JAPHET MATARRA Profile picture
Jun 13, 2021 35 tweets 15 min read Read on X
"YOU ARE UNDER ARREST"

#Uzi

📌Je, wajua Leo ilikuwa siku ambayo sheria inayomlinda mhumiwa [Miranda rights/Warnings] anapokamatwa na vyombo ulinzi ilipitishwa huko marekani?

💨YES it's Miranda Vs Arizona case

📌 Historia yake

📌 Chanzo chake

📌Maamuzi ya kihistoria.

👇👇 ImageImage
Mnamo Juni 13, 1966 Mahakama Kuu ya Juu (Supreme Court) nchini Marekani ilitoa uamuzi wa kihistoria juu ya taratib za uendeshaji kesi za jinai mahakamani.Uamuzi huo ulitokana na kesi ya Miranda Vs Arizona kwamba watuhumiwa wa kesi wanazo haki zao kabla ya kuhojiwa wawapo kizuizin Image
Nadhani ulishawahi kusikia maneno haya

1. Una haki ya kukaa kimya.

2. Chochote unachosema kinaweza, na kitatumika, kama ushahidi mahakamani.

3. Una haki ya kuwa na wakili.

4. Ikiwa hauwezi kumudu gharama za wakili mahakama, itamteua mmoja kusimamia kesi zako

Tuendelee 👇 Image
Hapa nchini sheria inayoratibu uendeshaji wa mashauri ya makosa ya jinai yanayohusu watu wazima iko chini ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 1985 kwenye sura ya 20. Lkn zipo sheria nyingine mbalimbali ambazo zinahusiana na uendeshaji wa mashauri ya makosa ya jinai.
Halikadhalika, ili kukamilisha utaratibu wa uendeshaji wa mashauri ya jinai kuna Sheria ya Ushahidi ya mwaka 1967, sura namba 6, inayoelekeza aina ya ushahidi, taratibu za kutoa ushahidi. Lengo langu sio hili bali ya kukuletea chanzo cha sheria hizi na taratibu za uendeshaji kesi Image
#Chanzo ni Miranda v. Arizona case, 384 U.S. 436 (1966)

Miranda vs. Arizona case ilikuwa kesi kubwa iliyofuatiliwa na kusisimua ulimwengu wote kutoka ktk Mahakama Kuu ya Jimbo la Arizona nchini Marekani.
RT. @Mangiwakwanza @biturojr @adamlutta @IAMartin_ @Gaspinho15 @Nkololotz Image
Kesi hii ilihusisha tuhuma za binti mmoja kubakwa na baadae ikaonekana polisi wa mjini Arizona wakiwa wamemfikisha kijana kwamba ndiye alihusika na jinai ile na kisha akahukumiwa kutokana na taarifa iliyolewa na polisi kwamba alikiri kufanya tukio lile.
@CarolNdosi @jtemba321 Image
HISTORIA

Mnamo Machi 2, mwaka 1963 katika mitaa ya Phoenix, huko Arizona nchini Marekani. Ikiwa ni mida ya usiku binti mmoja Patricia McGee (sio jina lake halisi) mwenye umri wa miaka 18 akiwa barabarani kuelekea nyumbani akitokea kwenye ukumbi wa sinema alikokuwa akifanya kazi Image
Ghafla alitokea mtu aliyekuwa kwenye gari na kumkamata kwa nguvu akamfunga mikono nyuma na kumlazimisha alale kwenye kiti cha nyuma.
Baada ya kuendesha kwa takribani dakika 20, alilisimamisha gari pembezoni mwa barabara mbali kidogo ya jiji na kumbaka. Image
Baada ya kumbaka alimlazimisha ampe pesa zake zote alizokuwa nazo la sivyo angemuua na kisha akamwambia alale tena kwenye kiti cha nyuma, kisha akamrudisha mjini na kumuachia maeneo ya karibu na nyumba kwao.
Binti yule alipofanikiwa kufika nyumbani na alichukua simu akawapigia polisi kuomba msaada, walipofika ndipo aliwaeleza mkasa uliomtokea na kuwaambia muonekano wa kisura, kiumbo wa mtu aliyemfanyia unyama huo na plate namba za gari kisha wakampeleka hospitali kupatiwa matibabu. Image
Polisi waliendelea na zoezi la kumtafuta mhalifu na siku chache baada ya tukio kutokea Patricia na binamu yake walikwenda polisi na kutoa taarifa ya kuona gari moja linalofanana na lile likiwa linapita mara nyingi ktk kituo cha mabasi ambapo alitekwa. Image
Polisi walifuatilia gari lile na kufahamu lilikuwa likimilikiwa na mwanamke aitwaye Twila Hoffman (29) aliyekuwa akiishi Mesa huko Arizona. Hoffman alikuwa ni mpenzi wa Miranda na wote walikuwa wakiishi pamoja. Image
Wakapata mkanganyiko wa kuendelea kutafuta mhalifu baada ya kujua mmiliki wa gari ni jinsi ya kike. Lakini hawakuishia hapo waliamua kwenda kwake Hoffman ili kumkamata na kwamba huenda anafahamu aliyefanya unyama ule kwa kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alitumia gari lake.
mnamo Machi 13 asbh Polisi walimbishia mlango Hoffman, akafungua na wakamweleza kilichowapeleka nyumban kwake. Baada ya kusikia polisi wapo ndani Ernesto Miranda kijana mwenye umri wa 24 na mwanafunzi wa Sekondari A-level kwa mujibu wa maelezo ya polisi akajitokeza kuzungumza nao Image
Miranda alifanya vile ili kunusuru penzi lake kwani alijua yeye ndiye anatafutwa akawaomba waondoke naye wakazungumzie kituoni. Kiufupi Miranda akakamatwa na polisi na moja kwa moja kituoni kwa tuhuma za uhalifu na jinai ya utekaji nyara, kumbaka na kumuibia binti Patricia. Image
CHUMBA CHA MAHOJIANO

Alihojiwa na wapelelezi maswali mengi kwa muda wa masaa mawili bila kuwepo Wakili wake, ambapo baadae alikiri kutenda uhalifu huo. Baada ya hapo wapelelezi walimleta mwathiriwa ndani ya chumba polisi mmoja wao alimuuliza Miranda "huyu ndiye mtu aliyembaka?" Image
Miranda alimwangalia na kusema "Ndio, msichana alikuwa huyo" akakiri na kisha kusaini kwa maandishi.

Karatasi ile ilisema "haya ni maelezo yangu binafsi na nakiri nimeyatoa kwa hiari na haki zangu nazielewa,hivyo maelezo haya yatumike mahakamani kama ushahidi na sio vinginevyo"
Maelezo yale yalichukuliwa kama ushahidi mahakamani ingawa hakukuwa na haki maalum zilizoorodheshwa kwenye karatasi ile kama yanavyosema.Akasomewa mashataka mahakamani na alihukumiwa kwa uhalifu huo na Mahakama ya Arizona kutumikia kifungo cha miaka 20 mpk 30 jela.
@rollymsouth Image
Baadaye, Wakili wake Alvin Moore alihisi kwamba kukiri kwake Miranda hakukuwa na ukweli kutokana na ukweli kwamba hakuwa anafahamu haki yake ya kimsingi ya kuwa na wakili atakaye mwakilisha na aidha kwamba maneno yake ya awali yangeweza kutumika kama ushahidi wa maneno dhidi yake Image
Baada ya miezi 6 Wakili Alvin aliamua kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Jimbo la Arizona kwamba hakukubaliana kuwa kukiri kwa maandishi ya mteja wake na kuongeza kuwa huenda maelezo yalitokana na kulazimishwa, hivyo akaisisitiza mahakama ktk uamuzi ilioutoa kuangalia hilo. Image
Rufaa ya kesi hii katika Mahakama kuu ndiyo ilibadilisha kabisa utaratibu wa uendeshaji wa kesi za jinai nchini Marekani nadhani hata ktk nchi nyingi duniani.

Katika rufaa Wakili Alvin alihoji Mahakama maswali yafuatayo.

"Je! Taarifa yake [Miranda] ilitolewa kwa hiari?" na Image
Je, "Alipewa kinga zote za haki zake zinazotolewa na Katiba ya Marekani kwa kuzingatia sheria na kanuni za uendeshaji kesi mahakamani?"

Rufaa yake ilijibiwa na Mahakama Kuu ya Arizona mnamo Aprili 1965 kwamba kukiri kwa Miranda kulikuwa halali na kwamba alikuwa akijua haki zake.
Baada ya uamuzi huo kutolewa ndipo kesi ya Miranda ilianza kuvutia macho watu mbalimbali ikiwemo mawakili wa kimataifa. Kutokana na kuchukua sura mpya ktk Jimbo la Arizona, Robert Corcoran ndipo aliibuka na ACLU (American Civil liberties Union) Umoja wa Uhuru wa Kiraia wa Amerika Image
Wakili Corcoran akaamua kuivalia njuga kesi hii akaenda kwa wakili mwenzie mashuhuri wa kesi John J. Flynn, akatafuta mtaalam mwingine wa sheria na katiba, John P. Frank, wote kwa pamoja kusaidina katika kukata rufaa kwa Mahakama ya Juu kabisa nchini Marekani. @Nkololotz Image
Wakili Frank Katika muhtasari wake kwa niaba ya Miranda, aliandika,

"Siku ni hii leo kutambua umuhimu wa kufanya marekebisho ya sheria sita.

"Marekebisho ya sita ya sheria ya uendeshaji kesi za jinai yanahakikisha haki za washtakiwa wa jinai pamoja na haki ya kuwa na wakili. Image
"Pia katika mfuatano huo Marekebisho ya Tano ya sheria hiyo yanawalinda washtakiwa dhidi ya kulazimishwa kuwa mashahidi wa kesi zao wenyewe.

"Ingawa Miranda alikuwa ameandika taarifa ya kukiri kwake na chini ya taarifa alisema kwamba alikuwa anajua kabisa haki zake za kisheria"
"wakili wake alisema haki hizo hazijafafanuliwa wazi kwake. Hivyo chini ya shinikizo la kukiri akiwa kizuizini, kukiri kwake hakukupaswa kuchukuliwa kuwa alikubali kutenda kosa."
UAMUZI WA KIHISTORIA

Mahakama Kuu, chini ya Jaji Mkuu Earl Warren, ilikubali.Katika uamuzi wa 5-4, Mahakama Kuu ilibadilisha uamuzi wa Mahakama Kuu ya Arizona na kutangaza kwamba kukiri kwa Miranda hakuwezi kutumiwa kama ushahidi katika kesi ya jinai.

Pichani: Jaji Earl Warren Image
Maoni ya Jaji Warren yaliyoandikwa kwenye kurasa 60 pamoja na marejeo, yaliyotolewa Juni 13, mwaka 1966, kufafanua zaidi utaratibu wa polisi ktk utendaji wa shughuli zao na kuhakikisha washtakiwa wanafahamishwa wazi haki zao wanapokuwa wakizuiliwa (chini ya ulinzi) na kuhojiwa. Image
Baadae kesi ya Miranda ilirudishwa kusikilizwa tena mahakamani na kile kiapo alichokiri kutenda jinai kilitupiliwa mbali lakini wakati huu mahakama ilibadilisha mwenendo mzima wa utaratibu wa uendeshaji kesi za jinai na hii ilikuwa ni mahakama zote nchini Marekani.
Kwa mara nyingine kesi iliunguruma mahakamani, lkn kwa bahati mbaya mpenzi wake wa zamani, Twila Hoffman, alitoa ushahidi kwamba kipindi Miranda alipokuwa gerezani alimwambia kuwa alihusika kweli, na mnamo Oktoba 1967, Miranda akahukumiwa tena kuhukumiwa kifungo cha miaka 20-30. Image
Alibahatika kuachiwa kutoka jela kwa msamaha Desemba mwaka 1975 baada ya kukaa jela kwa miaka 8 lakini kuishi kwake hakukuwa kwingi mwezi mmoja tu baadaye mnamo Januari 31, 1976, aliuawa kwa kuchomwa kisu hadi kufa kutokana na ugomvi katika baa moja mitaa ya Phoenix. ImageImage
#Mwisho: kutokana matukio ya kesi hii muhimu Ernesto Miranda, kila mmoja wetu hasa hapa nchini inapaswa atambue kuwa ni lazima afahamishwe haki zake za kimsingi awapo kizuizini (chini ya ulinzi) na anapohojiwa.
#Ahsante
RT is caring
Cc. @franklin_tissa @INFLUENCERjr
@TitoMagoti ImageImage

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with JAPHET MATARRA

JAPHET MATARRA Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Eng_Matarra

Oct 19, 2021
NANI ALIYEMUUA SOKOINE?

#UZI

🔲Mnamo April 12, 1984 ilikuwa ni siku mbaya sana ktk Taifa letu na haitosahaulika kwa Watanzania. Siku hiyo tulimpoteza kijana makini aliyekuwa Waziri Mkuu EDWARD MORINGE SOKOINE, aliyefariki kwa ajali mbaya ya gari eneo la Wami-Dakawa (Morogoro). ImageImageImage
🔲SOKOINE mmoja wa viongozi bora nchini amefariki miaka 37 iliyopita akiwa na miaka 46. Ikiwa ulizaliwa kpnd hicho sasahv ushakuwa na watoto na pengine unaelekea wajukuu.

🔲Ingawa historia tumesoma ndio, ILA #chanzo cha kifo chake bado kuna utata kuna maswali YasiYo na majibu. Image
🎤Nimeamua tufukue makaburi najua hukuambiwa haya💣⤵️

🔲Hv NANI HASA ALIYEMUUA SOKOINE?

🔲ILIKUWAJE AKAGONGWA NA GARI La "Private" #KATIKATI Ya MSAFARA na kupelekea kifo chake (Tujuavyo msafara wa VIP unakuwaga na ulinzi wa usalama, hakuna gari linaruhusiwa kutembea hadi upite) Image
Read 111 tweets
Sep 26, 2021
PUTIN ANAVYOPINDUA VIONGOZI WA AFRIKA KUJIIMARISHA

#UZI:

💨Rais Alpha Conde (Guinea) alipinduliwa kwa msaada wa USA & Ufaransa, lkn kwa ASSIMI GOÏTA (Mali) alisaidiwa na Urusi.Pia mauaji ya IDRIS DÉBY (Chad) yalifanywa na URUSI
👩‍💻𝐌𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐌𝐚𝐳𝐢𝐭𝐨 𝐓𝐮𝐬𝐢𝐲𝐨𝐲𝐚𝐣𝐮𝐚👇
Mnamo Aprili 20, 2021 majira ya jioni zilianza sherehe huko La Brasserie Kiss, umbali wa 100M kutoka ktkt ya mji wa Bangui (Afrika ya Kati). Kila aliyepita huo mtaa aliona magari kadhaa yamepaki mbele ya nyumba moja ya Ghorofa 3, jumba ambalo ni kivutio kikubwa sana ktk jiji hilo
Jengo hili lipo nje kidogo ya mtaa maarufu wa DU COLONEL CONUS na ikifika usiku hupendeza sana kutokana na mng'ao wa taa ulioizunguka. Kulingana na saa kule ilikuwa mida ya saa 2 usiku hivi na kwa wenyeji wa mji huo, ni muda ambao amri ya kutotembea usiku huanza kutumika.
Read 17 tweets
Sep 18, 2021
𝐂𝐈𝐀 ILIVYOTUMIA MWANAMUZIKI ARMSTRONG KUMUUA PATRICE LUMUMBA (Congo)

#Thread

Mnamo Sept 19, 1960, Mkuu wa CIA huko Leopoldville (sasa Kinshasa) alipokea SMS kupitia chombo cha siri kutoka wakuu wake huko Washington. Mtu aliyejiita 'Joe from Paris' ndiye aliyepiga simu na ..
kumwambia angefika Congo kwa ajili ya Operation maalum.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa. Baadae mkuu huyo alionywa kutozungumzia ujumbe huo na mtu yeyote. Wiki 01 baadae 'Joe' aliwasili nchini humo.

Leo nikiwa nasoma kitabu cha 𝐖𝐡𝐢𝐭𝐞 𝐌𝐚𝐥𝐢𝐜𝐞 (Author: SUZAN WILLIAMS)
kilichotoka Agosti 20, 2021, nimejikuta nikiumia sana nafsi baada ya kufahamu jinsi Marekani ilivyomuua Waziri Mkuu wa kwanza wa DR-Congo, mzalendo wa kweli, kijana mdogo mrefu, mwembamba miaka 36, kwasababu tu USA iliogopa Umoja wa Kisovieti (USSR) ikaamua kumuua.
Read 120 tweets
Sep 13, 2021
FULL OPERATION MAPINDUZI YA RAIS (GUINEA)

#Thread

Baada ya TALIBAN nchin Afghanistan, habari sasa ni MAMADY DOUMBOUYA kiongozi wa kijeshi huko Guinea, kumpindua rais na kuchukua madaraka #Unadhani kikosi kidogo cha SFG kiliwezaje kudhibiti kambi za kijeshi na kumkamata rais?👇
Yes, mwanajeshi wa zamani wa Ufaransa (French Legionnaire) aliyerudi nyumbani miaka 03 iliyopita na kuaminiwa na Rais ALPHA CONDÉ, ndiye aliyemsaliti na kumuondoa madarakani baada ya kutaka kuongoza nchi kwa muhula wa 03

MAMADY DOUMBOUYA ambaye ana cheo cha Kanali alionekana..
kwenye kituo cha Radio-Télévision Guinéenne(RTG), mnamo 5 Septemba majira ya saa 2 usiku, akiwa amevalia kofia nyekundu (Red Beret) ameweka bendera ya taifa hilo begani mwake, na kuzungukwa na wanajeshi wanane, akatangaza kuwa jeshi limechukua madaraka ya nchi.
Read 147 tweets
Sep 9, 2021
MAPINDUZI YA GUINEA TZ🇹🇿 YA SAMIA INACHAKUJIFUNZA

#UZI

Ilianza kama utani Mzee Condé hakuamini kijana wake mwenyewe aliyemlea, mwenye masters ya vita na cheo akampatia alipomwambia "simama juu hlf ukae chini" Unadhani ilikuwa rahisi kumpindua? Naam It's #Guinea:1958-Present👇
Sikuweza kuandika Uzi yalipotokea mapinduzi ktk nchi nyingine mbalimbali, lkn kwa yaliyotokea jumapili nchini Guinea nimeona niandike ili Watanzania tuone km kuna lolote la kujifunza. Nitaangazia upande wa kisiasa tu. Nitachambua kila kitu kuanzia uhuru hadi kutokea mapinduzi.
Maswali nayotaka kukujibu km ulijiuliza ni haya:👇

💨Historia ya Guinea ikoje?

💨Kwnn mpk mapinduzi?

💨Col. Doumbouya ana nguvu gani

💨Kwann wananchi wamefurahia?

History repeats itself, 1st as Tragedy, second as Farce.
Just retweet 🔄 huenda siku
Uzi huu ukakukumbusha kitu
Read 211 tweets
Aug 18, 2021
WHO is '𝐓𝐀𝐋𝐈𝐁𝐀𝐍'? WANATAKA NINI HASA AFGHANISTAN?

#𝕿𝖍𝖗𝖊𝖆𝖉:
Ifahamike, walikuwa yatima ktk kambi za wakimbizi Pakistan.
Je, wana uhusiano na AL-QAEDA? #Tragedy:UINGEREZA & URUSI kuchezea kipigo cha Mbwakoko.
✴️Chimbuko
📡Walio nyuma yao?
📋Tofauti yao na MUJAHIDINA..
Vita vya Marekani nchini Afghanistan vimedumu kwa takribani miaka 20. Nimeona watu wengi wakitoa maoni juu ya Jeshi la TALIBANI kuchukua nchi Lkn wengi hawana historia juu yake. Wengine wanasema Rais wa Marekani @JoeBiden mefanya 'makosa' kuondoa majeshi yake.
BIG NO __Hapana.
Wengi tusichojua ni kwamba, huu ulikuwa ni uhalifu wa kivita na DICK CHENEY, aliyekuwa Vice President wa G. W BUSH na DONALD RUMSFELD, Kiongozi Mkuu wa Ulinzi kipindi cha Vita ya IRAQ (alishafariki), ndio walioiingiza Marekani kwenye shida hii unaiona Leo, kisa wanamtafuta OSAMA
Read 114 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(