KUMBUKUMBU KIFO CHA JPM.
#UZI.

Ilikuwa saa 5 usiku 17 March 2021. Nilikuwa ndani ya kuta za gereza la Ruanda selo namba 17. Nikasikia kelele nyingi selo zingine ukizingatia kelele haziruhusiwi usiku mpaka kuwe na tatizo. Maana kelele ndio alarm ya kuwaita askari kuashiria kuna👇
tatizo ndani ya selo husika. Sasa kwa uzoefu wangu nilijua kelele zile ni mtu kanyatiwa. Maana haiwezi kuisha wiki tukio la mtu kunyatiwa halijatokea. Kwa waliokaa jela wanaelewa maaana ya kunyatiwa. Lakini kelele zile zilinishtua maana zilikuwa kelele za shangwe kiasi kwamba👇
nikashtuka kuwa huenda kuna jambo la neema. Kipindi hicho nilikuwa na mgogoro mkubwa kati yangu na Bwana jela pamoja na mkuu wa Magereza mkoa RPO. Hii ni baada ya kuwachakaza kwa hoja nikiwawakilisha wafungwa na mahabusu kwenye mkutano uliofanyika gerezani mbele ya 👇
Kamishna wa Magereza CGP, Naibu katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani pamoja na wabunge sijui kamati gani. Sasa siku hiyo yani tarehe 17 March 2021 Nyapara mkuu msaidizi wa ngome alipewa maagizo na afisa wa zamu Inspector akiagizwa kwamba hakikisha Mdude na wapambe wake 👇
Wanahamishwa selo na wapelekwe selo namba 4. Hii ilikuwa selo ya wagonjwa wa akili. Hivyo ilikuwa ni kawaida ukiwa na bifu na askari Magereza yoyote lazima akuhamishie selo hii kama adhabu. Maana mziki wa hiyo selo sio wa kitoto. 👇
Kumbuka wagonjwa wa akili wenyewe kwenye hiyo selo hawalali bila dawa za usingizi na wakati mwingine dawa za usingizi zikikata usiku wa manane kelele zinaanza. Wengine hujisaidia haja zote hapohapo walipolala. Huku ndio maagizo yalitolewa Mdude na wenzake wahamishiwe. 👇
Baada ya maagizo hayo Nyapara mkuu msaidizi akanifuata kabla ya mafungio kunijulisha huku akisikitika kuonesha kutokukubaliana na maagizo hayo ya boss wake. Nikamuambia asijali. Muda wa mafungio ulipofika nikiwa nimebeba Shako au mfuko wangu mkononi ambao ndani yake ulikuwa 👇na
na chakula, maji, matunda na nguo nilienda moja kwa moja kwa wale maafisa wa zamu. Nikawahoji kuwa; "hivi mnavyoniona mimi nina akili timamu kiasi kwamba litakuwa tatizo mimi kukaa selo namba 4? Selo ya wagonjwa wa akili?
👇👇
Nilihoji kwa sauti ya juu lengo ni kutaka wafungwa na mahabusu waliokuwa karibu wasikie. Halafu nikaondoka zangu kwa mwendo wa madowido kwenda kupanga foleni selo namba 4. Ikaonekana kuwa aliyekuwa afisa mkuu wa zamu mwenye cheo cha ASP hakufurahishwa mimi kulazwa 👇
selo za vichaa hata kama nilikuwa na mgogoro na maboss wake. Akamuagiza Nyapara mkuu msaidizi anihamishie selo namba 16 kutoka selo namba 11 niliyokuwa nakaa awali badala ya kunihamishia namba 4. Lakini wapambe wangu wapatao wanne walipelekwa selo namba 4 huko. 👇👇
Basi nikaingizwa selo namba 16 na tukawa tumefungiwa watu 82 huku mahabusu tukiwa wawili tu wengine wakiwa wafungwa. Kama ilivyokuwa kawaida yangu baada ya kufungiwa nikaenda kuoga halafu nikarudi sehemu yangu ya kulala nikafanya ibada nikafungua mfuko wangu nikatoa 👇👇
chakula nikala kisha nikakaa kwa kuegamia ukuta huku nikijisomea Biblia.

