SANUKAnaCHAPO Profile picture
| Storyteller | Owner @usedpointtz | SON OF BONGO FLEVA | THE WALKING MEDIA | Binamu wa BARAKA MAVIATU |

Jul 29, 2021, 8 tweets

“NILIPEWA GARI ILI NISITOE STORY ZA WASAFI”

Kuna kauli wasanii wanapenda kuitumia kuwa “Wasanii wenyewe hatupendani” hii kauli wala si utani ni ukweli kabisa kuwa muziki wa Bongo Fleva licha ya kukuwa na kuanza kuwanufaisha wasanii ila vita imekuwa kubwa kila mtu anataka👇UZI

Keki kubwa zaidi ya mwengine kupelekea chuki,uongo,fitna na kurogana ila bahati nzuri bado hawajafikia kuuwana 😂.

Nataka leo nikusimulie kisa cha msanii wa Bongo Fleva kutaka kuwekeza kwenye online Tv kwa sharti moja tu wasitangaze habari za wasafi😳👇

Labda nikuweke sawa waandishi wa habari wanapenda sana hela wao hela kwanza kabla ya kazi yako, wako tuyari waje kufanya coverage ya mkutano wako ila usipowapa bahasha juwa tu hawatorusha tukio lako, nimefanya kazi na waandishi kwa ukaribu kwa zaidi ya miaka mi3 sasa, wana 👇

Miyeyusho kinoma noma. Achana na hii story let’s back to the business, msanii ninaye mzungumzia hapa yupo kwenye Top 4 ya wasanii wakubwa nchini na amekuwa akifanya kazi na waandishi kwa ukaribu sana na kwa mujibu wao jamaa hana roho mbaya mtakula anachokula na 👇

Mtalala anapolala pale anapokuwa na show zake mikoani anawalipa hela nzuri tu.

Kuna moja ya online Tv amekuwa akifanya nayo kazi kwa muda mrefu na kujenga nayo ukaribu siku moja alimuita na kumpatia gari aina ya Noah kama shukrani ili imsaidie boss wa online Tv kwenye👇

Shughuli zake za habari, jamaa akachukua Noah na kwenda kuji brand na kubandika cover za jina la kampuni(mwana hajapewa kadi 😂 ila kajiongeza).

Baada ya muda kupita ndipo kasheshe liliopoanza(cha ntu nnya😂). Jamaa akaambiwa na msanii “kuanzia sasa sitaki utoe habari kuhusu 👇

Wasafi yaani hata kwa bahati mbaya na cha pili nataka share kwenye hii kampuni yako na mimi”😳😳

Boss wa Online Tv akaona hii sasa dhahama,mambo gani haya! Sasa nisiporusha story za wasafi itakuwaje na jamaa ndio chanzo cha content mjini kiki zote zipo huko daah na kuhusu👇

Share ni sawa hakuna kampuni haitaki kukuwa ila sharti la kwanza ni gumu mno.

Jamaa akakogoma na kurudisha gari ya watu akaona bora akose ndinga ila asijiaribie.

-MWISHO

#CodeZaChapo #ChapoWasHere #SanukaNaChapo

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling