Baba Mwita Profile picture
Husband | Father | Lawyer | Human Rights Activist | Democracy | Rule of Law | A People's Servant | An Agent of Change
Nov 22, 2020 7 tweets 2 min read
Endapo CCM watajidanganya kutegemea China kuwapa mikopo, basi nchi hii INAUZWA. China ilitoa Ksh 500 Bil kutengeneza SGR Kenya. Katika mkataba, wamekubaliana endapo Kenya itashindwa kulipa, basi China itamiliki Bandari ya Mombasa mpaka Deni litakapolipwa LOTE. Katika makubaliano hayo, China itakuwa inakusanya Ushuru na Mapato yote yatapelekwa moja kwa moja China mpaka deni litakapomalizika.

December 2017, China wamechukua umiliki wa miaka 99 wa Bandari ya Hambantota, Sri Lanka baada ya Serikali kushindwa kulipa mkopo wa billions za Dollars.
Sep 8, 2020 5 tweets 2 min read
Mara nyingi nimesikia CCM wakisema CHADEMA walipinga ununuzi wa Ndege lakini mbona leo wanazipanda! Ni hivi; hakuna anayepinga ndege zisinunuliwe, ila tatizo tuna VIPAUMBELE. Nchi hii kwa sasa, Sekta Afya, Elimu, Kilimo ni muhimu kuliko ndege. Mbona wagumu KUELEWA ninyi watu!!!🙌 Njia rahisi ya kuelewesha ni hii. Serikali imefanya kazi kubwa ya kusambaza UMEME, kujenga ZAHANATI, si ndio! Sasa ni lini mmesikia Upinzani unasema msisambaze Umeme au Msijenge Hospitali? Hivi ni vitu MUHIMU kwa Jamii, ndiyo maana Upinzani hawavipingi. Lakini unaponunua NDEGE👇
Aug 26, 2020 12 tweets 2 min read
#UZI MAPINGAMIZI YA TUNDU LISSU DHIDI YA RAIS JPM NA PROFESA LIBUMBA:

Mgombea wa Kiti cha Urais, Tundu Lissu ametoa mapingamizi mawili ambayo la kwanza linawahusu wagombea wote wawili, na la pili ninamuhusu Rais JPM peke yake. Prof. Lipumba amewekewa pingamizi moja tu!👇👇 Mapingamizi hayo yote yanahusiana na kuvunjwa kwa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama ifuatavyo;

Kosa 1:
Rais JPM na Profesa Lipumba wote wamevunja Sheria ya Uchaguzi inayosema; "𝗕𝗮𝗮𝗱𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗽𝗲𝘄𝗮 𝗳𝗼𝗺𝘂 𝘇𝗮 𝗨𝘁𝗲𝘂𝘇𝗶 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝘁𝗮𝗳𝘂𝘁𝗮 👇👇
Aug 8, 2020 5 tweets 2 min read
#UZI TUJIFUNZE KIINGEREZA - KISWAHILI:

1. Charger - kimemeshi
2. Remote - kitenzambali
3. Password - nywila
4. Akala (bladder shoes) - kirikiri
5. Passion fruit - karakara
6. Kangaroo - bukunyika
7. Fridge - jokofu
8. Juice - sharubati
9. Chips - vibanzi
10. PHD - uzamifu👇👇 11. Masters degree - uzamili
12. Degree - shahada
13. Diploma - stashahada
14. Certificate - astashahada
15. Keyboard - kicharazio
16. Scanner - mdaki
17. Flash disk- diski mweko
18. Mouse (for a computer)- kiteuzi
19. Floppy disk - diski tepetevu
20. Computer virus- mtaliga 👇👇
Aug 4, 2020 8 tweets 2 min read
#UZI KUHUSU NEMBO ZA TAIFA:

1- National Flag - Bendera
2- National Animal - Twiga
3- Uhuru Torch - Mwenge
4- Coat of Arms - Ngao ya Bibi na Bwana
5- National Anthem - Wimbo wa Taifa

Hizi nembo zote (National Symbols) zinalindwa na sheria yaani (Protected by law) isipokuwa 👇👇 Wimbo wa Taifa pekee ambao haulindwi na sheria.

KWANINI IKO HIVI?

Ili kitu kilindwe na Sheria ni lazima kiwe kinamilikiwa kwa asilimia 100. Tanzania haina Umiliki wa 100% wa Wimbo wa Taifa kwa sababu wimbo huu Tumeukopa kutoka kwa Jamii ya wa XHOSA 👇👇