My Authors
Read all threads
VISA VYA MADINI YA TANZANITE

#Thread

✴️Manuel De' Souza Fundi Cherehani na mgunduzi halisi ila hakupewa heshima,

✴️Mzee Ngoma atangazwa mgunduzi ilihali sio

Twende chap...

💨Asili ya Tanzanite
💨Historia yake
💨Visa ktk ugunduzi wake
💨Thamani yake
💨Sababu ya kuitwa hivyo👇
Kila mwaka July 07 huwa ni siku maalum na ukumbusho muhimu sana, na huwa ninafanya sherehe ya Birthday kwa ajili ya Mimi na Baba yangu (sisi wawili tulizaliwa siku hii), Lakini pia siku hii ndio madini ya Tanzanite yaligunduliwa.

Mwaka huu pia nilifanya..

Turudi ktk uzi👇
Tunapozungumzia juu ya vito vya thamani, basi fikra zetu kwa mbali hutupeleka ktk vito vya asili na bila shaka huwezi kukosa kuwazia madini ya Almasi, Emerald, Rubi na Lulu ila kama hufahamu Tanzanite ni moja ya madini ya asili na ghali sana na yenye historia tamu sana.

Twende👇
✴️MAANA & ASILI YAKE

💨Tanzanite ni Madini au kito (gemstone) chenye rangi ya Bluu hadi Zambarau na weusi ikiwa bado haijachongwa kuongezwa thamani ktk soko. Duniani pote madini haya yanachimbwa nchini kwetu Tanzania tu Mererani katika wilaya Simanjiro mkoani Manyara.
✴️ASILI

Tanzanite ilitokea kutokana matokeo ya athari za Tectonic plates movement ktk sehemu ndani zaidi ya dunia ambapo ndipo ulipo Mozambique Orogenic Belt ambao ni moja ya maeneo muhimu ktk muundo wa Dunia yenye utajiri mwingi wa madini.

Nitazaam deep siku nyingine

Twende👇
Kuna vitendo vya kimaumbo vingi ambavyo vilizopelekea kutokea madini haya mojawapo ni
💨Plate Tectonic Movement
💨Regional Metamorphism
💨Cooling & Solidification of Magma & Lava na
💨Melting mpk kupelekea matokeo kutokea

Naomba nitafute siku ili nielezee hii, Turudi ktk visa👇
✴️Madini ya Tanzanite ya rangi za kipekee na uzuri wake huonekana kutokana na pembe uliyosimama kuyatizama. Rangi za Bluu na Zambarau ndio rangi kuu ila unapoikata na kuichonga ama kuinakshi ndipo huiongezea thamani na muonekano mzuri ulioathiriwa na asili ya Vanadium na Titanium
HISTORIA

✴️Kisa cha MANUEL DE' SOUZA.

💨Kwanza kabisa licha ya kufichwa ukweli, madini ya Tanzanite yaligunduliwa kwa mara ya kwanza na raia wa India mwenye asili ya Kireno Bw. Manuel De' Mouse mnamo July 07, mwaka 1967 mkoani Arusha enzi hizo nchini Tanzania..

Shuka nayo..👇
💨De Souza ambaye alijulikana kama 'Mad Manuel' kama nilivyosema ni raia wa India aliyekuwa na asili ya Kireno, alizaliwa Jimbo la Goa nchini India mwaka 1913. Taaluma yake ni ushonaji nguo (Tailor) alikuja Tanganyika mwaka 1933 kabla WWII kama mshonaji aliyebobea.
Huyu ndiye mgunduzi halisi wa madini ya #Tanzanite moja ya madini yenye thamani sana, yanayopendwa duniani kuanzia karne ya 20 baada ya yale ya Alexandrite yaliyogunduliwa mnamo Aprili 1834 enzi za kina Alexandrite wa II wa Urusi.

Twende chap tuangalie aliyapataje?
Alipokuja Tanganyika aliamua kuwa msaka mali hivyo Baada ya vita ya II ya Dunia kuisha De Souza kutokana na ujasiri wake alimua kuchanja mbuga na misitu ya Kiafrika bila silaha na wakati mwingine kwa miguu kusaka madini yaliyobakizwa na wakoloni katika sehemu mbalimbali.
Moja ya sehemu ambayo De' Souza alikwenda ni ktk migodi ya dhahabu ya Lupa (Mbeya) iliyokuwepo magharibi mwa Tanganyika na alivyokosa mnamo mwanzoni mwa mwaka 1939 aliamua kurudi tena Dar es Salaam.
Akiwa Dar aliendelea na maisha huku akiendelea na shughuli yake ya ushonaji.
Kutokana na mikoa ya Pwani haikuwa na madini yeyote,
D'Souza aliamua tena kwenda Shinyanga katika migodi ya Almasi, Lakini kutokana sheria za kibepari zilizokuwa zimewekwa na wamiliki wa mgodi wa Williamson Diamonds ilikuwa ngumu kupata leseni ya uchimbaji.

Twende👇
Hivyo aliamua kwenda mikoa ya kanda ya ziwa (Victoria) ambapo huko nako alitafuta tafuta hakupata kitu.
Ndipo akili zikamtuma twende maeneo ya Kaskazini na akaamua kwenda Arusha kujaribu bahati yake katika maeneo ya Kilimanjaro.
✴️Siku moja mwaka 1967 ktk mapumziko ya sikukuu ya Pasaka akiwa barabarani gari iliwaharibikia njiani. Hivyo wakaamua kushuka sehemu hiyo iliyokuwa kusini mwa Arusha ili wapumzike kidogo kabla ya kuendelea.

Twende 👇
Sehemu waliyoshuka palikuwa panaitwa Kijiji cha Mtakuja, walipotengeneza gari alimwambia dereva na mwenzie watoke kutembea kidogo.
ILa kutokana na hali mbovu ya barabara dereva alikataa kwenda zaidi kwenye maeneo ya Wamasai kwa kuogopa misitu na tarambarare za nyasi nyingi
Hakujua pale alipokuwa ilikuwa umbali wa km 6 karibu na yalipogunduliwa madini ya Tanzanite (Mererani). Ila baadae aliamua kutembelea maeneo jirani ndipo akakutana na watu wanne inaosemekana walikuwa Wamaasai.
Watu wale alizungumza nao na akawaomba wamtembeze ktk maeneo jirani hawakumuelewa.
Ikabidi atoe kiasi fulani cha pesa akawapa wakakubali kumpa kampani ya kuzungukia vijiji jirani kutoka walipokuwa wamepaki gari.
Aliendelea kuzunguka maeneo ya kijiji cha Mtakuja mnamo trh 07 July akiwa njiani alijikwaa kwenye jiwe. Kutokana na rangi yake alidhania inaweza kuwa ni madini aina ya Sapphire baada ya kutizama lile jiwe alifahamu sio sapphire kutokana na ugumu wake.
Siku chache baadae alirejea Arusha mjini ili kuangalia ktk vitabu vyake vya madini ili kutambua itakuwa madini gani. Na baada ya kuyachunguza kwa muda na kwa umakini alidhania itakuwa ni madini ya aina ya Olivine kutokana na mfanano wake.
Mnamo July 25 1967 alikwenda ktk mamlaka za kiserikali akayasajili mawe yale kulingana na matakwa ya sheria iliyokuwepo kwa kipindi kile (mchimbaji wa madini alitakiwa kuyatambulisha madini kabla ya kuomba leseni kwa ajili ya uchimbaji).
Na baada ya hapo alirudi kuchimba.
👇
Haikuchukua muda mrefu De Souza aligundua kuwa haikuwa Olivine na alishindwa kabisa kutambua kuwa yalikuwa ni aina gani ya madini. Wengine walisema ilikuwa dumortierite, wengine wakasema itakuwa ni cordierite na waliokuwa wakizungumza Kiswahili waliyaita Skaibluu (sky-blue)
Aliposhindwa kabisa kuyatambua De Souza aliweka baadhi ya sampuli na kuzituma sampuli za katika maabara za Taasisi mbalimbali za Utafiti wa Madini zilizokuwepo kwa kipindi hicho ili kuyatambua kama ni aina gani ya madini.
Akiwa Arusha aliamua kumuita Beth Kabura kutoka Kenya👇
Dada huyu alikuwa mmiliki mwenza wa mgodi na Dr Saul Mmarekani aliyekuwa akichimba madini ya Berly katika mlima Kenya. Baadae Dr Saul aliamua kuja Mtakuja ili kuangalia hayo madini na yanapochimbwa, na ndiye alikuwa Geologist wa kwanza kuingia nchini baada ya Tanzanite kugundiwa
Alipokuja alichukua sampuli kadhaa akarudi nazo Kenya. Baada ya muda kidogo alimpa Taarifa baba yake Hyuman Saul kuhusu madini hayo ambapo mzee wake alifunga safari kuja Nairobi kuona yanapochimba na baadae akachukua baadhi ya sampuli akarudi nazo Marekani.
Dr. John Saul alikuwa raia wa Marekani, mtaalam wa utafiti wa madini yaani Geologist, mwenye elimu ya PhD kutoka chuo cha Massachusetts (M.I.T) na alikuwa akiishi Nairobi nchini Kenya akichimba madini aina ya Berly (Berylium na Aluminum) katika mlima Kenya.

Tuendelee..👇
Baba yake Dr John Saul,
Mzee Hyman Saul aliyekuwa Makamu wa Rais ktk kampuni maarufu ya Luxury American store, iliyokuwa Saks Fifth Avenue, alipofika Marekani alichukua sampuli zile akampeleka katika Taasisi ya Gemological Institute of America (G.I.A) ili kufanyiwa utafiti.
Kwa kipindi hicho taasisi zilizokuwa zinajishughulisha na masuala ya utafiti wa madini na vito hazikuwa nyingi sana na G.I.A ndiyo ilikuwa na wasomi wengi waliobobea ktk tafiti za madini na Vito mbalimbali duniani. Baada ya kupima walisema ni madini ni miongoni mwa Ziosite
Baadae sampuli ziligawanywa ktk sehemu 3, ambapo moja ilitumwa British Museum Uingereza ili kuangalia aidha ni mambokale na nyingine ikatumwa Heildelberg University Ujerumani iliyobakia waliichukua na kuita wasomi kutoka Havard University ili kusaidiana kufanya utafiti wa mwisho.
G.I.A kwa kushirikiana watalaam wa masuala ya utafiti wa mambokale na madini akiwemo Dr. William Pecora waliweka Tanzanite ktk kundi moja Blue Zoisite bila ya kuipatia jina, then wakaandika leseni ya kutambua mchimbaji na eneo yanapichimbwa ndipo walimtaja De Sousa km mgunduzi.
✴️JINA LA 'TANZANITE'

💨Kipindi sampuli hii imefika Amerika kulikuwepo na kampuni moja maarufu na kongwe sana ya Tiffany & Co. iliyoanzishwa mwaka 1837 na Charles Tiffany ikijishughulisha na masuala ya madini na usonara (ipo mpk leo inakadiriwa kuwa na utajiri wa Dolla 14.2 Bil)
💨Kampuni hii ilikuwa inaongozwa na mjukuu wa Louis Comfort Tiffany aliyeitwa Henry Platt akiwa kama Makamu wa Rais wa Tiffany & Co. Hivyo Mzee Hyman Saul alichukua baadhi ya sampuli na kumpelekea akiwa na Lengo ni kumuuzia na Platt alivutiwa na muonekano wake.
Baada ya kuliangilia jiwe alipenda na kumkaribisha Mzee Sauli kwenye meza ya chai kwa ajili ya mazungumzo. Platt aliipenda sana kw7bu liligunduliwa karne ya 20 na sababu nyingine ni muonekano tofauti tofauti mzuri wa kupendeza.
Hapa chini 👇ni Platt na mkewe ktk picha ya pamoja
Platt akaona jina la 'Blue Ziosite' halileti maana nzuri katika kutamkwa maana lilikuwa linatamkwa kama 'Blue Suicide' huwenda mapambo yake wanawake wengi hawatanunua na halitauza vizuri. Akabadili jina kuita #Tanzanite kutokana na nchi asili madini haya yalipokuwa yanapatikana.
Bw Platt baada ya kuona jina la 'Tanzanite' limekubalika na bidhaa zinatembea kwa kasi akaja na kampeni aliyokuwa akitangaza kuwa "kwa sasa madini ya Tanzinite yanapatikana Tanzania na Tiffany Co".

Tuendelee na habari za fundi cherehani tuone aliishia wapi👇
✴️DE' SOUZA & WAPINZANI DHIDI YA UGUNDUZI WAKE..

Twende chap..👇

Kama ilivyo ada wapinzani hawakosi hata katika msiba utakuta wengine wakilia machozi huku wengine utasikia wakizozana kisa msosi, naye De Souza hakukosa mpinzani. Akiwa anaendelea na uchimbaji wake kule Mererani
Akiwa anahangaikia kutafuta utafiti kamili ili afanye usajili, wengi walijitokeza wakidai ndio wagunduzi wa Tanzanite.Malumbano yao yalikoma baada ya Ian McCloud Geologist & mtumishi wa serikali (Tanzania) kutangaza kwamba Tanzanite inapatikana Tanzania na De Souza ndiye mgunduzi
✴️De' Souza akiwa na miaka 56 tu safari yake ilifika mwisho siku kama ya Jana August 21 mwaka 1969 miaka miwili tu baada ya ugunduzi wake kwa ajali ya gari akiwa Dodoma barabarani akielekea Dar es Salaam. Vyombo vingi vya nje vililiripo taarifa hii na ikaibua hisia zingine tena.
Muda mfupi baada ya kifo chake zilianza kuzuka habari kuhusu wagunduzi wengine wa madini ya Tanzanite.

#Wa kwanza alikuwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ally Juu ya Watu (inasemekana alikuwa Mmasai), akajitangaza kuwa ndio mgunduzi wa kwanza wa Tanzanite.
Alilalamikia vyombo vya Magharibi kuwa vinataka kupoteza ukweli na kupeleka sifa ya mgunduzi kuwa ni mzungu mwenzao. Lakini mambo yalibadilika baada Anthony Duwe mfanyakazi mwenzake kujitokeza na kumuita Ali mzushi na kumtetea Manuel De' Souza kama mgunduzi halisi wa Tanzanite.
Mwingine alikuwa Habib Esmail, yeye alipeleka kabisa barua serikalini akidai ndiye mgunduzi halisi wa Tanzanite na kipindi hicho alikuwa akimiliki kampuni ya madini aliyokuwa ameinunua kutoka kwa mchimbaji wa madini raia wa Ugiriki aliyefahamika kama George Pappas.
Mwishoni mwa 1969 ilitoka habari ktk jarida iliyosema De Souza alipata madini haya kwa kuongozwa na Wamaasai, Lkn Chief Soibhe kiongozi wa jamii ya Wamaasai alijitokeza na kukana taarifa hizo na kusema siku moja walikunywa maziwa ktk sehemu inayoitwa Naisinya Manyatta akiwa nayo
Maombi mengi ya kuomba vibali ikiwemo lile la De Souza alilotuma mwanzoni mwa 1967 yalifutwa baada ya serikali kuamua kutaifisha eneo la Merelani yalipokuwa yanachimbwa madini ya Tanzanite mnamo 1971 ambapo mwaka 1976 iliwekwa eneo chini ya uangalizi wa Tume ya Madini.
Kwa kumalizia kuhusu Manuel De' Souza, nyumba aliyokuwa akiishi kwa sasa ndio makazi ya Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK). Watoto na familia yake wametawanyika wengine wapo nchini, wengine Denmark, Malta na Uingereza.
✴️MZEE NGOMA NA TANZANITE

Mwaka 1984 alijitokeza mtu mwingine nadhani wengi tunamfaham anaitwa Mzee Jummanne Mhero Ngoma na kudai yeye ndiye mgunduzi wa madini ya Tanzanite na serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia ilimpa cheti cha kumtambua na kiasi cha fedha shs 50,000
Ukikumbuka hivi karibuni mwaka 2018 Rais Magufuli alimtangaza upya na kusema anamtambua tena kama shujaa aliyegundua Tanzanite na kumpa shilingi Milioni 100 kwa ajili ya kumsaidia kujikimu na matibabu baada ya mzee huyo kupooza sehemu ya mwili.
Mzee Jumanne M. Ngoma alizaliwa mwaka 1939 mkoani Arusha, kabila ni Mmeru, na Jumatano ya Trh 30 January, 2019 majira mchana ilitangazwa kuwa amefariki Dunia ktk Hospitali ya Taifa, Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akipewa akipewa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mzee Ngoma aliwahi kuwa mfanyakazi wa Habib Esmail kama mshauri wake ktk masuala ya madini huko Mererani na huko ndipo alisema aliyaona madini hayo na serikali ikaamua kumtangaza kama mgunduzi wa kwanza na hakuna taarifa zingine za ziada zinazoonyesha kuwa ndiye alikuwa mgunduzi.
MWISHO;-

