JAPHET MATARRA Profile picture
Father l Husband | Human Right Activist | Mineral Processing Engineer @JSPLcorporate |#Paralegal | Member @ChademaTz | #ManUTD |~Boss Himself | 💨StoryTeller💣

Jun 13, 2021, 35 tweets

"YOU ARE UNDER ARREST"

#Uzi

📌Je, wajua Leo ilikuwa siku ambayo sheria inayomlinda mhumiwa [Miranda rights/Warnings] anapokamatwa na vyombo ulinzi ilipitishwa huko marekani?

💨YES it's Miranda Vs Arizona case

📌 Historia yake

📌 Chanzo chake

📌Maamuzi ya kihistoria.

👇👇

Mnamo Juni 13, 1966 Mahakama Kuu ya Juu (Supreme Court) nchini Marekani ilitoa uamuzi wa kihistoria juu ya taratib za uendeshaji kesi za jinai mahakamani.Uamuzi huo ulitokana na kesi ya Miranda Vs Arizona kwamba watuhumiwa wa kesi wanazo haki zao kabla ya kuhojiwa wawapo kizuizin

Nadhani ulishawahi kusikia maneno haya

1. Una haki ya kukaa kimya.

2. Chochote unachosema kinaweza, na kitatumika, kama ushahidi mahakamani.

3. Una haki ya kuwa na wakili.

4. Ikiwa hauwezi kumudu gharama za wakili mahakama, itamteua mmoja kusimamia kesi zako

Tuendelee 👇

Hapa nchini sheria inayoratibu uendeshaji wa mashauri ya makosa ya jinai yanayohusu watu wazima iko chini ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 1985 kwenye sura ya 20. Lkn zipo sheria nyingine mbalimbali ambazo zinahusiana na uendeshaji wa mashauri ya makosa ya jinai.

Halikadhalika, ili kukamilisha utaratibu wa uendeshaji wa mashauri ya jinai kuna Sheria ya Ushahidi ya mwaka 1967, sura namba 6, inayoelekeza aina ya ushahidi, taratibu za kutoa ushahidi. Lengo langu sio hili bali ya kukuletea chanzo cha sheria hizi na taratibu za uendeshaji kesi

#Chanzo ni Miranda v. Arizona case, 384 U.S. 436 (1966)

Miranda vs. Arizona case ilikuwa kesi kubwa iliyofuatiliwa na kusisimua ulimwengu wote kutoka ktk Mahakama Kuu ya Jimbo la Arizona nchini Marekani.
RT. @Mangiwakwanza @biturojr @adamlutta @IAMartin_ @Gaspinho15 @Nkololotz

Kesi hii ilihusisha tuhuma za binti mmoja kubakwa na baadae ikaonekana polisi wa mjini Arizona wakiwa wamemfikisha kijana kwamba ndiye alihusika na jinai ile na kisha akahukumiwa kutokana na taarifa iliyolewa na polisi kwamba alikiri kufanya tukio lile.
@CarolNdosi @jtemba321

HISTORIA

Mnamo Machi 2, mwaka 1963 katika mitaa ya Phoenix, huko Arizona nchini Marekani. Ikiwa ni mida ya usiku binti mmoja Patricia McGee (sio jina lake halisi) mwenye umri wa miaka 18 akiwa barabarani kuelekea nyumbani akitokea kwenye ukumbi wa sinema alikokuwa akifanya kazi

Ghafla alitokea mtu aliyekuwa kwenye gari na kumkamata kwa nguvu akamfunga mikono nyuma na kumlazimisha alale kwenye kiti cha nyuma.
Baada ya kuendesha kwa takribani dakika 20, alilisimamisha gari pembezoni mwa barabara mbali kidogo ya jiji na kumbaka.

Baada ya kumbaka alimlazimisha ampe pesa zake zote alizokuwa nazo la sivyo angemuua na kisha akamwambia alale tena kwenye kiti cha nyuma, kisha akamrudisha mjini na kumuachia maeneo ya karibu na nyumba kwao.

Binti yule alipofanikiwa kufika nyumbani na alichukua simu akawapigia polisi kuomba msaada, walipofika ndipo aliwaeleza mkasa uliomtokea na kuwaambia muonekano wa kisura, kiumbo wa mtu aliyemfanyia unyama huo na plate namba za gari kisha wakampeleka hospitali kupatiwa matibabu.

