UKUAJI ni hali ya kuongezeka kwa ukubwa(size) ya mwili wa mtoto
Maendeleo ni hali ya mtoto kuweza kufanya jambo fulani kwa wakati fulani unaotarajiwa.
Mfano kutoka kutambaa hadi kutembea.
#afyakwawote.
Ukuaji na maendeleo ya mtoto huenda sambamba ila kwa kasi tofauti tofauti.
#afyakwawote.
ukuaji wa mtoto unaweza gawanywa katika makundi makuu mawili ambayo ni
1. Baada ya mimba kutungwa (pre natal)
2. Baada ya mtoto kuzaliwa (post natal)
#afyakwawote.
Baada ya miezi mitatu ya mimba kutungwa ogani mbali mbali kama ubongo, figo, mapafu moyo na nyinginezo huanza kutengenezwa.
#afyakwawote
Mazingira haya ni kama Uvutaji wa sigara, mionzi (x rays) baadhi ya dawa na virus.
#afyakwawote
Lishe duni, upungufu wa damu na malaria huathiri ukuaji wa mtoto katika kipindi hicho na mtoto huzaliwa na uzito mdogo au kudumaa akiwa angali tumboni kwa mama.
#afyakwawote.
Hapa tunaweza kugawa kipindi hiki katika hatua nyingine ndogo tatu ambazo ni
1. Mtoto mchanga
2. Mtoto
3. Balehe.
#Afyakwawote
Kipindi hiki hutegemea sana hali ya lishe anayopata mtoto.
Katika miezi hii mtoto anatakiwa kupewa maziwa ya mama tu na si vinginevyo.
#afyakwawote.
Kipindi hiki hutegemea sana vichocheo vya ukuaji katika mwili.
#afyakwawote
Kwa wasichana huanza balehe Kati ya miaka 8_13 na kwa wavulana ni Kati ya 9_14.
#AfyaKwaWote
1. UZITO.
Baada ya mtoto kuzaliwa uzito wake hupungua kwa asilimia Kati ya 5% hadi 10% ndani ya wiki 2.
#afyakwawote.
Kisha uzito huongezeka mara mbili yake ndani ya miezi 6, huongezeka tena mara 3 ndani ya miezi 9_12, huongezeka mara 4 ndani ya miaka miwili na baada ya hapo huongezeka kwa kilo 2 kila,mwaka.
#AfyaKwaWote
Urefu wakati wa kuzaliwa huwa ni 50cm kwa wastani, Kisha 75cm baada ya mwaka mmoja na hufikia 100 cm baada ya miaka 5.
#afyakwawote
Huu huongezeka kwa kasi hadi kufikia 15 cm na kisha kuongezeka taratibu taratibu kadri muda unavozidi kwenda.
#afyakwawote.
1. Genetics /urithi. Wazazi wenye vimo vifupi huzaa watoto wenye vimo vifupi, hivyo hivyo kwa wazazi warefu.
#afyakwawote.
3. Vichocheo vya ukuaji
4. Magonjwa. Magonjwa wakati wa utoto hupelekea mtoto kupungua uzito na kudumaa pia.
#afyakwawote.
Maendeleo ya mtoto ni jumla ya shughuli zote( kijamii, kitabia na kimatendo) anazoweza kufanya mtoto kutokana na umri alionao.
Hatua hizi huitwa developmental milestones na hugawanywa kwa miezi.
#AfyaKwaWote
KIJAMII
1.Huanza kutabasamu anapowaona watu au unapocheza nae. Hasa watu wa karibu anaokaa nao kila siku.
2. Anaweza kujituliza mwenyewe kwa kuleta mkono wake mdomoni na kuunyonya.
3.Anaweza kuanza kutazama wazazi au mlezi wake.
#afyakwawote .
Anaweza kumfuata mtu kwa kugeuza kichwa
Kwa kiasi kidogo anaweza kukaza shingo, pale anapoinuliwa kwa mikono.
#afyakwawote.
Huanza kutoa sauti ndogo ndogo kama anacheka (cooing and gurgling)
Anaweza kugeuza kichwa kuelekea upande sauti inapotoka.
#afyakwawote.
Anaweza kuanza kutambua uso. Atapendelea zaidi nyuso za watu aliowazoea.
Anaanza kufuata vitu kwa macho. Anaweza akapendelea kutazama upande wenye televisheni au vitu vingine.
Atalia iwapo hajisikii vizuri au hafurahii kitu kinachofanyika. #afyakwawote.
Hucheka mara kwa mara, huanza kuiga maneno anayosikia, huanza kuvifata vitu kwa mkono mmoja, huanza kupelekea mikono kinywani na huanza kumtambua mama.
#AfyaKwaWote
Huweza kutambua sura ngeni na aliowazoea.
Huanza kuonyesha muitikio akiitwa jina lake.
Huweza kukaa bila msaada.
Huanza kuvifata vitu vilivyo mbali
#AfyaKwaWote
Huanza kutamka neno kama mamamaaaaa.
Hutambaa na kuanza kusimama bila msaada.
Hutumii kidole kuonyesha vitu.
#AfyaKwaWote
1.Lishe
2.Msaada wa kihisia. Ili mtoto aendelee vizuri lazima ahisi anapendwa na wazazi na jamii inayomzunguka, ajihisi yupo salama wakati wote, ajihisi yupo huru, ajihisi anathaminiwa na anakubalika kama mtu.
#afyakwawote.