Kuduishe Kisowile Profile picture
MD | WHO Fides Influencer | P1L1 | Health Communications Consultant | #MeToo | Op-Ed Writer at TheChanzo | #KuduAfyaTips | #DaktariMwandishi 🇹🇿 #RadFem

Sep 26, 2022, 16 tweets

Kuna safari hata ziwe fupi vipi, hazisahauliki. Hazisahauliki kwa mengi; watu uliosafiri nao, watu uliokutana nao, experience ya safari na mengine mengi.
Mimi safari hii pichani sitaisahau.
Nilipata wasaa wa kushare na @buguzi @NormanJonasMD @DrArabiFrank na @JuliethSebbaMD #UZI

Ilianza kama utani hivi, nikafahamishwa nimepata nafasi ya kufanya mafunzo Morogoro ambayo yaliandaliwa na @sikika1 na @tacaidsinfo
Na mimi mpenda safari na mpenda afya, naanzaje kukosa? Nikafungasha kibegi changu uelekeo mji kasoro bahari.
Moro bwana! Moro PAZURI NYIE! Basi tu.

Katika mengi nilojifunza siku hizo mbili, kuna kitu kimoja kilichonivutia zaidi ya mandhari nzuri ya Morogoro, maana mara ya mwisho nilikuwa hapa ilikuwa ni trip ya Udzungwa na Mto Mawe.
Kitu hicho ni Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI Tanzania (ATF). Leo naomba niwashirikishe

Ulianzishwa Machi, 2015.
Lengo ni kuongeza mchango wa serikali na taasisi/sekta binafsi katika kutatua changamoto za raslimali zilizopo kwenye utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI hapa nchini.
Ifahamike kwamba, programu ya kitaifa ya VVU imekuwa ikitegemea sana fedha za wafadhili

Wafadhili wakuu ni pamoja na Serikali ya Marekani @PEPFAR , Mfuko wa Dunia @GlobalFund , ambao kwa pamoja wanachangia 93% ya fedha zote zinazopatikana kwa mapambano wa VVU nchini Tanzania.
Kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sera ya kujitegemea, kuna haja ya kuwa na vyanzo vya

ndani vya ziada ili kudhamini afua mbalimbali za VVU na UKIMWI nchini.
ATF imeanzishwa kwa lengo hilo. Kuziba pengo la ufadhili kwenye shughuli za utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI.
Fedha za mfuko hupatikana kutoka Serikali kuu pamoja na Harambee, michango ya simu n.k
Lengo

likiwa ni kuhakikisha mfuko wa ATF unaweza kuziba myanya katika utekelezaji wa afua za UKIMWI.
Fedha zilizokusanywa 2016-2020 zimetumika katika;
1. Bilioni 1.110 zilipelekwa @wizara_afyatz kwa ajili ya kununua dawa za magonjwa nyamelezi kwa Watu wanaoishi na VVU (WAVIU).

2. Shilingi Mil 250 zimetumika kujenga kituo cha kisasa cha kutolea huduma za VVU na UKIMWI kwa wachimbaji wa madini wa eneo la Mirerani, wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara, pamoja na wananchi wanaoishi maeneo ya jirani,

3. Shilingi Mil.182 zimetumika katika utekelezaji wa programu za kinga dhidi ya maambukizi ya VVU kwa vijana walio katika taasisi za elimu ya juu zilizopo jijini Dodoma

Hayo ni baadhi ya mafanikio ya mfuko huu pamoja na kuandika maandiko kupitia wataalamu elekezi na wataalamu wa

Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania. Yatako wasaidia Madereva wanaoendesha masafa marefu, Waendesha bodaboda/daladal na wavuvi maeneo mbalimbali nchini jinsi ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI.

Licha ya mafanikio hayo, mfuko bado una changamoto mbalimbali pamoja na:

1. Kutokuwepo kwa chanzo endelevu cha fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wa ATF
2. Mwitikio mdogo wa wadau katika kuchangia fedha kwenye mfuko wa ATF
3. Gharama kubwa za maandalizi ya shughuli za harambee

Vyanzo vinavyopendekezwa ni tozo mbalimbali kutumika kutunisha mfuko huu.

Katika kutekeleza uchangiaji wa mfuko huu, kutakuwa na ATF Marathon @atfmarathon trh 27 Nov, 2022 itakayofanyika viwanja vya Ilulu, LINDI.
Usajili ni TZS 35,000 TU utapata punguzo la TZS 5,000 ukijisajili mapema
Tembelea atfmarathon.co.tz au piga *150*50*1# ingiza 60491370

Sote tuna jukumu la kuchangia maendeleo ya afua za VVU na UKIMWI, na kwa wale wapenzi wa marathon kina @TOTRunners, wapenda mazoezi wote mnakaribishwa kuhudhuria ATF Marathon
Mimi kwa kuwa sitaweza kuhudhuria, nitamlipia follower wangu MMOJA atakayekwenda. Huo ndio mchango wangu

Safari yetu iliisha salama hapo tulisimama kwenye restaurant fulani hivi niliiona ikanivutia somewhere Pwani, naomba boss @buguzi uendelee kuwa dereva wetu katika kuchangia maendeleo ya Afya.

Na safari nyingi zaidi ziendelee, zituzungushe viunga vyote vya nchi hii katika kutimiza maendeleo na kuchangia huduma za afya nchini.
Naomba @buguzi @DrArabiFrank @JuliethSebbaMD na @NormanJonasMD mseme AMINA kubwa sana.
Basi #NovembaTukutaneLindi @atfmarathon #DaktariMwandishi

@threadreaderapp please unroll

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling