Mshindi na mbunifu wa jina "Tanzania" katika mashindano yaliyotangazwa mwaka 1964 akiwa kijana wa miaka 18 tu akisoma shule ya sokondari Mzumbe mkoani Morogoro.
Mohammed alisema nanukuu "Wakati huo nilikua maktaba nikisoma gazeti la Standards (sasa Daily News) nikaona tangazo la shindano hilo...
Ilimchukua dakika 5 tu kupata jina "TanZan" ikiwa ni muunganiko wa "Tan" (Tanganyika) na "Zan" (Zanzibar).
Muda wa kutangaza mshindi ulipofika familia yake ilipokea barua kutoka wizarani ikielezea pongezi kwa kijana huyu kwani ndiye aliyepatikana mshindi.
Mpaka leo Iqbal amekua shujaa asiyesikika katika vinywa vya watanzania, Wengi tumekua hatumfahamu na hatumuongelei katika historia ya Taifa letu la Amani Tanzania.