Traves Senior Profile picture
—PR, Marketing & Communication Officer —Movie critic @modernFlickstz ✝️ Born-again Christian 💪🏾🙏🏾 ⚽ FC Barcelona ❤️💙 🏀 #Dubnation 💙💛
Aug 10, 2021 43 tweets 8 min read
UZI: HUWA SIPIGI WEZI KWASABABU HII...👇
😥Wakati nimefika AYA Sec 2007 Kondoa kuanza form 1 (boarding), niliibiwa suruali 3, mashuka 2, viatu, nk. Ilikuwa ndio 'Welcome Party' pale kila mwaka. Kuhamishiana vitu ilikuwa ni kawaida sana bwenini kwetu.
#TravStories #Testimony Nilipofika Form 2 nikaanza kujifunza hizo mishe na mimi. Nakumbuka nilijifunza kutekenya KILA KUFULI unayoijua wewe. Enzi hizo SOLEX zinasifiwa balaa, ila kwangu hazikuwa shida kabisa😁. Nilikuwa na bunda la funguo natembea nalo. Nikitaka chochote napata fasta kwenye matranka😆