Sasa kwa mujibu wa taratibu za gerezani ni kwamba inapofika saa tatu kamili usiku ni muda wa kusikiliza taarifa za habari kutoka radio mbalimbali ambazo husoma taarifa za habari muda huo.👇
Baada ya taarifa ya habari amri hutolewa na nyapara wa zamu ndani ya selo redio kuzimwa mpaka asubuhi wakati wa kusikiliza taarifa ya habari ya BBC.

Ni kwamba mpaka radio ya selo inazimwa saa nne kamili usiku kulikuwa hakuna habari mpya zaidi ya habari tunazozisikia kila siku.
Basi tukalala. Sasa kuna watu ambao wana radio zao ukiacha ile ya selo. Hivyo amri ya kuzimwa radio ikitolewa wao huendelea kusikiliza radio kwa sauti ya chini sana kiasi kwamba ni ngumu kuwagundua. Naam hawa ndio waliosikia Rais Samia akitangaza kifo cha Magufuli mida ya saa 5👇
Kumbuka katika utawala wa Magufuli alishawahi kuagiza wafungwa wapigwe mateke na wafanye kazi mfululizo. Lakini pia upande wa mahabusu kulikuwa na kilio cha kubambikiwa makesi halafu kesi zenyewe za mchongo na upelelezi haukamiliki miaka na miaka. 👇👇
Sasa wakati nasikiliza kwa umakini kelele zile kutoka selo jirani, nikasikia mmoja wao akisema; "Mungu amesikia kilio chetu huyu alisema tupigwe mateke na tufanyishwe kazi mfululizo".
Hapo ndio nikajua mkubwa JPM katutoka nikawaambia selo yetu washeni Radio Rais hatuko naye.👇
Ni kweli wakawasha radio ndio nikamsikia rafiki yangu Samia akitangaza msiba wa taifa. Ndani ya selo sasa ,watu walishangilia wakaninyajua juu mpaka wakaniumiza enka ya mguu lakini hata sikuona ni tatizo kwangu pamoja na kwamba nilikuwa nachechemea.👇👇
Kifo kile kilinifundisha kwamba ukiwa na madaraka ni muhimu kuepuka kutesa na kuumiza watu wengine. Kwa sisi wakristo YESU alituagiza kwamba tusiwatendee wengine tusichotaka kutendewa sisi.👇
Kwa hiyo kama ni mkristo halafu ulitumia madaraka yako kuwatendea wengine usiyotaka kutendewa wewe hata tungeliombea kaburi lako mara elfu ni kazi bure mbele za Mwenyezi Mungu.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Mdude Chadema

Mdude Chadema Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @mdudechadematz

Jun 7, 2022
Uzi👇👇

KUKAGULIWA NA KUPEKULIWA NDANI YA GEREZA.

BEI YA KITABU NI 20,000/- NJE YA GHARAMA ZA USAFIRI NA UNAWEZA KULIPIA AU KUWEKA ODA KITABU HIKI KWA NAMBA ZIFUATAZO;
0767654303,
0710879487.

VITABU VINAPATIKANA DAR ES SALAAM, KILIMANJARO NA MBEYA NA MIKOA MINGINE TUNATUMA
Ni utaratibu wa magereza yote kwamba, lazima mfungwa au mahabusu akaguliwe anavyoingia na kutoka ndani ya jengo la magereza. Na Kuna aina moja ya upekuzi ambayo inahusisha kuvuliwa nguo na kubaki mtupu. 👇👇
Ni mara chache unaweza kukaguliwa kawaida bila kuvuliwa nguo lakini mara nyingi upekuzi unahusisha kuvuliwa nguo. Ukiwa umetoka nje ya jengo la magereza hasa unaporudishwa ukitoka mahakamani, hospitali au kwenye kazi zingine za magereza.
Read 16 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(