Dr. Mlaluko, MD Profile picture
Oct 9, 2021 7 tweets 7 min read Read on X
#FAHAMU: VYAKULA BORA KWA WATOTO WADOGO KULINGANA NA UMRI WAO.

Watoto wanahitaji vyakula maalumu tangu wakiwa wadogo kwa ajili ya kuboresha afya zao na kuimarisha kinga ya miili yao ili kuepusha udumavu na kumkinga dhidi ya magonjwa mbalimbali kama PNEUMONIA, kuharisha n.k
#UZI ImageImageImageImage
MIEZI SITA YA AWALI
Mtoto anahitajika kupata maziwa ya mama yake pekee bila kuhitajiwa kupewa kitu kingine kama maji/ juisi katika kipindi hiki. Isipokuwa anahitajika kupata chanjo ya matone au dawa. Mtoto anyonyeshwe usiku na mchana isiyopungua mara 10 kwa masaa 24. ImageImageImage
MIEZI 6-9
Mtoto anyonyeshwe kwa jinsi atakavyohitaji.Muanzishie uji au vyakula vya kupondwa(Viazi,ndizi, samaki,nyama) kwa kuanzia vijiko 2-3 vya mezani kila baada ya masaa 12.Akifiksha miezi 7 ongeza kiasi mpaka 2/3 ya kikombe cha 250mls kila baada ya masaa 8.
#ElimikaWikiendi ImageImageImageImage
MIEZI 9-12
Endelea kumnyonyesha atakavyo. Mpatie mchanganyiko wa vyako vilivyopondwapondwa. Mpatie robo-tatu (3/4) ya kikombe cha 250mls kila baada ya masaa nane (kutwa mara tatu). Na pia mpatie vitafunwa (snacks) mara moja ndani ya masaa 24.
#ElimikaWikiendi #ElimikaWikiendi ImageImage
MIEZI 12-MIAKA 2
Mnyonyeshe mtoto kwa jinsi anavyohitaji. Mpatie vyakula vya kupondwa au vyakula mnavyokula kama familia katika chombo/sahani lake. Apate milo 3 na kila mlo isipungue kikombe kilochojaa cha ujazo wa 250mls. Pia kati ya mlo na mlo mwingine apate vitafunwa (snacks) ImageImageImageImage
MIAKA 2-MIAKA 5
Ale chakula cha familia kama wali, ugali, ndizi n.k kutwa mara 3. Na kati ya mlo na mlo mwingine apate cha kuweka mdomoni (snacks) kama maziwa, juisi freshi, chai au kitafunwa na sio SODA. Zaidi, mpe muda mtoto kucheza na kupumzika ipasavyo.
#ElimikaWikiendi ImageImageImageImage
@threadreaderapp compile it

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Dr. Mlaluko, MD

Dr. Mlaluko, MD Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @drmlalukoMD

May 4, 2022
#FAHAMU: UGONJWA VIDONDA VYA TUMBO

Ni ugonjwa unaopelekea ukuta wa tumbo kuvimba (inflammation) au kulika (ulceration) kutokana na kiwango cha asidi kuzalishwa kwa wingi tumboni.

Tatizo hili niweza kusababishwa na sababu mbalimbali kama....
• Kunywa pombe,
• Kuvuta sigara,
• Mkazo/msongo wa mawazo (stress)
• Kuungua mwili (curling ulcer)
• Kuumia kwa ubongo hupelekea 'Cushing ulcer',
• Matumizi ya dawa za maumivu (NSAIDS) kama diclofenac, ibuprofen kwa muda mrefu
• Gastrinoma; uvimbe unaozalisha ASIDI
• Maambukizi ya bakteria aina ya HELICOBACTER PYLORI. Huyu ni bakteria ambaye anaambukizwa kwa njia ya kula chakula/matunda,/kachumbari au kunywa kinywaji yenye mdudu huyo.

Kuna aina kuu mbili za vidonda vya tumbo; vidonda kwenye ukuta wa mfuko wa chakula (gastric) na duodenal
Read 12 tweets
Sep 18, 2021
#FAHAMU: ATHARI ZA UTOFAUTI WA KUNDI LA DAMU KATI YA MUME NA MKE.
Kuna baadhi ya wanawake wanapoteza mimba zao na wengine kupoteza watoto wao baada ya kujifungua sababu ikiwa ni utofauti wa kundi la damu kati ya mume na mke. Katika makundi ya damu kuna kitu kinaitwa RHESUS FACTOR ImageImageImageImage
Kulingana na rhesus factors kuna makundi yafuatayo ya damu A+, A-, B+, B-, AB+, AB-, O+, O-.

Katika makundi ya damu mara nyingi mtoto hufuata damu ya baba. Hivyo, ikiwa kundi la baba lina antigen ya rhesus factor (A+, B+, AB+, O+) na mama akiwa hana hiyo antigen(A-,A-,AB-,A-) Image
Mtoto katika ujauzito wa kwanza atakuwa kama kundi la baba (rhesus positive) na hivyo mwili wa mwanamke utatengeza kinga (antibodies) dhidi kundi la baba. Hivyo katika mimba zinazofanya kiumbe kitakuwa kinashambuliwa na kinga ya mama (Rhesus incompatibility)
#ElimikaWikiendi ImageImage
Read 8 tweets
Oct 19, 2020
TATIZO LA MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI VIZURI (HEART FAILURE).
Moyo ni kiungo muhimu ktk mwili kinachotumika kusambaza/kupokea damu sehemu mbalimbali mwilini (mapafu, ubongo, figo, matumbo n.k). Hivyo, moyo kushindwa kufanya kazi hupelekea mwili kukosa hewa na chakula.
#Thread
SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA MOYO KUSHINDWA KAZI.
1. Shinikizo la damu lisilothibitiwa barabara
2. Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital)
3. Magonjwa ya mishipa ya moyo (coronary artery d'se/ischemic heart d'se)
4. Magonjwa ya tezi shingo (thyroid dysfunction) n.k
WATU WALIO KTK HATARI YA KUPATA TATIZO HILO NI;
1. Wenye shinikizo la damu
2. Kisukari
3. Wenye uzito mkubwa (obesity)
4. Watumiaji wa pombe na sigara
5. Wenye historia ya matatizo ya moyo kwenye familia yao n.k
Read 7 tweets
Oct 18, 2020
TATIZO LA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI (KIDNEY FAILURE).
Figo ni kiungo muhimu sana kwenye mwili wa binadamu kwani hutumika kutoa takamwili kama; urea, maji ya ziada, chumvi n.k. Kushindwa kwa figo hupelekea takamwili kubakia mwilini hivyo kumletea shida mgonjwa.
#Thread
SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI.
1. Kisukari
2. Shinikizo la damu
3. UKIMWI
4. Matumizi ya muda mrefu ya dawa zinazoweza kuathiri figo mfano; dawa za maumizi (diclofenac, ibiprofen n.k)
5. Matumizi ya miti-shamba
6. Pombe yaliyozidi
7. Ugonjwa wa figo kuwa na vifuko vyenye maji (polycystic kidney disease)
8. Matatizo yanayoweza kupoteza maji mwilini. Mfano; kutapika sana, kuharisha sana n.k
9. Maambukizi kwenye damu (sepsis).
Read 7 tweets
Aug 1, 2020
FAIDA ZA KUNYONYESHA KWA MAMA NA MTOTO KIAFYA
Kutokana na utandawazi na harakati za maisha wanawake waliojifungua wamelazimika kutokunyonyesha watoto wao sawa sawa. Kitaalamu mtoto anatakiwa kunyonya miezi sita bila kupewa chakula isipokuwa dawa na chanjo tu
#UZI
FAIDA KWA MAMA
1. Kumpunguzia hatari ya kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua
2. Ni njia moja wapo ya kupanga uzazi
3. Kumlinda dhidi ya kansa ya matiti na kansa ya kizazi
4. Kumjengea uhusiano mzuri na mtoto
FAIDA KWA MTOTO
1. Kuimarisha kinga ya mwili na kumlinda magonjwa mfano; magonjwaya upumuaji na magonjwa ya mfumo wa chakula kama vile KUHARISHA
2. Kumjengea uhusiano mzuri na mama yake. Hivyo kumfanya mtoto awe ni mwenye furaha na kuchangamka
Read 7 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(