HabariTech Profile picture
Ulimwengu wa Teknolojia kiganjani mwako. #HabariTech

Oct 12, 2021, 19 tweets

📡Mass Surveillance Afrika na Duniani kote.

Huu ni uchunguzi ambao unajikita kufatilia umati mkubwa wa watu na mara nyingi huwa kwa kigezo cha kupunguza uharifu na kuzuia ugaidi.

Mass surveillance inasemakana kuanza miaka ya 3800 kabla ya kristo huko Babylon.

#HabariTech

📡Kwa vizazi vya sasa Mass Surveillance haikuonekana mpaka miaka ya mwisho ya 1940s baada ya UK na USA walikubaliana kubadilishana taarifa za intelejensia.

Baadae katika makubaliano haya ziliongezeka Canada, Australia na New Zealand na kufanya muunganiko huu kuitwa “Five Eyes”.

📡Muungano huu baadae mwaka 1971 ulileta kitu kilichoitwa “Global Surveillance Network” ambayo ilipewa jina la “ECHELON”.

ECHELON ni mtandao maalum wa uliofuatilia mawasiliano ya kijeshi na kidiplomati ya Soviet Union na washirika wake wa Mashariki kipindi cha Vita Baridi.

📡Kufikia mwisho wa karne ya 20 “ECHELON” ilitoka kufatilia mawasiliano ya kivita na diplomati mpaka kuanza fatilia mawasiliano binafsi ya mtu mmoja mmoja nay a kampuni.

Turuke mbele mpaka karne ya 21. Bilas haka umeshasikia neno NSA?

📡NSA ni shirika la juu kabisa la intelejensia la USA. Shirika hili lilianzishwa na Raisi Harry Truman mwaka1952, lakini liliendeshwa kwa siri mpaka mwaka 1975.

📡Huku kwetu wengi walilifahamu/kusikia kuhusu NSA mwaka 2013 Edward Snowden alipotoa siri kwamba NSA wanafanya Mass Surveillance ya Wamarekani na watu wote duniani bila idhini yetu.

Baada ya kujulikana NSA waliacha kufanya hivyo? Hapana, kazi iliendelea kama kawaida.

📡Marekani waliipa hii kitu jina la Mass Surveillance State kwa kigezo cha kwamba wanafanya hivyo ili kujilinda dhidi ya matukio ya kigaidi kama lile la 9/11.

Sio Marekani pekee wanaofanya hivyo. China pia wanahusika na Mass Surveillance.

📡China mwaka 2005 walianzisha mtandao wa Camera za kufanya mass surveillance ulioitwa Skynet.

Serikali ya China ilikuja kuweka wazi kuhusiana na mtandao huu mwaka 2013 baada ya kufunga CCTV cameras 20 million ndani ya China.

📡Hizo ni zile tu zinazomilikiwa na serikali ya China bila kujumuisha za Kampuni na Watu binafsi.

Kufikia June mwaka huu serikali ya China ndiyo inayoongoza kumiliki camera za CCTV zinazofanya kazi ya kufatilia watu wake.

📡Dunia nzima kuna CCTV camera 770 million, kati ya hizo China inamiliki CCTV 415.8 Million (54% ya zilizopo).

Serikali hizi zikiulizwa maoni yao ni kwamba camera hizi zinawasaidia kupunguza uhaifu, Usalama barabarani na kufatilia uendashaji wa viwanda.

📡Wasichotuambia ni namna zinatumika kuchunguza maisha ya watu. CCTV za kisasa zinaweza kufanya mpaka facial recognition, kufanya video streaming remotely.

Hivi ni vitu ambavyo huko mbeleni vitaingilia privacy ya mtu.

📡Kwa namna moja zinasaida mfano Polisi wa New Delhi india walipoamua kutumia CCTV zenye facial recognition. Ndani ya siku 4 ziliwasaidia kuwapata watoto 3000 walioripotiwa kupotea.

Huko china CCTV za hivi zina historia mbaya kwa kiasi kikubwa.

📡Mara kadhaa zimekuwa zikiwatambua watu wenye ndevu nyingi na wanatumia milango ya nyuma kutoka majumbani mwao kama magaidi.

Na kuna baadhi mpaka sasa wapo chini ya ulinzi baada ya kukutwa na app ya Whatsapp kwa sababu imezuiliwa nchini China.

📡Baadhi ya nchi za Afrika zimeanza kuingia katika mfumo huu polepole kwenye baadhi ya miji yao.

Miji kama Nairobi (Kenya), Johannesburg (South Africa), Addis Ababa(Ethiopia) na Kampala (Uganda).

📡Africa inatumia teknolojia tofauti tofauti kutoka mataifa ya nje kufanya mass surveillance.

Teknolojia kutoka Israel, Germany na China ndizo zinatumika kwa wingi zaidi. Kutoka Israel teknolojia za kutfatilia mawasiliano wa watu ndizo zinatumika zaidi Afrika.

📡Nchi za Afrika zilizoonekana kutumia hizi teknolijia zaidi ni Botswana, Nigeria na Zimbabwe.

Katika nchi 13 za Afrika zinazofanya Mass Surveillance ikiwemo Tanzania kulingana na taarifa ya “Africa Center” zote bado zinashida kubwa ya demokrasia.

📡Serikali za nchi hizi zinafanya uhalifu wa kufatilia mawasialiano ya wanachi wao kinyume na sharia za mitandao.

Na mbaya zaidi ni kwamba katika nchi hizi hakuna hata moja yenye sharia za ulinzi wa data za kimtandao na kama inazo basi bado zina mianya mingi.

📡Utumiaji wa bidhaa za ufuatiliaji Africa unahiska zaidi na project ya Huawei ya Safe cities. Kulingana na Huawei wamesema kwa Kenya imesadia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa.

Lakini polisi wa kenya walisema ni kinyume cha hivyo.

📡Afrika kwa sasa ipo katika mabadiliko ya kidijitali. Kuna haja ya kuwa na uelewa wa haki zetu za kidijitali, lakini pia kujua namna tunaweza kulinda haki zetu mtandaoni.

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling