My Authors
Read all threads
#FahamuNaFesto: Je unalifahamu kundi lako la damu (blood group)? Ni moja ya maswali mengi sana ambayo wengi wetu tunajiuliza. Wengi tunaenda mbele zaidi kutaka kujua Je kwa kundi ulilonalo unaweza kumpa damu mwenye kundi gani. Basi leo nakujibu maswali yote haya.
Katika sayansi ya makundi ya damu kwanza tutaanza na mifumo ya ugunduzi wa makundi ya damu. Mpaka julai mwaka jana tafiti zinaonesha kuna takribani mifumo 39 ya damu. Nikukumbushe tu kuna mfumo wa ugunduzi wa kundi la damu na kuna kundi la damu hivi ni vitu viwili tofauti.
Mfumo wa ugunduzi wa makundi ya damu ni njia tofauti ambazo wanasayansi walibaini zinaweza kutumika kugundua kundi la damu mfano kuna MNS,Rh, KELL, LEWIS na ABO. ABO ndio mfumo unaotumika sana. Ndio mfumo unaotupatia makundi ya damu kama vile A, B, AB na O.
Mfumo wa ABO umeonesha usahihi wa hali ya juu kutokana na namna unavyofanya kazi. Ni mfumo unaohusisha moja kwa moja urithi wa sifa za chembechembe nyekundu za damu kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto.
Unapofika hospitali na kuonana nasi wanasayansi wa maabara tunakuchukua sampuli (damu) kisha tunaichakata na dawa maalumu kuangalia una kundi gani. Kwakweli hapa kwenye sindano huwa mnatusumbua sana lakini kipimo hiki hakichukui muda mrefu sana.
Kama nilivyosema mwanzo. Mfumo huu wa ABO (ambao ndio unatumika) unatupatia makundi ya damu aina nne A, B, AB na O. Baada ya hapa tunatumia mfumo mwingine wa Rh (Rhesus) kujua kama wewe ni A+ au A-
Hii + au - isikuchanganye sio ya UKIMWI. Kuna mzee mmoja niliwahi kumuambia ana group o+ kidogo azimie. Hii positive au negative kama inavyojieleza tu kwa tafsiri yake ni kutokuwepo (negative) au kuwepo (positive) kwa kitu tunaita rhesus factor.
Sasa kama ipo utaambiwa positive na kama haipo utaambiwa negative. Usijali nitaandaa siku maalumu niwaelekeze kwa undani zaidi leo naomba tuelezee kundi A, B, AB na O ambapo ukiongeza na mfumo wa Rh tunapata makundi A+,A-,B+,B-,AB+,AB-,0+ na O-
Kuambiwa una kundi A,B,AB au O inatokana na uwepo wa aina ya seli katika uso wa chembechembe zako nyekundi za damu. sasa kama una kundi A maana yake una seli A, kama B maana yake una seli B hivyo hivyo kwa makundi mengine. Ndio maana A huwezi kumpa mwenye B na B hivyo hivyo.
GROUP A: Ni kundi la damu ambalo mtu huyu anakuwa na aina ya seli A kwenye chembechembe zake nyekundu za damu.

Group A+ : Ukibainika una kundi hili basi ujue kuna watu aina 4 wanaoweza kukupatiaa damu. A+, A-, O+ na O- na unaweza kutoa kwa A+ na AB+.
Najua unajiuliza kwamba mbona nimesema kundi A anampa wa kundi A lakini hapa nimeongelea kundi AB?
AB ana seli zote A na B hivyo yeye kuchangia mwenye A haiwezekani kwani atampa na B ambayo itakuwa hatari kwake lakini kupokea kutoka kwa A inawezekana maana AB ana A ndani yake.
Group A- : Unaweza kupokea damu kutoka kwa A- na O- maana ukiwa negative inamaanisha huna rhesus factor hivyo mwenye positive (yeye anakuwa na rhesus factor) akikuamishia damu inakuletea matatizo. A- anaweza kumpatia mwenye A-,A+, AB- na AB+.
Umejiuliza tena inakuaje anampa mwenye positive? iko hivi mwenye negative ina maana hana rhesus factor hivyo damu yake haiwezi kuteta shida kwa mwenye rhesus factor.
Group B: Mwenye kundi B ina maana ana aina ya seli B kwenye chembechembe nyekundi za damu.

B+: unapokea kutoka kwa B+, B-, O- na O+ na unaweza kutoa kwa B+ na AB+ pekee.

B-: unaweza kupokea kutoka kwa B- na O- pekee na kutoa kwa B-, B+, AB+ na AB-.
Group AB: Hapa ina maana una seli zote A na B kwenye chembechembe nyekundu za damu.

AB+: Huyu kwa lugha ya kitaalamu tunamuita universal receiptient maana yake anapokea kutoka kwa makundi yote ya damu ila anampatia AB+ pekee.
AB-: unaweza kupokea kutoka kwa AB-,A-, B- na O- na unaweza kutoa kwa AB+ na AB- pekee.
Group O: Mwenye kundi O maana yake ni 0 (zero) yani hana seli zozote kati ya A na B kwenye chembechembe nyekundu za damu yake.

O- :Kitaalamu tunamuita universal donor yani anaweza kumpatia mtu mwenye kundi lolote la damu. Hawa watu ni adimu sana. Kama wewe ni mmoja wapo comment
O+: Kundi hili ni wengi sana. Hapa ndio wote tunakutana. Ni kundi lenye asilimia kubwa sana ya watu. Mtu huyu anaweza kupokea kutoka kwa O- na O+ na anaweza kutoa kwa A+, B+, AB+ na O+
Ukifatilia vizuri nimeongelea sana seli A,B,AB na O hizi sio seli kama unamaanisha seli nyeupe au nyekundu hizi kwa kitaalamu tunaziita antigen.

Kuna faida nyingi za kulijua kundi lako la damu hata wakati wa ndoa au wakati wa ujauzito. Kama utakua na swali usisite kuuliza.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Festo Ngadaya | #StayHome

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!