Madinidotcom Profile picture
Show ya radio kwa #TAARIFANaMAARIFA kila wiki.Tunajadili ya dunia kwa lugha rafiki na nyepesi. kila Jumamosi 9alasiri - 10jioni Eastafrica Radio..Subscribe👇

Jun 23, 2022, 23 tweets

UMESIKIA MENGI KUHUSU MGOGORO WA #RWANDA NA #DRC LAKINI PENGINE UNASHINDWA KUELEWA WTF IZ GOING ON?🧐🤭
Kuna njia mbili za kuelewa,ya kwanza ni usome Uzi ufuatao.
Pili usikose show'Jmosi hii eastafricaradio.com
History iliyorahisishwa na #SabulaMaarifa wa #MadiniDigital.

Iko hivi!! Kitambo hicho Rwanda iliwahi ku-operate chini ya mwamvuli wa KIFALME uliokuwa ukiongozwa na mwamba wa kuitwa KIGELI IV RWABUGIRI.
Rwabugiri alikuwa ni jamaa fulani hivi kutokea Kabila la walio wachache (TUTSI) kule Rwanda.

na aliingia kwenye vitabu vya kihistoria kama kiongozi pekee wa taifa hilo aliyeamua kufanya mashirikiano na Serikali za KIKOLONI. By the way kama tunavyojua kuwa RWANDA kuna Makabila makuu mawili, na la 3 ni nyongeza, kuna walio wengi ambao tunawatambua kama Wa-HUTU

na walio wachache ambao ni TUTSI lakini kabila la 3 ni TWA ambao kihistoria ndio wa kwanza kuja Rwanda.Wahutu na Watutsi waliwakuta pale ila ni wachache na shughuli zao za kijamii haziwapi kiki sana.

Sasa huyu RWABUGIRI alikuwa kutokea upande huu wa jamii ya walio wachache ambao Wa-TUTSI (anapotokea Kagame)
RWABUGIRI aliongoza kwa muda mrefu na baadae alifariki lakini misingi yake iliendelea kuishi.Sasa ujue issue ya kushirikiana na MABEBERU,

haikuwapendezea kabisa jamaa zetu wa KI-HUTU na mara kadhaa walishakinukisha kujaribu kuuondosha madarakani UTAWALA wa KIFALME bila mafanikio.
Ujue walichokuwa wakifanya WAKOLONI kule Rwanda ni kwamba waliacha milango wazi kwa MACHIFU wote kuja na kufanya nao mashirikiano.

Wa-HUTU wao jambo hili lilionekana kupingwa vikali kwakuwa waliamini walikuwa na uwezo wa kujitawala wenyewe.
RWABUGIRI ambaye alikuwa akiongoza jamii ya walio wachache aliona ni fursa kuamua kutembea na HASHTAG ya JK 🇹🇿 kwamba 'Ukitaka kula lazima na wewe uliwe kidogo' 🥳

Kwa namna fulani mgogoro baina ya jamii hizi mbili Wa-HUTU & Wa-TUTSI ni kama ulianziaga hapa .Hii dillema ya machaguo ya kijamii wakati wa uhuru iliwapata pia NIGERIA tulikuletea saga la BIAFRA.
So Wa-HUTU walianzisha struggle za kuhakikisha wanauondoa UTAWALA wa KIFALME.

Mapinduzi yale yalifanya jamii kubwa ya Wa-TUTSI kuikimbia nchi na kwenda kutafuta hifadhi kwenye mataifa jirani kama Uganda,Congo na Tanzania ikiwemo.

Sasa wakiwa huko bhn Wa TUTSI hawakulaza damu,wakaanza kujipanga kwa kutoa mafunzo ya kijeshi kwa vijana wao...

LENGO KUU likiwa ni kuona siku moja wanarejesha UTAWALA wao ndani ya Rwanda 🇷🇼
Hapo katikati (Toka Mapinduzi ya mwaka 1960) kulifanywa majaribio kadhaa ya kupindua nchi by Wa-TUTSI ambayo yalifeli.
Ni katika kipindi hichi ndipo neno COCKROACHES (Mende) nchini Rwanda.

Wa-HUTU walitumia neno hili kuyaelezea makundi mbalimbali ya Wa-TUTSI yaliyokuwa yakijaribu kupindua Nchi. baadaye lilitumika kwenye Media wakati wa mauaji.
Mfululizo wa majaribio haya ya ki-mapinduzi yaliyokuwa yakifanywa na vikundi vya Wa-TUTSI uliendelea bila mafanikio.

Then ukafika mwaka 1990 Paul Kagame akiwa na kikundi Chake cha waasi Rwanda Patriotic Front (RPF) wakafanya Uvamizi wa NGUVU ulioitikisa Serikali.KIKAUMANA HASWA!
Wakati huu jamaa walikuja na nguvu kiasi cha kufanikiwa kushikilia baadhi ya miji na kushikilia mateka wa kivita

Kitendo cha kikundi kufikia kushikilia wapiganaji wa serikali,you can see walikua walikuwa zaidi ya kundi la waasi.Ikamlazimu Rais Juvenal Habyarimana kukubali kurudi mezani kwa mazungumzo.
Eneo la mazungumzo likawa ni CHUGANISTAN kwa Machalii wa R (Arusha-Tanzania)

na haikushangaza kuona trip za Kigali to Tanzania kwa Rais Habyarimana pamoja na delegation yake zikiongezeka maradufu kwa wakati huo
Huku mazungumzo baina ya Upinzani ambao ni ulikuwa ni Rwanda Patriotic Front (RPF) na Serikali ya Rwanda yakionekana kwenda vizuri kule ARUSHA.

Ghafla #PichaLinaanza taarifa zikaja, ndege ya Rais Habyarimana imetunguliwa ilipokuwa ikijaribu kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kigali(Rwanda) na kuuwa watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo akiwemo rais wa Burundi ambaye aliomba Lift! ukawa ukaribisho wa RWANDA GENOCIDE!!

Jamii ya Wa-HUTU ililihusisha tukio hili la kutunguliwa kwa ndege ya wao Habyarimana na jamii za Wa-TUTSI so KIKAUMANA.
Yakafanyika mauaji dhidi ya jamii ya walio wachache (TUTSI) lakini hatimaye RPF chini ya Rais Paul Kagame wakafanikiwa kuyatwaa madaraka na kukomesha yote.

Utakumbuka tulikuletea Deep kuanzia hapa na kuendelea kwenye episodes zetu kuhusu visa na mikasa ya tukio hili.
AND THAT WAS THE BEGINNING OF THE NEW TUTSI SUPREMACY IN RWANDA.
Upande wa pili baadaye wengi ilibidi waikimbie nchi na kwenda nchi jirani ya CONGO.

Huko walikwenda kufanya makazi katika miji mbalimbali iliyopo Mashariki mwa nchi hiyo 🇨🇩Sasa wakiwa huko bhn ni kama nao wanaonekana kuendelea na mipango ya chini kwa chini ya kuona namna siku moja watarejesha tena UTAWALA wao ndani ya taifa la RWANDA 🇷🇼

Wanachofanya RPF (RWANDA) ni kuzuia uwezekano wa hawa jamaa kujipanga upya na kufanya kile walikifanya wao 1994 .Ukumbuke hadi leo kuna vikundi na watu binafsi wengi wanaopambana kumng'oa rais Kagame,na yeye ameshasema na kuonyesha mipango yake ya kupambana nao MAADUI WA TAIFA.

#Taarifa ya hivi majuzi iliyotolewa na Serikali ya Kongo imeonyesha kuishutumu moja kwa moja Serikali ya Rwanda kwamba inasapoti kikundi cha UASI cha M23 .Ni kwasababu kuna story ya MASLAHI ya jamii za wanyarwanda ndani ya DRC na maeneo hayo ambayo yana utajiri mkubwa

Jambo ambalo pengine utakuwa hulifahamu ni kuwa hawa wa M23 ni aina ya Wa-TUTSI wapatikanao CONGO ingawa kwa kule huwa wanaitwa BANYAMULENGE kwasababu ni jina(bandia)walilolitumia wakati wanaoung'oa utawala wa MOBUTU SESE SEKO wakisaidiana na LAURENT KABILA.

Usaidizi huu wa BANYAMULENGE wa MCHONGO yalikua makubaliano ya SIRI kati ya LAURENT KABILA na WANYARWANDA hao wakimbizi wakati huo,na unafahamika kama MAKUBALIANO ya Lemera ya mwaka I996.
Mkataba huu wa siri ...

Tunaujadili kiundani na YERICO NYERERE,mwandishi wa kitabu cha UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI.Ukitufuatilia utagundua unaunganisha doti nyingi za matukio ya dunia kwa lugha ya kishkaji.Usikose Eastafricaradio kila jumamosi saa 9alasiri hadi 10jioni .

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling