Martin Maranja Masese Profile picture
May 31, 2022 10 tweets 7 min read Read on X
Mwaka 2013 Club Billicanas ilifunguliwa baada ya ukarabati wa gharama kufanyika. Ilikuwa ni uwezo wako wa kunywa/kula siku hiyo. Freeman Mbowe alilipa bili zote. 2015 anaingia mwendazake madarakani, anaanza vibweka, 2017 BILLZ inavunjwa kwa unyama. Mwendazake alikuwa katili sana.
Picha ya kwanza Club BILLZ ikiwa na uhai wake. Show kubwa za wasanii wa ‘bongo fleva’ zilifanyika hapo. Frame ya pili ni baada ya Club Billicanas kubomolewa kwa hila tu, sababu nyingi zikiwa za kisiasa. Watu wengi wakakosa ajira. Eneo hilo sasa ni parking tu ya magari. Roho mbaya
Mbowe Hotels ambao walikuwa wapangaji wa muda mrefu kwenye jengo hilo ambapo mbali ya kuendesha Club Bilicanas pia kulikuwa na ofisi za gazeti la Tanzania Daima. Mwendazake alibomoa na hakujali mali na samani zilizokuwa ndani. Ilikuwa ni mbaya sana. Uharibifu ulikuwa mkubwa.
Watu wakajiokotea mali na vitu vingi, ilikuwa ni kubeba unavyoweza na kutokomea na NHC wakatangaza mbada wa mali zilizokamatwa kwamba Mbowe alikwepa kodi ya Shs. 1.2 bilioni kwa miaka 20, jengo la NHC makutano ya mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi, katikati ya jiji Dar es Salaam
Magari yalishuhudiwa yakisomba mali mbalimbali ambapo mmoja wa maafisa wa NHC ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema wanachukua mali ambazo zinaweza kupigwa mnada tu. Lakini mali nyingi hazikuwahi kuonekana tena hata katika mnada Julai 6, 2019. Ulifanyika wizi wa mali tu.
Vyombo hivyo vilikamatwa na kampuni ‘HEWA’ ya udalali ya Fosters Auctioneers & General Traders iliyopewa kazi ya kuondoa vifaa hivyo baada ya Freeman Mbowe kudaiwa kushindwa kulipa deni hilo ndani ya miezi 2 ya notisi ambayo shirika hilo lilikuwa limempatia. Ukatili wa mwendazake
6 Jul 2019, Dalali wa mahakama Joshua Mwaituka, kwenye ghala la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo maeneo ya Bandari alivitaja vifaa vilivyonunuliwa ikiwa ni pamoja na taa, jukwaa, viti, kreti za bia, jenereta, Mashine za kupozea na samani mbalimbali kasoro makochi.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC wakati huo, Nehemia Mchechu alisema pamoja na Bilicanas, shirika linazidai taasisi za umma, binafsi na watu binafsi jumla ya Sh. bilioni 15 akasisitiza Notisi ya siku 60 ya kuondoka Bilicanas pamoja na majengo ya wadaiwa wengine ilishatolewa.
Mchechu alisema ukusanyaji wa madeni hayo kwa nguvu ni mkakati wa shirika hilo kukusanya fedha ili kusaidia ujenzi wa nyumba za watumishi wanaohamia Dodoma. “Mwaka huu ujenzi unaanza Dodoma,” alisema Mchechu, hivyo “fedha tunazodai zitatusaidia kukamilisha uwekezaji mjini humo.”
Mungu siyo Athumani, 16 Dec 2017 — Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akaagiza kusimamishwa kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu na June 21, 2018 uteuzi wake ukatenguliwa.

Ingawa sasa karejeshwa kulamba asali.

#MMM

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Martin Maranja Masese

Martin Maranja Masese Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @IAMartin_

Aug 8, 2023
“Martin Maranja Masese’s open letter to Samia Suluhu Hassan”

Dear madam president, HE. Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania

As-salamu alaykum! Image
Madam President, I am honored to be writing to you about issues that are important to our country’s interests. Writing to you directly instead of starting with your assistants may seem unfair since the President is an institution. But, I decided to write to you straight away.
Today, again, I come to you with great humility, but not diffidence, as an ordinary citizen of this beloved land. I will try to use my very vertical percipience, prudence and sagacity to try speak out, and I hope you will hand-pick these writings in a very positive way.
Read 68 tweets
May 15, 2023
Unaagiza MZIGO wa nguo wa TZS 43,200,000/- unalipa kodi TZS 26,892,000/-.

Mfanyabiashara kurejesha faida yake atapaswa kuuza mzigo bei gani ili alipe kodi na tozo nyingine?

Waziri wa fedha na Mipango, @mwigulunchemba1 lengo lako ni kodi katika kila kitu katika eneo moja? ImageImage
. @TRATanzania wanafanya hivi miaka yote, hapo bado TBS, service levy 0.3% ya mauzo (haijalishi umepata faida) bado gharama ya usafirishaji kutoka bandarini ambayo ina kodi kibao... Yote hii ni uvivu tu wa kufikiri, wanakamua wachache badala ya kuongeza tax base ili kodi zipungue
Hapo bado service levy, kodi ya pango, kodi ya taka, kodi ya Jengo, fire extinguisher, leseni ya biashara, kodi ya mapato, tozo ya mabango, umeme, ulinzi, wafanyakazi, ulinzi stoo, kodi ya stoo, died stock, kibali cha TBS. Mfanyabiashara atapata kweli nguvu za kiume kwa mkewe?
Read 6 tweets
Apr 28, 2023
MSEMAJI wa serikali anasema @Nnauye_Nape na wizara ya Habari wanashawishi Instagram kuleta ofisi Tanzania. Ofisi za Instagram za kazi gani @MsigwaGerson? Tumieni akili ndogo mlizonazo kushawishi Volkswagen, Mercedes-Benz, Ford, Jeep, Hyundai, Honda, BMW, TVS wafanye assembling TZ ImageImage
Mfano, gari zilizoshushwa kutoka katika meli ya mizigo 9 April 2022 katika bandari ya Dar es Salaam, gari 1,105 (sawa na 27%) ya mzigo ulioshushwa bandarini zilibaki Tanzania na gari 2,936 (73%) zilikwenda nchi jirani (Sudan, Zimbabwe, Mozambique, Malawi, Zambia).
Mkurugenzi wa mamlaka ya bandari Tanzania anasema, kuanzia April 5 hadi April 7 (ndani ya siku 3 tu) bandari ya Dar es Salaam ilipokea meli nne zenye jumla ya magari 8,384 (ukilinganisha na mwaka 2021, walikuwa wakipokea gari 10,000 kwa mwezi mmoja).
Read 20 tweets
Mar 17, 2023
"JPM ALICHELEWA KUWA RAIS WETU. NDIYO"

Tulitakiwa kuwa na JPM kabla ya miaka 20 iliyopita. JPM alichelewa kuwa Rais wetu kwa katiba ya kifalme/kisultan tuliyonayo. Miaka 5 na miezi 5 ilituonyesha rangi za udikteta. Ingawa rangi hiyo haikufika kwa mtu mmoja mmoja, wapo walioguswa
Bado tulihitaji kuwa na JPM kwa miaka mingi au tuseme kwa lugha rahisi kabisa, JPM alichelewa kuwa Rais wetu. Ndiyo. Kabla ya JPM, kuna masuala mengi ya hovyo hatukuwahi kuyaona au kupitia katika siasa za nchi yetu, lakini katika uwepo wake tumeona masuala mengi ya kuogofya.
JPM alikuwa daktari bingwa wa propaganda. Aliweza kuwaaminisha watu uchumi wetu ni imara na ukuaji wake ni wa kadi kubwa, watu waliamini ingawa bado walikuwa maskini wa kutupwa, hawana huduma za kijamii katika maeneo yao, hawana miradi ya maendeleo na kipato chao ni duni.
Read 66 tweets
Nov 7, 2022
“Shujaa Mvuvi — Muokoaji”

Majaliwa Jackson (Maja Munyama), mvuvi wa dagaa anasema alipoona ndege imetua ndani ya maji (kutoka upande wa Kyaka) isivyo kawaida, kwa kuwa ilikuwa asubuhi, saa 8:53 EAT, aliwasanua wenzake waliokuwa na mtumbwi mdogo, walipiga kasia hadi kwenye ndege.
Majaliwa anasema alipofika kwenye ndege, alikuta watu wakijadili jinsi ya kuingia ndani kutoa msaada, lakini mlango umejifunga (locked). Majaliwa akatumia kasia yake, akapiga, mlango ukafunguka, watu wakaanza kuokolewa kupitia mlango huo. Majaliwa akahamia upande wa rubani.
Majaliwa akazama hadi kwa rubani, captain Baruhani Rubaga akaonyesha ishara, abomoe kioo, akafuata shoka, walinzi wakampa, sauti ya mamlaka kutoka katika kipaza sauti, kikamzuia, asithubutu. Kwanini? kwamba rubani wanawasiliana kwenye simu zao, yupo salama, maji hayajafika kwake.
Read 6 tweets
Oct 10, 2022
“Letter to the president of the United Republic of Tanzania”

Dear madam president, HE. @SuluhuSamia

How are you doing? Image
These are my quarterly (4th quarter, 1 October–31 December (92 days) greetings to U & yours as well. We prayed 2022 to be a better year for all of us, the year in which we (would) refined ourselves, because it was another year of struggle for existence as always. Let’s talk now!
Today, again, I come to you with great humility, but not diffidence, as an ordinary citizen of this beloved land. I will try to use my very vertical percipience, prudence and sagacity to try speak out, and I hope you will hand-pick these writings in a very positive way.
Read 61 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(