My Authors
Read all threads
UFAHAMU MFUMO WA KODI NA MAPATO YA SERIKALI ZA MITAA

Serikali za mitaa zikiwa ndani ya Halmashauri za miji/Majiji na Wilaya zina mamlaka ya kukusanya mapato na ushuru kutoka vyanzo mbalimbali vya kodi. Pia zina mamlaka ya kutumia mapato hayo kwa mujibu wa sheria.

T H R E A D👇
Kulingana na mipaka ya kisheria inayowekwa na Serikali Kuu, hizi Serikali za mitaa zina uwezo wa kutengeneza sera zake za mapato ili kuleta maendeleo katika shughuli zinazogusa kwa ukaribu maendeleo jamii nzima kama mashule, hospitali, mazingira ya mitaa na ulinzi shirikishi.
Mapato haya yanayokusanywa yanapata Mamlaka kutoka katika Sheria ya Mapato ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1983 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Sasa leo ukimaliza kusoma makala haya, utakuwa umezijua kodi/tozo zote zinazokusanywa pamoja na matumizi yake kwa ujumla.
Idadi ya kodi na ushuru unaokusanywa chini ya Mamlaka ya serikali za mitaa hutofautiana kutoka Halmashauri moja na Halmashauri nyingine. Mambo yanayoleta utofauti huu ni maendeleo katika sekta za Biashara, makazi, Uwepo wa maliasili na shughuli za kiuchumi.
Kuna baadhi ya tozo hukusanywa kwa siku, zingine mlipakodi hutozwa kwa mwaka, na zingine humpa nafasi mlipakodi kuchagua wakati wa kulipa (kwa mwezi, wiki, miezi mitatu/sita au kwa mwaka). Mfano; ushuru wa masoko, huu kawaida hukusanywa kwa siku. Hata hivyo Halmashauri zingine
hutoa nafasi kwa mlipakodi kulipia ushuru huu kwa mwezi, miezi 3/6 au kwa mwaka mzima. Mwisho wa mwaka wa fedha kila Halmashauri inatakiwa kuandaa akaunti za kifedha ikiwa na wadau wafuatao:
i. Halmashauri Nzima
ii. Muwakilishi wa wizara (TAMISEMI)
iii. Ofisi ya Waziri Mkuu
iv. Ofisi ya Mdibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG)
v. Umma

Serikali za Mitaa hupata mapato yake kutoka katika vyanzo vikuu vitatu:
1. Mapato yake yenyewe
2. Ruzuku kutoka Serikali Kuu
3. Misaada kutoka mifuko ya Maendeleo.
MAPATO/KODI ZINAZOTOZWA

1. USHURU WA BIDHAA (PRODUCE CESS)
Ushuru huu hutozwa na halmashauri kutoka katika mauzo ya mazao kama mahindi, mchele, kahawa, chai, pamba korosho pamoja na mifugo. Ushuru huu hutozwa kutokana na uzito/ujazo wa bidhaa yenyewe. Hii hufanya thamani ya
bidhaa kutokua thabiti ikitegemea uzito/ujazo wa bidhaa (the source to be inelastic unless adjustments become frequent enough to catch up with inflation), hapa watu wa uchumi mtakuwa mmenipata vizuri sana. Viwango vya ushuru huu hubadilika kutegemeana na Halmashauri kutokana na
Jiografia ya eneo, misimu ya hali ya hewa pamoja na hadhi ya kiuchumi ya Halmashauri husika.

2. LESENI ZA BIASHARA
Kodi hizi hutozwa kutokana na ukubwa na aina ya biashara, yaani maduka mawili ya rejareja yatatozwa kodi ya leseni sawasawa bila kujali ukubwa wa mitaji yao au
hesabu zao wanazowasilisha kwenye mamlaka za mapato (turnovers).

3. ADA YA MASOKO
Aina hii ya Ushuru kwa kawaida hutozwa kwa siku kwa wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao katika maeneo ya sokoni. Viwango vya tozo hii hubadilika kulingana na bidhaa zainazouzwa.
4. KODI YA ARDHI/MAJENGO
Kisheria, Serikali kuu inatakiwa kukusanya kodi kutoka kwenye mali zote zinazohamishika, wakati Serkali za Mitaa zitakusanya kodi katika mali zote zisizohamishika. Hata Hivyo, kodi ya ardhi na majengo haijaweza kutumika ipasavyo katika mambo ya kisiasa
na uongozi katika nchi zinazoendelea. Katika kitabu chake kuhusu kodi ya ardhi, Richard Bird (1974:223) anasema, "The administrative constraint on effective land on effective land tax administration is so severe in most developing countries today that virtually all the more
refined fiscal devises beloved by theorists can and should be discarded for this reason alone. Not only will they not be well administered, they will in all likelihood be so poorly administered as to produce neither equity, efficiency, nor revenue." Nadhani hoja yake imeeleweka😀
5. USHURU WA HOTELI/NYUMBA ZA WAGENI
Kodi hii kisheria hutegemea na tathmini binafsi kuhusu hesabu za hoteli/nyumba za wageni. Viwango vikubwa vya kodi huhamasisha ukwepaji wa kodi hasa kwa kurekodi hesabu mara mbilimbili. Katika utekelezaji, hasa kwa biashara ndogo ambazo
hazitoi risiti, turnover zao hukadiriwa tu na hivyo kupunguza mapato kwenye serikali za mitaa. Hata hivyo, biashara kubwa ambazo pia hazitoi risiti huwekewa utaratibu wa kufanya maridhiano kati ya wakusanya kodi na walipa kodi. Utaratibu huu unaongeza gharama za uendeshaji
na kuongeza mianya ya rushwa. Hata hivyo, kutokana na makusanyo haya kuzingatia asilimia za mapato ya biashara, makusanyo yanategemewa kubadilika kadhalika.

6. KODI YA MABANGO/MATANGAZO
Hii kodi wafanyabiashara wengi huilalamikia, wengine wasijui kwanini wanatozwa wakiweka tu
mabango katika biashara zao. Viwango vya kodi hii hutegemea ukubwa wa bango, kama linawaka taa usiku na muda bango hilo litakavyokuwa wazi. Mapato ya mabango yanaendelea kukua kutokana na kuongezeka kwa biashara ambazo pia zinahitaji matangazo kujiimarisha.
7. USHURU WA MCHANGA
Unashangaa? Hadi mchanga wa kujengea unalipiwa kodi ndio katika baadhi ya halmashauri. Gharama ndogo za mchanga pamoja na kuongezeka kwa kasi ya watu kujenga kumechochea mmomonyoko wa udongo kwenye machimbo jambo lilifanya serikali kupiga marufuku
Uchimbaji holela wa mchanga na kuanzisha utaratibu mpya wa kuchimba mchanga katika maeneo maalum na hivyo kudhibiti mapato yatokanayo na mchanga.

8. USHURU WA MACHINJIO/PARKING
Halmashauri nyingi ambazo zina machinjio ya wanyama na maengesho ya magari hutoza kodi hio vizuri.
Mapato yatokanayo na kodi hii yamekuwa yakiongezeka hasa maeneo ya mijini ambapo kumekuwa na uhitaji mkubwa wa maegesho ya magari na pikipiki pamoja na kuongezeka kwa wanyama wanaonmchinjwa katika maeneo maalum. Hii ni kwa kuwa serikali imefanikiwa kudhibiti machinjio zote za
mitaani na kulazimisha wanyama wote kuchinjwa maeneo maalum ya machinjio ambayo yana udhibiti wa kiserikali na kuzingatia viwango vya nyama kwa manufaa ya walaji. Wale wanaopajua vingunguti watakuwa wamenipata sawasawa hapa.
9. KODI ZINGINE
Serikali za Mitaa hukusanya kodi nyingine nyingi sana. Unaweza kuzipata kwa ufupi katika tovuti rasmi ya Wizara ya Fedha kupitia link hii👇
mof.go.tz/mofdocs/revenu…

Serikali za mitaa hazitozi kodi ambazo zipo nje ya zilizopo kwenye listi iliyo kwenye link hio👆
Vile vile unaweza kupata maelezo kuhusu Kodi na wajibu wake katika matumizi ya mwaka 2018/2019 kupitia link hii hapa chini 👇
rednet.co.tz/download/taxes…

HIZO KODI ZINATUMIKA VIPI?
Kodi zinazokusanywa na Halmashauri za Wilaya/Miji/Majiji hutumi kodi hizo kuimarisha mambo yafuatayo
i. Ulinzi shirikishi
ii. Barabara za mitaani pamoja na miundombinu yake
iii. Zimamoto na uokoaji
iv. kuimarisha shughuli za kiuchumi (masoko, biashara) nk

Uzi umedhaminiwa na @chawanyu kiwango cha #CertifiedThreads

cc @Mkuruzenzi @tonytogolani @mpambazi_ @Sirjeff_D @chapo255
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Faustine

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!