Martin Maranja Masese Profile picture
MMM | Full-time Father | Public-spirited | Sperm That Won The Race, ME | Think Deep Don’t sink | Cogito, ergo sum |

May 31, 2022, 10 tweets

Mwaka 2013 Club Billicanas ilifunguliwa baada ya ukarabati wa gharama kufanyika. Ilikuwa ni uwezo wako wa kunywa/kula siku hiyo. Freeman Mbowe alilipa bili zote. 2015 anaingia mwendazake madarakani, anaanza vibweka, 2017 BILLZ inavunjwa kwa unyama. Mwendazake alikuwa katili sana.

Picha ya kwanza Club BILLZ ikiwa na uhai wake. Show kubwa za wasanii wa ‘bongo fleva’ zilifanyika hapo. Frame ya pili ni baada ya Club Billicanas kubomolewa kwa hila tu, sababu nyingi zikiwa za kisiasa. Watu wengi wakakosa ajira. Eneo hilo sasa ni parking tu ya magari. Roho mbaya

Mbowe Hotels ambao walikuwa wapangaji wa muda mrefu kwenye jengo hilo ambapo mbali ya kuendesha Club Bilicanas pia kulikuwa na ofisi za gazeti la Tanzania Daima. Mwendazake alibomoa na hakujali mali na samani zilizokuwa ndani. Ilikuwa ni mbaya sana. Uharibifu ulikuwa mkubwa.

Watu wakajiokotea mali na vitu vingi, ilikuwa ni kubeba unavyoweza na kutokomea na NHC wakatangaza mbada wa mali zilizokamatwa kwamba Mbowe alikwepa kodi ya Shs. 1.2 bilioni kwa miaka 20, jengo la NHC makutano ya mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi, katikati ya jiji Dar es Salaam

Magari yalishuhudiwa yakisomba mali mbalimbali ambapo mmoja wa maafisa wa NHC ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema wanachukua mali ambazo zinaweza kupigwa mnada tu. Lakini mali nyingi hazikuwahi kuonekana tena hata katika mnada Julai 6, 2019. Ulifanyika wizi wa mali tu.

Vyombo hivyo vilikamatwa na kampuni ‘HEWA’ ya udalali ya Fosters Auctioneers & General Traders iliyopewa kazi ya kuondoa vifaa hivyo baada ya Freeman Mbowe kudaiwa kushindwa kulipa deni hilo ndani ya miezi 2 ya notisi ambayo shirika hilo lilikuwa limempatia. Ukatili wa mwendazake

6 Jul 2019, Dalali wa mahakama Joshua Mwaituka, kwenye ghala la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo maeneo ya Bandari alivitaja vifaa vilivyonunuliwa ikiwa ni pamoja na taa, jukwaa, viti, kreti za bia, jenereta, Mashine za kupozea na samani mbalimbali kasoro makochi.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC wakati huo, Nehemia Mchechu alisema pamoja na Bilicanas, shirika linazidai taasisi za umma, binafsi na watu binafsi jumla ya Sh. bilioni 15 akasisitiza Notisi ya siku 60 ya kuondoka Bilicanas pamoja na majengo ya wadaiwa wengine ilishatolewa.

Mchechu alisema ukusanyaji wa madeni hayo kwa nguvu ni mkakati wa shirika hilo kukusanya fedha ili kusaidia ujenzi wa nyumba za watumishi wanaohamia Dodoma. “Mwaka huu ujenzi unaanza Dodoma,” alisema Mchechu, hivyo “fedha tunazodai zitatusaidia kukamilisha uwekezaji mjini humo.”

Mungu siyo Athumani, 16 Dec 2017 — Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akaagiza kusimamishwa kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu na June 21, 2018 uteuzi wake ukatenguliwa.

Ingawa sasa karejeshwa kulamba asali.

#MMM

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling