akawaambie wenzake.
Ule haukuwa utaratibu
Namaanisha nini?
Yaani pale mpakani huwa kuna wazee ambao kiutaratibu kukiwa na jambo lolote, basi bwana shamba anatakiwa aongee nao pamoja akiwemo kilanja wao.
Sasa huu utaratibu wa kumtuma kilanja aongee nao hawakuupenda.
Na zaidi ya yote,
Maelekezo yaligusa maslahi yao
Unajua pale mpakani kulikuwa na Zabuni nyingi sana kuanzia catering services, Mafuta n.k
Zabuni hizi zilikuwa kiutaratibu zinachukuliwa na wazee ili nao wafurahie keki ya shamba kidogo.
Kwani wazee walikuwa wanaona wizi mkubwa tu pale shambani na kukaa kimya.
Zile zabuni angalau zilikuwa zinawafanya wazee wakae kimya na kutoingilia kwani uwezo wa kuingilia wanao na wanaweza kumweka bwana shamba yeyote kutokea kwenye kundi lao la wazee.
Sasa maelekezo yakatolewa kwa kilanja kwenda kwa wazee.
Kuwa zabuni sasa basi!
Yaani mchakato wa zabuni mpakani utakuwa unafanywa na bwana shamba kuanzia siku ya maelekezo hayo.
Mkutano ulikuwa wa moto!
Wazee wakafura!
Wakamuuliza kilanja huyo bwana shamba yuko wapi?
Kwa nini kakutuma wewe asije hapa azungumze hayo mbele yetu?
Wakamwambia unajua wewe ingawa ni kilanja lakini wewe ni bwana mdogo sana.
Wakamwabia kwanza wewe umeishia shule ya upili.. wewe sio size yetu, kamwite bwana shamba aje atueleze hayo.
Kilanja akarudisha zile taarifa kwa bwana shamba.
Bwana shamba alikuwa na tabia za ujeuri,
Hakuwa anapenda hata siku moja aonacho yeye ni sahii atokee mtu wa kukipinga.
Alishapewa ushauri na kilanja wa zamani kuwa kuna nyaya za kuchezea pale shambani lakini sio nyaya za transformer.
Hata bwana shamba wa zamani alimshauri hilo
Yeye hakutaka kusikia,
Sasa taarifa zile za mkutano wa mpakani zikamjia.
Akapuuzia kwenda mkutanoni.
Yeye akaanza kuwa anajihusisha na zabuni za watu wa mpakani.
Yaani wazee waliendelea kuhudumiwa bila wao kumtafuta muhudumu.
Bwana shamba hakujua kama swala lile ni nyeti.
Hakujua kama vikao vya usalama ndivyo vilivyoamua kuwa wazee wajipe zabuni wenyewe za kujihudumia.
Sababu kubwa ilikuwa kuwa kama mtu kutoka nje angewahudumia, angeweza kuwafanya chochote walinzi wa mpaka.
Mtu wa nje angeweza kuwa compromised akawawekea hata sumu kwenye chakula
Wazee walipoona tu Bwana shamba amewakwepa na kuanza kuwawekea watu wa nje kuwahudumia wakaamua kuandika barua kwa pamoja kuomba kuacha ulinzi.
This action a distress message security wise
Ikabidi bodaboda guy amfate bwanashamba.
Bodaboda guy without mincing words dared to inform Bwana shamba kuwa “Mzee hapa inamaanisha umeng’oa kiraka kwenye jeans ya bishoo”
Akamwambia “Find a way to resolve the matter before this deteriorated relationship with “wazee” sours much more.
Kama kawaida jamaa hapangiwi
Jamaa akaona hakuna threat yoyote
Lakini akawa ni mtu wa wasiwasi mwingi
Mara siku nyingine asilale kwenye nyumba ya bwana shamba.
September 11 2018 Wakazi wa Mapinga Bagamoyo walishtushwa na milio ya risasi usiku.
Milio ile ilikuwa ikitokea katika kambi ya mafunzo ya kijeshi Comprehensive Training Center (CTC) Mapinga.
Kwa wasioifahamu, Kambi hii ni ya pili na mpya mahususi kwa mafunzo ya Makomandoo baada ya ile ya 92KJ Ngerengere.
Kijiografia kambi hii haiko mbali sana na majengo ya watu wa Kaunda Suti.
Ilishatokea mara nyingi wanakamatwa watu wanaoingia katika kambi ile ya Jeshi na katika mahojiano ambayo sometimes yanahusisha mabavu, watu hao walionyesha ustahimilivu mkubwa wa mateso.
Ikabainika watu wanaoingia pale kambini sio raia wa kaida.
Rais Nkurunzinza anaondoka Dar Es Salaam majira ya saa 12 na robo jioni kurundi nchini kwake Burundi.
Anaondoka huku akiwa tayari ana taarifa ya kupinduliwa kwake
Baadae tulikuja kushangaa kuona ndege ile iliyombeba Rais Nkurunzinza yenye namba ZS-OPR ikigeuza na kutua tena katika anga la uwanja wa ndenge wa Dar Es salaam masaa machache tu baada ya kuondoka.
Haikufanya hivi kwa kupenda.
La hasha!
Neno la mapokezi kutoka kwa waongoza ndege katika uwanja wa ndege wa Bujumbura, ndio hasa liliwafanya wageuze.
Mwaka 2004 kabla hajaingia madarakani, mwishoni mwa mwaka 2005 akiwa Madarakani,na hata miaka iliyofatia katika utawala wake, Rais Kikwete alipata Changamoto kubwa sana ya ujambazi kwenye mabenki.
Mwaka 2004 May 21 majambazi yalivamia NBC Moshi na kupora 5.3 billions.
September 20,Mwaka 2005, duka la kubadilisha pesa la Mc Sons lilivamiwa jijini Dar na majambazi walikwapua Tshs Milioni 150 na kuondoka bila wahusika kubainika.
March 30,2006 benki ya Standard charted Dar ilivamiwa zikakombwa Tshs Milioni 300.
Huu mchezo sasa ukazoeleka!
Mwaka ule ule wa 2006(mwezi mmoja tu uliofuata) tarehe 20 April likapigwa tukio Kabambe pale lilipokuwa eneo maarufu kama Ubungo mataa (Sasa Kijazi interchange)
Naam,
Ilikuwa ni saa 6 na dk 30 mchana watu wa dar walishuhudia movie la kivita katika uhalisia.