HabariTech Profile picture
Ulimwengu wa Teknolojia kiganjani mwako. #HabariTech

Mar 15, 2022, 28 tweets

🎁T O R R E N T S, Zinafanya vipi kazi?

Naweka dau langu kwamba ukisikia torrents, kitu kinakuja kichwani mwako ni software, video au audio za wizi (Pirated Files).

Uko sahihi lakini, torrent protocol haihusiana na hivyo tu.

#HabariTech

🎁Torrents ni nini?

Kwanini pirates wanatumia torrents kusambaza na kupakua files zao?

Huduma nyingine za internet zinazoendana na torrents kwanini hazitumiki katika sharing ya pirated files?

Haya maswali yote yanapatiwa majibu kupitia Bittorrent protocol.

🎁Unapofungua browser ili kuperuzi mtandao, browser inatuma request kwenda kwenye server yenye IP address ya website unayotaka kuifikia.

Request hii inaenda kuiomba server ikupe HTML za hiyo website ili uweze kuiona na kufanya kitu unataka.

🎁Ombi lako likikubalika, kwamba server iko hewani na website unataka kuifikia ipo, jibu linarudi kwako kwa mfumo wa picha, video na maneno (Kama websites zinavyo onekana).

Hapa kila unapotafuta website au kwenda page mpya, browser yako inapakua hizi data kutoka kwenye server.

🎁Mtandao umeundwa na WWW.

Kila website unayoona mtandaoni ipo katika server moja au zaidi katika maeneo tofauti tofauti duniani.

Unapotaka kuifikia website kama habaritech.com request inatumwa kwa moja wapo ya server ndipo majibu yarudi kwako.

🎁Uhusiano huu unaitwa Client-Server Model.

Yani ni sawa na pale mtaani kwenu kuna duka 1 la mangi ila wateja wengi.

Mangi = Server
Wateja = Clients

Kwa maana hiyo client hautakuwa wewe pekee unayetuma request kwenye server.

Inawezekana clients 1000 mkatuma request kwa pamoja

🎁Itakuwaje sasa kama duka la mangi likafungwa?

Watu wote mtashindwa kupata mahitaji yenu kwa siku hiyo. Maana yake server inapoacha kufanya kazi, request zote kwenda kwenye server hazitajibiwa.

Client-Server ni uhusiano ambao uko centralized, na hii ndiyo moja ya hasara yake.

🎁Torrents

Torrents zinatumia BitTorrent protocol.

Hii ni Peer-2-Peer (P2P) protocol. Yaani mteja na mteja mnahudumiana wennyewe moja kwa moja.

Mama chausiku akihitaji mafuta ya kula anaenda kwa Mama Majuto. Hakuna haja ya duka la mangi.

🎁P2P protocol inaruhusu kila computer kwenye mtandao kuwasiliana zenyewe moja kwa moja.

Hapo nadhani umeona utofauti uliopo kati ya Client-Server Network na hii Peer-2-Peer Nerwork.

🎁Tunapopakua files kutoka torrent. Kwanza huwa tunapakua torrent file ambayo tunaenda itumia kwenye torrent client kama uTorrent (Micro Torrent).

Wengi huwa mnaita u-Torrent, ile sio U. ni herufi ya kigiriki yenye maana ya Micro.

🎁Torrent client ndiyo inaanza pakua file yetu tunayotaka kama vile movie ya Batman 2022.

Ile .torrent file ya Batman tuliyo ipakua imebeba Metadata kuhusu movie ya Batman na sio movie yenyewe.

Metadata na ni taarifa kuhusu data zenyewe kabisa (eg file size, structure ya file)

🎁Metadata ndani ya .torrent file pia inabeba tracker addresses.

Trackers ni server inayobeba orodha ya computer zote ambazo tayari zina movie yetu ya Batman.

Computer hizi tunaziita seeders.

Bila shaka mtumiaji wa torrents umeshakutana na huu msamiati wa seeders.

🎁Seeding ni kitendo knachotokea mara baada ya kumaliza kupakua movie yako kupitia torrent client.

Unapofanya seeding unaruhusu watu wengine (Leechers) kupakua vipande vya movie hiyo kutoka kwako.

Nitaelezea mbele kwanini nasema vipande.

🎁Kabla hatujafika mbali ieleweke kwamba kutumia torrents ni kinyume cha sheria, na baadhi ya nchi kama Germany wana sheria kali kupinga torrents.

Ukiwa Germany na PC yako ikagundulika inafanya torrent seeding, utawekwa chini ya ulinzi wa polisi mara moja.

🎁Sasa unapofungua ile .torrent file kwa torrent client, ile client ya uTorrent kwanza itafanya connection na trackers zote ili kuunganika na computer zenye hilo file unapakua.

Baada ya hapo uTorrent itapakua file hiyo moja kwa moja kutoka kwenye hizo PC (seeders) kuja kwako.

🎁Seeders wataendelea kufanya upload ya file, endapo tu torrent client (uTorrent) yake inafanya kazi.

Akizima uTorrent yake, utaendelea kupakua kutoka kwa wengine.

Zoezi hili litashindika iwapo hakuna seeder hata mmoja wa hiyo file.

🎁Unapopakua torrent file, wewe unaitwa "Leecher".

Huu mtandao wa Seeders & Leechers unaitwa Torrent Swarm.

Unapofanya leeching haupakui file lote kutoka kwa seeder mmoja. File inakuwa katika vipande ndani ya PC tofauti tofauti.

Hivyo wewe unapakua kipande kwa kila seeder.

🎁Baada ya kumaliza kupakua hivi vipande ndipo, torrent client yako inachukua jukumu la kuviweka pamoja hivi vipande ili kuunda file zima kama inavyotakiwa.

Kwa kufanya hivi download speed inakuwa kubwa, kwa kuwa unachukua vipande vipande kutoka kwa watu wengi.

🎁 Ukimaliza kupakua file yako, unageuka kuwa seeder. Unaanza upload file ili watu wengine wapakue kutoka kwako.

Sio lazima uwe seeder. Unaweza zima seeding ya file ili kutoendelea tumia bando lako.

Ila huo ni ubinafsi 😁 Wewe umepakua kwetu bure, ila hutaki wenzako wapate.

🎁Nasema hivyo kwa sababu, kadiri seeder wanavyokuwa wengi ndivyo ambavyo download speed inaongezeka.

Kama bando ni ya mawazo, sio mbaya zima tu seeding.

🎁Kwanini Pirates wanatumia torrents kusambaza files zao?

Pirates wengi hawaamini katika taarifa kuuzwa. Hivyo njia sahihi kwao kusambaza files ni torrents.

Lakini sababu kubwa ni kwamba ni ngumu sana kujua huyu pirate ni nani anapotumia torrents.

🎁Mwanzo kabisa huyu pirate ndiye atakuwa seeder wa kwanza na seeder pekee ambaye anafanya seeding ya hilo file.

Leechers watakuwepo wengi na kufanikiwa kuanza fanya seeding ndivyo idadi ya seeders inaongezeka.

🎁Seeders kuwa wengi tunapoteza ushahidi wa centralized source ya ile file yetu.

Kwa maana hiyo mamlaka husika watashindwa kujua msambazaji wa hiyo file ni nani.

Seeders tukiwa wengi mtu wa kwanza kufanya seeding anaweza kujitoa katika orodha ya seeders.

🎁Niibe msemo wa @NNgailo "Biashara sio utapeli, ila kuna matapeli katika biashara".

Ninachotaka kusema ni kwamba, torrents hazina shida na ni njia nzuri kufanya file sharing.

Shida ni kuna baadhi ya watu wanaotumia torrent vibaya.

@NNgailo 🎁Sijasema nakubaliana na piracy. Mimi mwenyewe sipendi kuona content zangu zinatumika bila ruhusa yangu.

Ila hatuna maisha ya kulipia $300 kununua genuine windows au kununua FIFA kila mara inapotoka mpya.

Bila kusahau kwenda kulipia Netflix na Spotify kila mwezi 😒

@NNgailo 🎁Ugumu wa maisha ndiyo unafanya tutumia torrents kupata pirated contents.

Muhimu ni kuwa makini na files unazopakua kwenye torrents. Kuna nyingine zinakuja na virusi vinavyoruhusu wadukuzi kuwa na control ya PC yako.

@NNgailo 🚀Habaritech Magazine Startup edition inapatikana katika @mPaperApp kupitia link hii bit.ly/3vDWwtE pamoja na Gumroad kupitia link hii habaritech.gumroad.com/l/habaritech5

@NNgailo @mPaperApp Uzi unaanza hapa.

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling