Kuduishe Kisowile Profile picture
MD | WHO Fides Influencer | P1L1 | Health Communications Consultant | #MeToo | Program Lead #MweleMalecelaDOA | #KuduAfyaTips | #DaktariMwandishi 🇹🇿 #RadFem

Aug 23, 2020, 18 tweets

Mara ya kwanza nilimuona kwenye muvi ambapo kichwa chake kilikuwa dili.
Ni mwanamke mrembo, ingawa filamu nyingi humuonyesha tofauti na historia isemavyo.
Nywele zake ni nyoka na ukikutanisha macho yake na yako unageuka jiwe. Anaitwa MEDUSA! #UZI FUATILIA
#DaktariMwandishi

Historia yake inatoka kwenye hadithi za kigiriki, jina lake MEDUSA likimaanisha "mlinzi". Alikuwa binti mrembo, bikra na mtumishi wa mungu wa bikra, Athena. Alimtumikia kwenye helalu lake hadi mungu wa bahari, Poseidon alipombaka Medusa. Akapata mimba ya mapacha lkn hakuzaa.

Yule mungu Athena, akamlaani Medusa, akabadili nywle zake nzuri kuwa nyoka na kila kiumbe, binadamu, mnyama au miungu iliyokutanisha naye macho aligeuka jiwe.
Medusa akakimbia kwa hofu baada ya kushindwa kuishi na watu na miungu. Akaenda kuishi mapangoni. Akajificha.

Lakini je, Athena alimlaani Medusa au alimlinda? Baada ya kubakwa na mungu wa bahari Poseidon, baadhi ya wanaamini Athena alimbadili Medusa kuwa vile kama njia ya kumlinda asidhuriwe tena na miungu au wanadamu, wengine wanaamini alimlaani hivyo kwasababu ya wivu wa uzuri wake.

Medusa alijificha kwa miaka mingi, huku wanadamu na miungu ikijaribu kumtafuta ili kukata kichwa chake na kukitumia kama silaha dhidi ya maadui zao.
Alikuja kufanikiwa mungu-mtu (demigod), akamkata kichwa.
Alipomkata kichwa, wale watoto aliokuwa nao Medusa, walitoka, mmoja

anaitwa Chrysaor, aliyekuwa binadamu na Pegasus, farasi mwenye mabawa.
Kifo cha Medusa kilikuwa kama ishara ya uhuru wake baada ya maisha ya tabu, ya kujitenga ya mateso na ya kukosa haki.
Filamu nyingi na vitabu vinamuonyesha Medusa kama jini mwenye kudhuru watu lakini uhalisia

ni kwamba, Medusa alikuwa mhanga wa uovu wa miungu na wanadamu. Alikuwa mhanga wa ubakaji, na hata baada ya hapo, hakuna aliyemuelewa zaidi aligeuzwa kuwa kiumbe cha kutisha na kushindwa kuishi maisha ya kawaida tena.
Kwa wale walio wahanga wa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia,

hadithi ya Medusa si kitu kigeni kwao. Ni hadithi ambayo wahanga wa vitendo vya ubakaji hukutana nayo. Wanapokwenda kuripoti waliyotendewa, jamii huanza kwa kuwahukumu na kuwalaumu wao, na mwisho wao huonekana ni tatizo na wale wabakaji kubaki huru wakilindwa na jamii.

Baada ya karne nyingi za mapokeo ya kumuona Medusa kama mtu muovu, sasa maandiko mbalimbali yanabadilisha namna ambavyo yanamuandika. Yanaandika ukweli. Yanamuandika kama mhanga aliyehukumiwa na jamii. Binti aliyejitoa kumtumikia mungu Athena, na bado alipopatwa na shida, dunia

ikamgeuka. Laana ya Athena, ilikuwa baraka kwa Maisha ya Medusa. Ilikuwa ni kinga dhidi ya mtu yeyote kumdhuru tena. Leo hii, nembo ya kichwa cha Medusa, hutundikwa kwenye makazi ya wanawake waliotoka kwenye ndoa za manyanyaso, wahanga wa vipigo na ubakaji.
Ni nembo ya UNYONGE

uliobadilishwa kuwa NGUVU. Nembo ya kuonyesha uhodari wa kuweza kushinda mapito.
Leo hii, MEDUSA si mwovu tena, bali ni shujaa mbele ya mamilioni ya wahanga wa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia. Kila mmoja wao anaielewa vema stori ya Medusa, kwani ni stori yake #MimiNiMedusa🐍

Karne nyingi zilizopita huko Ugiriki, miungu na wanadamu walishindwa kumlinda Medusa. Bahati mbaya, hali haijabadilika hata leo. Tumeshindwa kuwalinda wahanga wa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia. Wengine wamelazimishwa kuolewa na waliowabaka. Wengine wamegeuziwa vibao na

kushtakiwa, wengine wamelaumiwa kwa kuwa wahanga wa vitendo hivi na wengine wamepotea kama Medusa. Wamewekewa alama kuwa "fulani yule aliyebakwa", ilhali waliowabaka wanatembea huru mitaani. Ni kaka, baba, waume, wajomba, babu, wachumba, wapenzi, mabosi, walimu, madaktari wetu.

Tumewalinda kwasababu hatuna utu, hatuna ubinadamu, hatujali maumivu ya wengine, kwasababu bado tunakumbatia maovu kwa mlango wa familia, utajiri na vyeo.
Ndio maana kesi hizi haziishi wala hazipungui. Zinapunguaje wakati tuna madaktari wanabaka wagonjwa hospitalini na hatusikii

mwisho wa kesi zao? Zinaishaje wakati, mtoto akibakwa tunayamaliza kifamilia? Zinaishaje wakati tunaona ni sawa kulewesha watu kisha kuwabaka? Zinaishaje wakati tunawatazama watoto wadogo wanafunzi kwa macho ya matamanio na tunaona ni sawa kuwataka kimapenzi, huu nao ni ubakaji.

Jambo moja naloamini, tunahitaji mahakama ya kesi za unyanyasaji wa kijinsia itengwe kwa hiyo kazi tu.
Kesi hizi nyingi hazifiki popote, na takwimu zinaonyesha kuwa 99% ya wabakaji hawapewi adhabu yoyote.
Tunahitaji kutoa elimu kwa watoto, jamii kusimama pamoja na kupiga vita

vitendo hivi kwa pamoja.
Watoto wetu wa kike na wa kiume, na wanawake wetu hawana ulinzi.
Sheria yetu inabidi kubadilishwa, hasa katika kipengele cha nini maana ya mwanaume kubakwa, kwasababu sheria yetu inalinda wabakaji wa kike. Na kulinda wanaume wanaobaka wake zao.

Iwapo kila mtu aliyebakwa, au kufanyiwa kitendo cha unyanyasaji wa kijinsia akiandika #MimiPia au #MimiNiMedusa🐍, tutashangaa kuona ni wangapi & watu kutoka rika, jinsia, umri, dini, kabila na vyeo mbalimbali wataandika.
NI JANGA.
NI JINAMIZI TUNALOLIKUMBATIA.
#DaktariMwandishi

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling