My Authors
Read all threads
I WAS A REASON FOR SOMEONE'S SMILE ❤

Uzuri wa maisha siku zote ni kuishi kama vile ulikua na chaguo lakuamua unavotaka kuishi Furaha ni maana halisi ya kuishi
Inaleta faraja ukifurahi na inafurahisha zaidi ukiona mwenzako anafuraha na wewe ndo chanzo cha furaha
T H R E A D👇🏼
Kupitia story hii utaweza kujifunza maana halisi ya kupenda na kutamani😄.
Ilikua mida ya likizo baada ya masomo mengi ya semester ile nikawa nyumbani tuu nimechill coz ilikua likizo fupi ya wiki mbili sikuona haja ya kuumiza kichwa kutafuta mishe nkaona niupe mwili pole tuu
Mara nyingi nakua home nasoma novels,writing some of my stupid articles 😁and other stuffs lakini ikifika jioni lazima ntaenda kwa rafiki yangu Alvin.
Huyu tumetoka nae mbali sana anasoma chuo kimoja hapo Dar so mara nyingi tupo wote.
Kwa bahati mbaya hana uwezo wa kuona (kipofu)
Lakini kachangamka sana,ana nguvu mcheshi shabiki wa Simba na Man U😂. Kiufupi tofauti yangu na yeye ni kwamba tuu mimi nauwezo wa kuona yeye hana na ana aibu ila vingine vyote tunaringana maana ashawahi mpaka kunizibua enzi za utoto🤣
So, ntakua kwao tunapiga story nyingi
Za mpira,movies,mademu na vitu kama ivo vijana sisi asee😁.
So siku moja nikiwa kwao nkaona simu yangu inaita anapiga binti mmoja anaitwa Isabella.Huyu yupo natural sana mzuri weusi wa kung'aa na macho ya mviringo kama round about ya Msamvu 😂.
Aliahidi kuja kuntembelea
Na kweli ilivofika saa 16:30 akatimiza ahadi yake ya kuja so nkaona sio mbaya nikampokee.Nikamshika mkono mwanangu Alvin tukaenda ila tuu nkamuonya asiharibu kazi maana alishawahi kuomba namba binamu yangu 😂
So tukafika baada ya salamu tukaenda home kutulia na story zikafata
Nkawa nimetoka kidogo kufata soda za wageni ile narudi nakuta Alvin na Isabella story zimekolea binti wa watu anacheka sana kwa ucheshi wa jamaa yangu huyu 😀

So ikafika kama 18;00 binti anataka awahi kwao maana ni kafikia kwa ndugu itakua jau akichelewa.
Tukamsindikiza mpaka
Kituo cha daladala za kuelekea mitaa ya Kilakala huko ndo kafikia.Sasa ile tunarudi yakatokea niliyoyategemea bhana maana Alvin akaanza mambo yake 😁
" Oya skia mzee ile perfume ya yule dada nlihisi nipo ndani ya bustani ya maua tupu,vile ulifata soda nlitamani hata usiwahi kuja
Nkajua kadata huyu 😂..Kwa sababu haoni (he is blind 💔 ) akaomba nimpe maelezo binti anafananaje ili atathmini viwango legend.
Sikumficha nkampa A-Z ya muonekano wa Isabella na nikamwambia ni rafiki tuu anasoma chuo kimoja pale Mbeya.Basi jamaa akanambia nimtengenezee njia 😂
Sikua na noma,nkamuahidi lazima ntatimiza. Kesho yake nimetulia nkaona Alvin ananipigia simu na Nokia yake ya Tochi 😂anasema " We fala kama unampenda yule manzi siuseme sio tunabaniana mpaka mapito haya halafu mi nataka nimuoe yule mwisho wa siku 😒" duh nkaomba radhi maana
Nlijisahau tuu. Hapo hapo nkaanza kumchokoza Isabella
"Hey Isabella mambo,leo nataka tuongee mahaba leo 😁" by the way she is my friend Veery friend.Akacheka sana akasema " We Noh wewe hayo mapenzi vp wakati najua unatoka na binti yuko Shanghai China 😏" alitania tuu nkacheka
Baada ya story kidogo nkamchomekea " So Isabella unapenda mume wa aina gani au mume aliye na sifa zipi " akatabamasamu kwenye simu ile akasema " awe na urefu wa kawaida tuu,kajazia design ya 6 packs,rangi yoyote 🤗" nkasema oouh kumbe nkaanza kuwaza daah sasa..
Alvin msela wangu lazima ashinde hii mechi nkasema " Isabella bana ni vizuri kuwa na mwanaume wa ndoto zako lakini isikufunge kupata mwanaume atakaekupa furaha na kukupa maana ya kuishi"
Akaniuliza " Noel una maana gani kwa kusema ivo " nkaendelea
"..Unajua ipo ivi,katika yote
Uliyotaja ni mazuri lakini unaweza ukampata jamaa wa aina na sifa hizo lakini katika kuishi akaanza kupoteza sifa moja baada ya nyingine mfano, izo six packs ni matokeo ya kwenda gym na kufanya mazoezi so unaeza mpata mwenye nazo lakini mwisho akazipoteza kutoka na umri kwenda
Na pia majukumu kumbana akaacha zoezi zikatoweka, unaweza kumpenda mwanaume kisa miguu mizuri lakini mwisho wa siku umempata akapata ajali bahati mbaya akakatwa miguu je utamuacha kwa sababu hana tena ile miguu uliyompemdea??😄

Hapo akaanza kujichekesha bila hoja nkasema
"Bhana we ni mshikaji wangu nakuzimia kishenzi na siezi kukuacha utumbukie kwenye shimo wakati naona njia nzuri kiufupi kuna rafiki yangu kakupenda ile sana😀"

Akacheka sana anafikri masikhara akasema "Kwaio Noh leo unaamua kuniuza rafiki yako " nkasema " hapana mi sikuuzi
Nipo hapa kama daraja la kukupeleka njia nzuri" akasema nimtumie picha ya huyo mtu ikabidi nipekue picha ya Alvin nkatuma huku naomba Mungu mambo ya ende sawa maana Alvin kweli alikua analengo afunge ndoa na hapo baadae.
Ile picha alivoiona akapiga yeye simu
"Noel huyu si yule alikuepo jana " nkasema " yeah ndo yule anaitwa Alvin " akashusha pumzi akaendelela"..Noel sikuwahi kuwaza kumpenda mtu asiyeona,kipofu nadhani mtafutie mtu mwingine sio mimi " akakata simu 💔
Dah wazee nilijiskia vibaya mno maana ntafikishaje taarifa mbaya iv
Kesho yake nkatulia tuu..Saa tatu asubuhi naona Alvin anapiga simu sikupokea maana nilikua bado sina cha kusema.Hata sijakaa sawa naskia mtu keshaingia anapiga kelele nyumba nzima anaparamia vitu 😂😂
Uzuri walishamzoea pale home.Jamaa akaingia mpaka room nkajifanya nimelala
Fujo zilivozidi nkaamka nkamwambia demu anaeleweka kasema nsubiri atanipa jibu kesho..Basi nkaona Alvin anafurahi sana lakini moyoni naumia mno nkimuangalia 💔
Jioni nkampigia Isabella nkamuambia maneno meengi sana but "ujafa hujaumbika " ilikua maneno nlotamka zaidi nkaona
Anaelekea akasema kesho nije na Alvin tukutane mahali..Aisee nilijikuta naruka ruka mule ndani kama nimeshinda Tatu mzuka🤣
Nkampa taarifa msela akaandaa pamba zake kesho ikafika tukakutana Coco beach restaurant pale story zikaanza sasa bhana huyu Alvin sio fala
Akaanza kuvimba anaita muhudumu mara anatuagizia mazaga pale alichangamka sana😂
Story zikaanza Alvin anamwaga sera zile swaga nlihisi kuna mahali anasoma yule jamaa🙌🏼
Isabella anang'ata kucha mbele ya legend mwisho akasema atatuma jibu kwa meseji nikauliza " utatuma jibu kwangu
Au kwa Alvin " Jamaa alivoskia ivo alinifinya mpaka leo nipo na alama kwenye paja😂..Kesho yake Isabella akampigia Simu Alvin akamwambia amekubali kuwa wake.
Jamaa alikuja home speed kuleta majibu anaruka sana tukaenda zetu kupata moja baridi moja moto 🍺
By the way mpaka sasa
Wako pamoja Alvin na shemji yangu Isabella na mpango wa kuoana upo maana jamaa kila siku analeta habari za kushona vitenge😂❤
#End
#MyMindSpeak
#NohTalk ☕️
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Noe_Wenc 💊

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!