Baada ya serikali kutaifisha iliamua kuligawa eneo la Mererani katika vitalu vinne (A, B, C na D). Kitalu A kilichokuwa kusini Magharibi walipewa kampuni ya Kilomajaro Mines Ltd iliyokuwa inamilikiwa na Mfanyabiashara, kitalu B & D walipewa wachimbaji wadogo.
Aidha, kumewahi kutokea mafuriko yaliyoua watu 200 mwaka 1998 ktk kitalu B na ukikumbuka hata mwaka 2008 wachimbaji 74 walipoteza maisha na kitabu C walipewa wazungu ambao ndio hawa Tanzanite One Group (T.O) wazalishaji wakubwa duniani wa Tanzanite katika nchi ya Afrika kusini.
#USICHOKIJUA..

✴️Tanzanite ni moja ya madini yenye thamani kubwa. Thamani yake ni ghali na bei zake zinacheza kati ya dola za Marekani 200 na 650 kwa karati moja (Carat 1 = Milligram 200).
2. Aidha, unaambiwa kuwa baada ya ugunduzi rasmi mnamo 1967, inakadiriwa kuwa ni karati 2,000,000 tu za tanzanite ndio ambazo zilizokuwa tayari zimeshachimbwa kabla ya serikali kutaifisha maeneo ya Mererani ili kuchimbwa kwa utaratibu.
✴️Kama ilivyo kwa madini mengine vito vya Tanzanite ni zaidi ya miaka milioni 585 iliyopita chini ya vilindi vya mlima mrefu Afrika Mlima Kilimanjaro ndio kito cha Tanzanite kiliumbika, lakini kilikaa kwa muda ndipo kikagundulika mwaka 1967 ktk nchi pekee Tanzania.
✴️Madini ya Tanzanite yana rangi za kipekee na uzuri wake huonekana kutokana na pembe uliyosimama kuyatizama. Rangi za Bluu na Zambarau ndio rangi kuu ila unapoikata na kuichonga ama kuinakshi ndipo unapoingezea thamani na muonekano mzuri ulioathiriwa na Vanadium na Titanium.
✴️Inakadiriwa zaidi ya watu milion 2.7 duniani wamepata ajira kutokana madini ya Tanzanite kuanzia kwenye uchimbaji, ukataji, na ufanyaji biashara kama vile usonara. Kwa Tanzania pekee madini haya yamezalisha ajira za watu zaidi ya 70,000.
Laizer mwenyewe ametoa ajira 200 👇👇
✴️Kingine usichokijua ni kuwa Miongoni mwa watu ktk jamii ya Wamaasai huchukulia rangi ya bluu iliyopo kwenye madini haya kama rangi iliyobeba bahati na mwanamke wa kimaasai anapojifungua hupewa kipande cha kito hiki kama ishara ya kumtakia malezi mema ya mtoto na afya njema.
Kabla Laizer kupata mawe mawili makubwa na kushikilia rekodi ya kupata Tanzanite yenye uzito mkubwa kuliko yote (9.72/5.103)Kg ambapo aliuza zaidi ya Bil 7.4 palikuwepo na jiwe lililokuwa na uzito wa 3Kg (16,839 carats) ambalo lilipewa jina la Mawenzi ili kuenzi Mt. Kilimanjaro
Ahsanteni sana 🙏🙏

Shukreni ziwaendee wote mlioretweet, kulike na kucomment/kureple..
Cc. @SaidiKichenje
@mkomonisti
@balozi_twita
@pompeowabuza
@njiwaflow na @JacquilineHenr7 kwa support yenu.

RTs iliwafikie wengi wajifunze kidogo.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with JAPHET MATARRA

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!