Polisi waliendelea na zoezi la kumtafuta mhalifu na siku chache baada ya tukio kutokea Patricia na binamu yake walikwenda polisi na kutoa taarifa ya kuona gari moja linalofanana na lile likiwa linapita mara nyingi ktk kituo cha mabasi ambapo alitekwa.

Polisi walifuatilia gari lile na kufahamu lilikuwa likimilikiwa na mwanamke aitwaye Twila Hoffman (29) aliyekuwa akiishi Mesa huko Arizona. Hoffman alikuwa ni mpenzi wa Miranda na wote walikuwa wakiishi pamoja.

Wakapata mkanganyiko wa kuendelea kutafuta mhalifu baada ya kujua mmiliki wa gari ni jinsi ya kike. Lakini hawakuishia hapo waliamua kwenda kwake Hoffman ili kumkamata na kwamba huenda anafahamu aliyefanya unyama ule kwa kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alitumia gari lake.

mnamo Machi 13 asbh Polisi walimbishia mlango Hoffman, akafungua na wakamweleza kilichowapeleka nyumban kwake. Baada ya kusikia polisi wapo ndani Ernesto Miranda kijana mwenye umri wa 24 na mwanafunzi wa Sekondari A-level kwa mujibu wa maelezo ya polisi akajitokeza kuzungumza nao

Miranda alifanya vile ili kunusuru penzi lake kwani alijua yeye ndiye anatafutwa akawaomba waondoke naye wakazungumzie kituoni. Kiufupi Miranda akakamatwa na polisi na moja kwa moja kituoni kwa tuhuma za uhalifu na jinai ya utekaji nyara, kumbaka na kumuibia binti Patricia.

CHUMBA CHA MAHOJIANO

Alihojiwa na wapelelezi maswali mengi kwa muda wa masaa mawili bila kuwepo Wakili wake, ambapo baadae alikiri kutenda uhalifu huo. Baada ya hapo wapelelezi walimleta mwathiriwa ndani ya chumba polisi mmoja wao alimuuliza Miranda "huyu ndiye mtu aliyembaka?"

Miranda alimwangalia na kusema "Ndio, msichana alikuwa huyo" akakiri na kisha kusaini kwa maandishi.

Karatasi ile ilisema "haya ni maelezo yangu binafsi na nakiri nimeyatoa kwa hiari na haki zangu nazielewa,hivyo maelezo haya yatumike mahakamani kama ushahidi na sio vinginevyo"

Maelezo yale yalichukuliwa kama ushahidi mahakamani ingawa hakukuwa na haki maalum zilizoorodheshwa kwenye karatasi ile kama yanavyosema.Akasomewa mashataka mahakamani na alihukumiwa kwa uhalifu huo na Mahakama ya Arizona kutumikia kifungo cha miaka 20 mpk 30 jela.
@rollymsouth

Baadaye, Wakili wake Alvin Moore alihisi kwamba kukiri kwake Miranda hakukuwa na ukweli kutokana na ukweli kwamba hakuwa anafahamu haki yake ya kimsingi ya kuwa na wakili atakaye mwakilisha na aidha kwamba maneno yake ya awali yangeweza kutumika kama ushahidi wa maneno dhidi yake

Baada ya miezi 6 Wakili Alvin aliamua kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Jimbo la Arizona kwamba hakukubaliana kuwa kukiri kwa maandishi ya mteja wake na kuongeza kuwa huenda maelezo yalitokana na kulazimishwa, hivyo akaisisitiza mahakama ktk uamuzi ilioutoa kuangalia hilo.

Rufaa ya kesi hii katika Mahakama kuu ndiyo ilibadilisha kabisa utaratibu wa uendeshaji wa kesi za jinai nchini Marekani nadhani hata ktk nchi nyingi duniani.

Katika rufaa Wakili Alvin alihoji Mahakama maswali yafuatayo.

"Je! Taarifa yake [Miranda] ilitolewa kwa hiari?" na

Je, "Alipewa kinga zote za haki zake zinazotolewa na Katiba ya Marekani kwa kuzingatia sheria na kanuni za uendeshaji kesi mahakamani?"

Rufaa yake ilijibiwa na Mahakama Kuu ya Arizona mnamo Aprili 1965 kwamba kukiri kwa Miranda kulikuwa halali na kwamba alikuwa akijua haki zake.

Baada ya uamuzi huo kutolewa ndipo kesi ya Miranda ilianza kuvutia macho watu mbalimbali ikiwemo mawakili wa kimataifa. Kutokana na kuchukua sura mpya ktk Jimbo la Arizona, Robert Corcoran ndipo aliibuka na ACLU (American Civil liberties Union) Umoja wa Uhuru wa Kiraia wa Amerika

Wakili Corcoran akaamua kuivalia njuga kesi hii akaenda kwa wakili mwenzie mashuhuri wa kesi John J. Flynn, akatafuta mtaalam mwingine wa sheria na katiba, John P. Frank, wote kwa pamoja kusaidina katika kukata rufaa kwa Mahakama ya Juu kabisa nchini Marekani. @Nkololotz

Wakili Frank Katika muhtasari wake kwa niaba ya Miranda, aliandika,

"Siku ni hii leo kutambua umuhimu wa kufanya marekebisho ya sheria sita.

"Marekebisho ya sita ya sheria ya uendeshaji kesi za jinai yanahakikisha haki za washtakiwa wa jinai pamoja na haki ya kuwa na wakili.

"Pia katika mfuatano huo Marekebisho ya Tano ya sheria hiyo yanawalinda washtakiwa dhidi ya kulazimishwa kuwa mashahidi wa kesi zao wenyewe.

"Ingawa Miranda alikuwa ameandika taarifa ya kukiri kwake na chini ya taarifa alisema kwamba alikuwa anajua kabisa haki zake za kisheria"

"wakili wake alisema haki hizo hazijafafanuliwa wazi kwake. Hivyo chini ya shinikizo la kukiri akiwa kizuizini, kukiri kwake hakukupaswa kuchukuliwa kuwa alikubali kutenda kosa."

UAMUZI WA KIHISTORIA

Mahakama Kuu, chini ya Jaji Mkuu Earl Warren, ilikubali.Katika uamuzi wa 5-4, Mahakama Kuu ilibadilisha uamuzi wa Mahakama Kuu ya Arizona na kutangaza kwamba kukiri kwa Miranda hakuwezi kutumiwa kama ushahidi katika kesi ya jinai.

Pichani: Jaji Earl Warren

Maoni ya Jaji Warren yaliyoandikwa kwenye kurasa 60 pamoja na marejeo, yaliyotolewa Juni 13, mwaka 1966, kufafanua zaidi utaratibu wa polisi ktk utendaji wa shughuli zao na kuhakikisha washtakiwa wanafahamishwa wazi haki zao wanapokuwa wakizuiliwa (chini ya ulinzi) na kuhojiwa.

Baadae kesi ya Miranda ilirudishwa kusikilizwa tena mahakamani na kile kiapo alichokiri kutenda jinai kilitupiliwa mbali lakini wakati huu mahakama ilibadilisha mwenendo mzima wa utaratibu wa uendeshaji kesi za jinai na hii ilikuwa ni mahakama zote nchini Marekani.

Kwa mara nyingine kesi iliunguruma mahakamani, lkn kwa bahati mbaya mpenzi wake wa zamani, Twila Hoffman, alitoa ushahidi kwamba kipindi Miranda alipokuwa gerezani alimwambia kuwa alihusika kweli, na mnamo Oktoba 1967, Miranda akahukumiwa tena kuhukumiwa kifungo cha miaka 20-30.

Alibahatika kuachiwa kutoka jela kwa msamaha Desemba mwaka 1975 baada ya kukaa jela kwa miaka 8 lakini kuishi kwake hakukuwa kwingi mwezi mmoja tu baadaye mnamo Januari 31, 1976, aliuawa kwa kuchomwa kisu hadi kufa kutokana na ugomvi katika baa moja mitaa ya Phoenix.

#Mwisho: kutokana matukio ya kesi hii muhimu Ernesto Miranda, kila mmoja wetu hasa hapa nchini inapaswa atambue kuwa ni lazima afahamishwe haki zake za kimsingi awapo kizuizini (chini ya ulinzi) na anapohojiwa.
#Ahsante
RT is caring
Cc. @franklin_tissa @INFLUENCERjr
@TitoMagoti

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling