Dr. Norman Jonas Profile picture
Medical Doctor | Internal Medicine - Kilimanjaro Christian Medical University College | Always a Beautiful Day to Save Lives | norman.jonas@kcmuco.ac.tz

Oct 29, 2021, 12 tweets

#DondooZaDaktari | Leo ni siku ya #KIHARUSI #WorldStrokeDay

➡️Tatizo la dharura la kiafya ambalo ni moja ya magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo.

➡️Mitindo ya maisha na Lishe ni vitu vinavyochangia wagonjwa wanaopata stroke kuongezeka

➡️Kiharusi huacha ulemavu au kifo

➡️KIHARUSI hutokea pale seli za ubongo 🧠 zinapokufa kutokana kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo hivyo kukosa hewa ya oksijeni na virutubisho.

➡️Kiharusi kikihusisha mshipa wa mkubwa wa damu kwa wastani mgonjwa hupoteza seli za ubongo (neuroni 1.9) kila dakika.

KUNA AINA KUU MBILI ZA KIHARUSIBrain

1️⃣Kiharusi kinachotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya damu ya ubongo

2️⃣Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo

🗒️80% ya watu wanaopata kiharusi hutokana na kuziba kwa mishipa ya damu kwenye ubongo.

Vitu ambavyo huchangia watu kupata kiharusi

1️⃣Ugonjwa wa Shinikizo kubwa la damu
2️⃣Ugonjwa wa kisukari
3️⃣Lehemu kuzidi kwenye damu
4️⃣Uvutaji sigara
5️⃣Magonjwa ya moyo
6️⃣Uzito uliopitiliza
7️⃣Unywaji wa pombe uliokithiri
8️⃣Kutokufanya mazoezi

Lishe ni muhimu sana katika kupunguza hatari ya kupata kiharusi.

➡️Takribani 25% ya kesi za kiharusi uhusishwa na ulaji usiofaa

🗒️Boresha lishe kwa kuzingatia:
-Matunda kwa wingi
-Mboga za majani
-Punguza kiasi cha chumvi
-Punguza matumizi ya nyama nyekundu

➡️Shinikizo kubwa la damu huchangia watu wengi kupata kiharusi.

➡️Msukumo mkubwa wa damu kupasua mishipa ndani ya ubongo na kupelekea kiharusi

🗒️Pima presha yako mara kwa mara ili kama una presha uanze tiba mapema

Unene uliopitiliza na kitambi huchangia watu kupata kiharusi

➡️Unene husababisha mrundikano wa mafuta kwenye kuta ya mishipa ya damu ambayo ni kihatarishi cha kuziba kwa mishipa kwenye ubongo

🗒️Kupunguza uzito ni njia mojawapo ya kudhibiti kiharusi.

DALILI ZA KIHARUSI

1️⃣Ganzi au udhaifu upande mmoja wa mwili
2️⃣Kushindwa kuona ghafla
3️⃣Kushindwa kuongea au mdomo kupinda kuelekea upande mmoja
4️⃣Kichwa kuuma ghafla kama umepigwa nyundo kichwani
5️⃣Kupoteza fahamu, kuchanganyikiwa

"FAST" ni namna unayoweza kugundua kiharusi haraka na kutafuta msaada haraka

F-ace : Mdomo kupinda kulekea upande mmoja
A-rm : Kushindwa kunyanyua mkono
S-peech Kushindwa kuongea au kuongea maneno hayaeleweki
T-ime : Muda ni muhimu ili kuokokoa maisha, tafuta tiba ya haraka.

Be F.A.S.T to recognize #STROKE and save LIFE.

@pikaso_me please "screenshot this"

@pikaso_me please "screenshot this"

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling