My Authors
Read all threads
MAMA FATMA KARUME; anasema mzee ABEID KARUME alimueleza, endapo atakutwa na mauti katika mapinduzi ya kumuondoa SULTAN katika ardhi ya Zanzibar, basi mkewe abakie kwa furaha na amani kwa sababu mumewe ni shujaa na akamtaka asomeshe watoto wao (endapo atakutwa na mauti). UZI 👇
PAULINE OPANGO LUMUMBA; mke wa mwanamapinduzi wa Zaire (sasa DR Congo) Patrice Emery Lumumba, alishuhudia kukamatwa kwa mumewe mjini Ilebo jimboni Kassai-Occidental kabla ya kuuwawa jimboni Katanga Januari 17, 1961. Alichofanikiwa kubaki nacho Pauline ni Barua ya Lumumba
Ambayo Patrice aliita “risala yangu ya mwisho kwa Pauline” Kwenye risala Patrice Lumumba alisema "sihofii maisha yangu mwenyewe, ikiwa itahitajika kumwaga damu yangu ili wakongo wapate uhuru wa kweli, kamwe siwezi kusita kuwa sehemu ya sadaka hiyo kwa taifa langu"
Pauline Lumumba alishuhudia mumewe akikamatwa, lakini hakuwahi kuona maiti ya mumewe hadi nae mauti yanamkuta. Mwili wa mumewe unatajwa kuchomwa na tindikali na kuyeyuka baada ya kuchomwa visu na kuachwa dakika 20 asikilize maumivu..
MARIAM SANKARA; Mke wa mwanamapinduzi, Thomas Isidore Nöel Sankara, alikuwa Rais wa Burkina Faso (Upper Volta) kuanzia 4 August 1983 kabla ya kuuwawa 15 October 1987. Sankara aliuwawa 1987 katika mapinduzi ya kijeshi ambayo yanatajwa kuratibiwa na rafiki yake Blaise Compaore.
Wakati Sankara anafariki, alimuacha mkewe mjane na watoto wawili (Phillipe na August). Wakati baba yao anafariki Phillipe alikuwa na miaka 7, August alikuwa na miaka 5. Baada ya kifo cha mumewe aliamua kwenda kuishi uhamishoni nchini Ufaransa, Mariam Sankara ameishi uhamishoni
uhamishoni Montpelier, France tangu 1987 hadi 2007 aliporuhusiwa kurejea Burkina Faso. Baada ya kurejea akaendelea kushinikiza kesi ya mauaji ya mumewe iliyokuwa imesahaulika ianze kusikilizwa upya na mahakama ikatoa amri kaburi la Sankara lifukuliwe mwili ufanyiwe uchunguzi
Winnie Madikizela-Mandela Mandela: miaka 27, Winnie aliishi bila uwepo wa mumewe (Nelson Mandela), mumewe wakati anafungwa jela kwa makosa ya uchochezi. (Mandela alifungwa mwaka 1963 na kuachiwa huru mwaka 1990) alimuacha Winnie na watoto wawili (1) mkononi (Zenani na Zindzi)
Winnie hakukata tamaa, aliendelea na mapambano ya kisiasa dhidi ya ubaguzi wa rangi. Mandela akiwa gerezani, kisiwani 'Robben Island'. Winnie anaaminika kuwa mmoja kati ya wanawake jasiri kuwahi kutokea Afrika katika historia ya kupigania haki za watu weusi wa Afrika kusini
Afrika Kusini inamtaja Winnie kama mama wa taifa, alifungwa gerezani akawaacha watoto wake uraiani. Akiwapigania wananchi wa RSA. Winnie na Nelson Mandela walikamilisha rasmi talaka yao machi 19, 1996. Pia Winnie amewahi kufungwa jela miezi 18 kwa kosa la uchochezi mwaka 1969
Graça Simbine Machel, ni mjane wa watu wakubwa wawili Afrika. Ni mjane wa Nelson Mandela na pia Rais wa zamani wa Mozambique, Samora Machel. 1975 baada ya Mozambique kupata uhuru, aliteuliwa kuwa waziri wa elimu na utamaduni wa taifa hilo, na baadae kuolewa na Samora Machel
1950, Samora Machel akiwa muuguzi katika kisiwa cha Inhaca alikutana na Sorita Tchaiakomo wakaanzisha mahusiano na kupata watoto. Joscélina, Idelson na Olívia

1963 kabla Machel hajajiunga na FRELIMO, alianzisha mahusiano na Irene Buque ambaye walipata mtoto anaitwa Ornila
Hakuwaoa Tchaiakomo au Buque. Mwaka 1969,Tunduru Tanzania, Samora Machel alimuoa Josina Abiatar Muthemba. Akiwa msituni na jeshi la FRELIMO akiusaka uhuru wa Msumbiji. Novemba mwaka huo, walimpata mtoto wao anaitwa Samora (Samito)..
Josina alifariki 1971 kwa ugonjwa wa kansa, miezi 3 baada ya uhuru wa Mozambique (1975) Samora Machel alimuoa Graça Simbine maarufu kama Graça Machel. Walipata watoto wawili Josina na Malengane.. Samora alikuwa rafiki wa Mandela. Wakawekeana nadhiri. Anaekufa mapema mke arithiwe
1986, Samora machel alifariki katika ajali ya ndege nchini Afrika kusini. Graça Machel ni mwanamke pekee ambaye ametumikia nafasi ya 'first lady' kwenye mataifa 2 tofauti. Mozambique 1975—1986 na Afrika ya Kusini 1998—1999, Graça Machel aliishi na mumewe kwa miaka 11 pekee.
Fathia "Rizk" Nkrumah, mke wa Rais wa kwanza wa Ghana huru, Osagyefo Kwame Nkrumah. Fathia alizaliwa katika wilaya ya Zeitoun katika nchi ya Misri. kabla ya kuolewa na Nkurumah, alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi inaitwa Notre Dame des Apôtres huko Zeitoun..
Aliacha kazi ya ualimu na kuanza kufanya kazi benki, huko alikutana na Kwame Nkurumah, ingawa mama yake Fathia alikataa kwa sababu Fathia alikuwa mwarabu wa Misri na Nkurumah 'mweusi' wa Ghana.., bado kulikuwa hakuna mahusiano mazuri ya rangi kati ya waarabu na waafrika.
Lakini mchana mmoja, mwaka mpya (1957—1958) walifunga ndoa. Mwaka 1966, mapinduzi ya kijeshi yaliyoendeshwa na wanajeshi katika nchi ya Ghana yanahusishwa na mkono wa CIA, waliwakamata na kuwaua wanachama wa chama cha kisiasa cha Nkurumah kiliitwa Convention Peoples Party (CPP)
Watu wengine waliobaki wakiwepo Kwame Nkurumah walikimbia nchi na kuanza kuishi uhamishoni. Kwame alikimbilia Guinea Conakry. Ambako alipewa hifadhi na Rais wa nchi hiyo Ahmed Sekou Toure. Huko alipewa heshima ya kipekee kama Rais wa nchi hiyo. Alithaminiwa sana.
Nkurumah alifariki kwa ugonjwa wa kansa mwaka 1972 akiwa na miaka 62. Hadi anakwenda kuishi uhamishoni Nkurumah alimuachia mkewe Fathia, watoto watatu wakiwa wadogo, Gamal (1959), Samiah (1960) na Sekou (1963). hivyo ameishi uhamishoni Guinea Conakry bila uwepo wa familia yake.
Wakati Kwame Nkurumah akiwa uhamishoni nchini Guinea Conakry, mkewe, Fathia "Rizk" Nkrumah aliishi pekee yake kwa upweke kwa miaka 6 tangu mwaka 1966 alipoondoka na kwenda Cairo baada ya mapinduzi ya kijeshi (coup d'état) February 24, 1966.
ALEIDA MARCH; (mke wa Ernesto Che Guevara), aliachwa na watoto wawili mkononi wakati mumewe akikutwa na mauti Oktoba 9, 1967 (akiwa na miaka 39) huko La Higuera, Vallegrande, Bolivia, Aleida walikutana na Che Guevara wakati wa mapinduzi ya Cuba kumuondoa Fulgencio Batista.
Aleida March alikuwa ni kati ya wanajeshi waliopigana upande wa jeshi la Fidel Alejandro Castro Ruz kutoka milima ya Sierra Maestra. Walikuwa kwenye mapinduzi ya kuondoa utawala wa kibabe wakati huo wa General Fulgencio Batista.
Ernesto El Che" Guevara Del Serna alimuoa Aleida March baada ya kuachana na Hilda Gadea Acosta ambaye alikuwa mchumi kitaaluma, mwandishi wa vitabu na mjamaa kutoka Peru.. Unaweza kuona sasa, Aleida aliolewa na Che Guevara akifahamu mumewe ni mwanamapinduzi.
BETTY DEAN SANDERS; maarufu kama Betty Shabazz, alikuwa mke wa Malcom X, mpigania usawa na haki za watu weusi na pia mwanaharakati wa haki za binadamu. Alifariki Februari 21, 1965 (akiwa na miaka 39) Manhattan, New York, USA, hadi anafariki, alikuwa amepata watoto 6.
Hadi Malcom X anauwawa alikuwa amefanikiwa kupata watoto sita ambao ni (Qubilah Shabazz, Ilyasah Shabazz, Attallah Shabazz, Malikah Shabazz, Gamilah Lumumba Shabazz, Malaak Shabazz). Betty aliachiwa watoto sita wa kutunza bila uwepo wa baba yao.
Rais wa 35 wa Marekani (1961—1963), John Fitzgerald "Jack" Kennedy, alifariki 1963, Dallas, Texas, USA.. Alimuoa Jacqueline Kennedy Onassis, Jacqueline aliachiwa watoto wanne (Caroline Kennedy, John F. Kennedy Jr., Patrick Bouvier Kennedy, Arabella Kennedy)
Martin Luther King Jr, alikuwa mhuburi wa injili wa dhehebu la Marekani la Baptist, moja kati ya waanzilishi wa vuguvugu la kudai na kupigania haki za wamarekani weusi, aligwa risasi Aprili 4, 1968, Memphis, Tennessee, USA Alikuwa amemuoa Coretta Scott King, wakapata watoto wanne
(Martin Luther King III, Dexter Scott King, Bernice King, Yolanda King), hivyo mwaka 1968 wakati wa kifo cha Martin, alimuacha Coretta akiwa mjane... Coretta alibaki na jukumu la kuwalea hawa watoto wake kwenye misingi na taswira ya baba Rao aliyekuwa mtu maarufu miaka ya 1960
wanawake wa sasa Tanzania yetu, wanawazuia waume zao wasiingie kwenye harakati za kisiasa za upinzani na hata kuwa wanaharakati, mbaya zaidi ni aina ya sababu zao wanazotoa, eti.., watabaki wajane waume zao wakiuwawa kwenye mapambano hayo na harakati za kisiasa..
Unaweza kubaki mjane bila mumeo kujihusisha na harakati za kisiasa, wapo wanawake wengi waliobaki wajane kwa sababu waume zao walikutwa na mauti katika ajali, magonjwa, ugomvi, vifo vya ghafla etc, Kuwa mjane hakutokani na mumeo kujihusisha na siasa za mageuzi pekee. JIFUNZENI
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Martin M. M

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!