My Authors
Read all threads
MELI KUBWA YA MIZIGO
MS MUNCHEN ILIVYOTOWEKA DUNIANI
#cipherdotseriesandmoviesuzi
#CertifiedThreads
Meli ya MS Munchen  ilikuwa ni meli ya mizigo ya kijerumani iliyozama December 1978 pakiwepo na nadharia moja ya kuwa meli hii ilipigwa na Rogue Waves( Rogue hujulikana kwa majina
...kwa majina mengi kama freak wave, monster wave, episodic waves, Killer waves, Extreme waves na abnormal waves...Haya ni mawimbi makubwa sana yanayoweza kwenda juu mita 70 hadi 300 (kwa utafiti wa hivi karibuni) sawa na viwanja vitatu vya mpira mguu kutokea kwenye usawa wa
...usawa wa bahari, hutokea ghafla bila sababu inayofahamika na kupotea kama lilivyokuja, huja na nguvu ya ajabu na uharibifu utakaofanya kwa kipindi hicho kifupi ni mkubwa na wa kutisha, huja bila taarifa inasemekana huweza kuvunjika au kuigonga meli kwa nguvu ya tani mia
...mia za mraba) haya wazee turudi kwenye maada yetu. MS Munchen ilikamilika  may 12, 1972 huko kwenye karakana za meli za Hoboken, Flanders, Belgium na kukabiziwa September 22, 1972 ilikuwa meli ya mizigo ya aina ya LASH;(sijapata kiswahili fasaha) na ilikuwa meli ya kipekee
...kipekee iliyokuwa inapeperusha bendera ya kijerumani kwa wakati huo
Munchen iliondoka bandari ya Bremerhaven tarehe 7, December 1978 miaka 6 baada ya kutengenezwa ikielekea bandari iliyoko Savannah Georgia hii ilikuwa ndo njia yake ya kawaida kwa miaka yote 6 ikiwa imebeba
...wa chuma na mizigo mingine, ilikuwa na uwezo wa kubeba tani 44,600 na kwa siku hiyo ilikuwa pia na mabaharia wapatao 28 meli hii ilikuwa na urefu (length) wa mita 261.4 karibia urefu wa viwanja vitatu (length) upana wa mita 32.2(beam) ikiwa na  kimo cha mita 18.29( height)
...Kwa MS Munchen hii ilikuwa safari yake ya 62 iliyoichukua meli hii kuvuka bahari ya Atlantic ambayo kuanzia Novemba ilikuwa na vimbunga na dhoruba kali sana, pamoja na uzito wake na aina ya mizigo inayobeba meli hii  iliheshimika na kwa maana ilichukuliwa kuwa ni meli
...isiyoweza kuzama (unsinkable) MS Munchen iliendelea vizuri na safari yake hadi kufikia usiku wa kuamkia  tarehe 13 December ndipo mauza mauza yalipoanza
Saa 00: 05 na 00: 07 (GMT) Munchen ilitoa taarifa kwa afisa Jorg Ernst taarifa ya hali ya hewa kuwa mbaya na uharibifu mdogo
...kwenye meli na kuumia kwa baharia moja ndani ya meli kwa meli nyingine iliyoitwa MS Caribe meli nyingine ya kijerumani iliyokuwa umbali wa maili 2,400 sawa na kilometa 4,44o hali ya hewa ilikuwa mbaya mawasiliano hayakuwa mazuri  na afisa huyo akuelewa vizuri alichoambiwa na
...na wala hakutoa taarifa kwa wamiliki wa meli hiyo, kweli siku ya kufa nyani miti huteleza. Taarifa hizi zilifika kwa wamiliki wa meli tarehe 17 December 1978

Wito wa shida (Distress Call)
Masaa matatu baadae ujumbe SOS (SOS ni siginal yenye dots 3  dash 3 na dots 3 pasipo
...nafasi ktkt ..._ _ _...) Ujumbe huu ukipokelewa na chombo chochote kilichokaribu kinatakiwa kwenda kutoa uokozi, huo ni wito sawa na mayday, basi SOS kutoka MUNCHEN ilipokelewa na meli ya kigiriki Panamax ambao nao wakautuma tena na kupokelewa na meli ya Kirusi ya Yermelova na
...tug boti ya kijerumani Titan, MS Munchen ikatoa sehemu ilipo ambayo ilioneka  hadi taarifa inapokelewa muda mrefu ulikuwa umepita na wakahic labda itakuwa imeshatembea zaidi ya km 200 nje ya eneo iliyokuwepo mwanzo
Na kuanzia sa 04: 43 signal za dharura ziliweza kupokelewa kwa
...radio station zote ilipofika saa 7: 34 hakuna mwiito uliosajiliwa labda kwa sababu utafutaji wa meli ulikuwa umeanza, meli ya MS Munchen ikawa imepotea kutoka uso wa dunia

Kuitafuta meli ya Munchen.
Msako ulianza tarehe 13 December ndege aina ya Lockheed c-130 Hercules
...kutoka ujerumani na meli sita zilianza kuhusika na msako wa MS Munchen, siku hiyo saa 03:06 asubuhi michael Sinot mbeligiji aliyekuwa hajabobea kwenye mambo ya radio siginal alipokea ujumbe katika frequency isiyo ya kawaida na ujumbe ulikuwa na makelele lakini aliweza kusikia
...jina MS Munchen na alama ya mwito wao( call sign) baadae wakiwa mahakamani sinot alisema kuwa alipokea ujumbe wa mtu aliyekuwa amatulia(calm) aliyekuwa anaongea kiingereza chenye lafuzi ya kijerumani na kwa kuwa sinot ndo pekee alipokea ujumbe huu aliutuma kwa telex kwenda.
...kwenda radio staion huko Ostend
Kufikia saa 11 jioni na saa 1: 19 usiku MAYDAY iliyokuwa dhaifu sana ilipokelewa na kituo cha radio cha jeshi la maji la kimarekani nchini spain inaonaka ujumbe huu ulirekodiwa na kujituma kila baada ya muda fulani ukisema "Watu 28 ndani ya
...meli" Meli (tug) ya ukoaji ya uholanzi iliyokuwa ikirudi nyumbani baada ya kufanya uokoaji meli nyingine ikapata ujumbe huu ikageuza na kuelekea eneo la ajali, meli (tug) ilipofika eneo la ajali  Nahodha wa meli hiyo ambao huwaga na ujuzi mkubwa ktk uokoaji  akaanza kupanga
...mpango wa utafutaji pakiwepo zaidi ya meli 100 na ndege 16 angani kwenye eneo hilo la ajali lkn MS Munchen Haikuonekana kabisa wala dalili yake yoyote, msako ulikuwa mkali sana meli zote 100 zilizokuja kutoka na ule wito wa SOS zilifanya utafutaji wa nguvu kwa kutumia kila
...aina ya utaalamu na teknolojia waliokuwa nayo kwa wakati huo, na ndege nazo angani zilihangaika kwa kadri ya uwezo wake wakipigina angalau wawaokoe mabaharia 28 waliokuwepo ndani ya meli lakini mpaka kuna kucha MS Munchen Haikuonekana katika uso wa dunia ikapotea
...kabisa bila hata kuacha dalili (Vanished)

Kufikia tarehe 14 December 1978 upepo mkali na hali ya hewa mbaya vikapungua baadhi ya meli ziliendelea na safari kukabaki meli 17 na ndege 4 kuendeleza utafutaji wa MS Munchen
Kufikia saa saa 1 usiku wa tarehe 14 meli ya uingereza
...iliweza kupata boat tupu la kukoa maisha(life raft) lilotoka kwenye Meli ya Munchen, siku hiyo hiyo meli iliyoitwa Hapag-LLoyd iliweza kugundua baadhi ya vifurushi vitatu vya mizigo kwenye lighter carrier
Pamoja na msako wote huu na juhudi zote hizo meli ya Munchen
...haikuonekana kabisa na ikashangaza sana kuwa imepotelea wapi, kufikia December 20 wiki moja kuanzia msako ulipoanza msaka ulisimamishwa lkn serikali ya Ujerumani wakisaidiwa na Hapag-Lloyd waliamua kuendelea kwa siku 2 zaidi wakasaidiana na majeshi ya serikali ya Uingereza na
...na Marekani ikiwa kwa pamoja na ndege 13 kutoka UK, USA, Ureno na wajerumani wenyewe, kitu cha mwisho kuoneka ilikuwa life boat iliyopasuka ubavu mmoja, na huu ndo ulikuwa mwisho wa kuitafuta meli hii ikawa imepotea kabisa kutoka uso wa dunia meli waliyosema haizami ilizama
...na kupotea kabisa

UCHUNGUZI:
Uchunguzi wote wa meli hii ulizingatia (based) life boat ile ambayo iliyokuwa imepasuka ubavuni maboti haya uokoaji huning'inizwa juu na kushikiliwa na chuma zenye aina ya ndona mwishoni, chuma iliyoshikilia boat ilipinda kwa kuelekea ndani
...ikionyesha kuwa boat ilipigwa na kitu chenye nguvu kubwa kutokea ubavuni na kwa kawaida life boat huning'inizwa mita 20 kutoka kwenye usawa wa maji na kwa wakati huo hawakuweza kuwaza kuwa Rogue wave inaweza kufikia kimo hicho wakiwa hawaelewielewi kilichotokea  wakaamua
kusema hali ya hewa mbaya kimbunga na dhoruba ndio chanzo cha kupotea kwa meli hiyo
Nyongeza kutoka vijalada
Kwa wakati huo walisema haiwezekani kwa Rogue Waves kuwa kubwa zaidi ya mita 75 kwenda juu na kama hali hiyo ikitokea basi itatokea baada ya miaka 4000 lakini cha
...kilitokea pale mtambo wa kuchunguza mawimbi ulipofungwa kwenye setelite na kusoma tabia za mawimbi, inasemekana katika wiki 2 tu za uchunguzi huo  kulitokea Rogue Waves kumi zilizokuwa na ukubwa wa zaidi ya mita 300 kutoka usawa wa bahari zilizosajiliwa na mtambo huo kwa
...kipindi hicho kifupi...kama hii ndo hali meli hii iliwezaje kupita njia hii zaidi ya mara 62 bila shida?? Je kweli hizi Rogue waves ni za asili au kuna nguvu za ziada kama wanavyoamini mabaharia wote kuwa kuna nguvu kubwa ya giza inayozamisha meli na kutengeneza mawimbi ya
...kuua. kama una rafiki baharia (sio hawa mabaharia wa instagram) piga naye story akupe hii Myth mimi sitaki kuisema kwa maana nikisema utasema mimi mshirikina kwa maana HAKIKA ningekuacha hoi.
Usisahau hii ni Cipherdot Series and Movies waliopo DODOMA Tanzania
...Tufuate kwenye Ukurasa wetu wa Twitter@cipherdotm au @cipherdotsv kwa kupata UZi kama huu au kwenye page yetu ya instagram kwa kupata update za movies na series bit.ly/2nRLyzV

PLEASE RETWEET
PLEASE FOLLOW US WE FOLLOW BACK
@CipherdotM @CipherdotSV
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Cipherdot Series And Movies✍️

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!