Akasimama Mama Victor, kila mtu alikuwa akisubiria maneno yake. Ni mama wa makamo, alipendeza sana. Akasema yeye ana funzo dogo, AINA TANO ZA MANENO.
Nimeona nisiwe mchoyo, niwashirikishe niliyojifunza jana kwenye #SisterhoodTeaParty by DinaMarious #UZI (MFUPI)
#DaktariMwandishi
1. Maneno matamu-
Yapo ya aina mbili
a)maneno ya faraja (maneno ya kutia moyo, maneno ya kuinua nafsi ya mtu)
b)maneno ya mapenzi (yamejaa huba, yanakufanya utekenyeke kabla hata hujaguswa, haya ni maneno ya kumpa umpendaye, maneno ya kutia hamasa)
#SisterhoodTeaParty
2. Maneno ya Raia- hautakuwa na maadui wala marafiki, unakuwa ni mtu wa salamu na watu lakini hujengi mahusiano zaidi. Unakuwa na mipaka, unajenga ukuta kukuzunguka hivyo unakuwa huna adui wala rafiki, huna mwandani, huna mtu wa kukuegemea wala wa kumuegemea.
#SisterhoodTeaParty
3. Maneno makali- tumepewa kukemea, usiache kukemea lakini usiwe na maneno makali. Yatakuzeesha. (Uso na maneno vinaendana). Mwanadamu yoyote anahitaji kupendwa.
Maneno haya hukujengea maadui wengi. Unakuwa unafokea watu, wafanyakazi na watoto wako wanakuogopa
#SisterhoodTeaParty
4. Maneno ya uchungu-
a)maneno ya matusi
b)maneno ya masimango
Maneno yanaumba uchungu. (je, ni kwa kufilisika maneno?) weka kaa mdomoni, mwambie Mungu usitoe maneno ya kumfanya mtu ajisikie vibaya. Unapopanda maneno ya uchungu, utavuna uchungu.
HAPA NASEMA
#SisterhoodTeaParty
Leo, kisima cha kijiji nakiwekea uzio. Humu ndani wengi mna maneno ya uchungu, kutwa kucha matusi na masimango. Sio TL, sio DM. Mtu umemkalia kooni mwana wa mwenzio kama unamdai? We ukiamka unashinda kwenye page za watu kazi kutukana, kukosoa, oooh miguu yake imefanyaje, ooh hana
ndevu, mwili kabati, ooh anajidai, maneno mengi kama mpigadebe. Maneno ya shombo yamewajaa sana. Sijui ni uchungu wa maisha yenu au vipi, ila kutwa wewe kuongelea ya watu. Haya ukishamsema, ukamtengenezea magroup DM au whatsapp, mkakaa na mlojaa uchungu wenzio, mkamchamba
mmepata nini? Kamomonyoka?
Tena kwa hawa celebrities, viongozi, watu maarufu na wenye followers wengi, ndo mnahisi kama vile hawana mioyo. Kila kukicha mtu umepiga kambi kwenye page zao, unatukana, unasimanga unahisi hawana mioyo? Hivi mnajisikiaje mtu anawaza kujiua sababu yako
Yakimkuta ya kumkuta, wewe wewe waja "jamani, tuwe kind to each other, hujui mtu anapitia nini"
Ooh, "muwe na thick skin"
Mnasahau hujui mtu anapitia yapi unamuongezea uchungu halafu unashangaa mambo yako hayaendi, hao followers wa kiki unaowataka hawaji, kujitaftia milaana tu!
5. Maneno Dhaifu - maneno ya mizaha, mropokaji, maneno yasiyo na mfupa, unaongea bila kufikiri.
Haya ndo maneno ya wengi pia. Kuna utani, na kuna mizaha. Unakuta watu wanataniana, na wewe unadandia tu. Jamani, utani wa watu uache kama ulivyo. Mizaha mingi alafu unawaza kwanini
mtu anakublock au watu hawakushirikishi mambo yao ya ndani. We kila jambo la mtu unaropoka, binadamu huna kifua, huna la sirini jamani. Khaa! Umefanya mapenzi na mtu, ushaenda kutangaza, limekuwa tangazo la DUME condom hilo hadi kila mtu ajue? Muwe na haya.
#SisterhoodTeaParty
Kila mtu, hata mimi katika nafasi moja au nyingine inawezekana tumeyaongea ain zote za maneno.
Basi tujitathmini. Tujifunze kuwa na upendo. Kuwa na kiasi. Kuyaangalia maisha ya wenzetu. Kuwa na mipaka. Kuwa na breki jamani.
Kusambaza upendo.
#SisterhoodTeaParty
#DaktariMwandishi
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.
