Dr. Mlaluko, MD Profile picture
|MedicalDoctor|Author|TheResident|Poet|HealthJournalist|Father (Ammar, Raiyyan&Rufaydah)|HealthEyeAdvocate|SelfMotivated|Founder @jukwaalaafya|

Oct 9, 2021, 7 tweets

#FAHAMU: VYAKULA BORA KWA WATOTO WADOGO KULINGANA NA UMRI WAO.

Watoto wanahitaji vyakula maalumu tangu wakiwa wadogo kwa ajili ya kuboresha afya zao na kuimarisha kinga ya miili yao ili kuepusha udumavu na kumkinga dhidi ya magonjwa mbalimbali kama PNEUMONIA, kuharisha n.k
#UZI

MIEZI SITA YA AWALI
Mtoto anahitajika kupata maziwa ya mama yake pekee bila kuhitajiwa kupewa kitu kingine kama maji/ juisi katika kipindi hiki. Isipokuwa anahitajika kupata chanjo ya matone au dawa. Mtoto anyonyeshwe usiku na mchana isiyopungua mara 10 kwa masaa 24.

MIEZI 6-9
Mtoto anyonyeshwe kwa jinsi atakavyohitaji.Muanzishie uji au vyakula vya kupondwa(Viazi,ndizi, samaki,nyama) kwa kuanzia vijiko 2-3 vya mezani kila baada ya masaa 12.Akifiksha miezi 7 ongeza kiasi mpaka 2/3 ya kikombe cha 250mls kila baada ya masaa 8.
#ElimikaWikiendi

MIEZI 9-12
Endelea kumnyonyesha atakavyo. Mpatie mchanganyiko wa vyako vilivyopondwapondwa. Mpatie robo-tatu (3/4) ya kikombe cha 250mls kila baada ya masaa nane (kutwa mara tatu). Na pia mpatie vitafunwa (snacks) mara moja ndani ya masaa 24.
#ElimikaWikiendi #ElimikaWikiendi

MIEZI 12-MIAKA 2
Mnyonyeshe mtoto kwa jinsi anavyohitaji. Mpatie vyakula vya kupondwa au vyakula mnavyokula kama familia katika chombo/sahani lake. Apate milo 3 na kila mlo isipungue kikombe kilochojaa cha ujazo wa 250mls. Pia kati ya mlo na mlo mwingine apate vitafunwa (snacks)

MIAKA 2-MIAKA 5
Ale chakula cha familia kama wali, ugali, ndizi n.k kutwa mara 3. Na kati ya mlo na mlo mwingine apate cha kuweka mdomoni (snacks) kama maziwa, juisi freshi, chai au kitafunwa na sio SODA. Zaidi, mpe muda mtoto kucheza na kupumzika ipasavyo.
#ElimikaWikiendi

@threadreaderapp compile it

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling