Hivi ndivyo alivyoungua Bibi yangu. akisimulia dada mmoja na machozi yakinilenga.
Ilikua majira ya saa 2 asubuhi Oktoba 27, 2020, Unguja, maeneo ya Garagara Mtoni Kidatu.
Mara ghafla nyumbani kwetu askari wengi wemejazana mlangoni. Wanagonga...🧵
mlango kwa kishindo kikubwa huku wakisema "Fungua Fungua" tupo nyumbani mimi, ndugu zangu, mama na Bibi yetu ambae ni mgonjwa ana stroke.
Mara mama akajibu "hatufungui Mlango".
Askari wakajibu "Nasema fungua" dozen ya Askari mlangoni mara malango ukavunjwa.
Wanaingia ndani...
tokeni hatutoki bomu la kwanza (Bomu la machozi).
Mama akajibu watoto wangu wamefanya nini hapa hawatoki.
Bomu la Pili tukaingia chooni huku tukinawa nyuso zetu, bibi yetu hawezi kuinuka wala kuita wala kukimbia.
Dada yangu yupo chumbani na mtoto mdogo akawa analia kwa moshi..
mkali wa mabomu. Mara likapigwa jengine moto ukawaka askari wakatoka ndani, moshi umetanda hatuonani ndani na moto unakolea.
Tukatoka nje askari washaondoka, tahamaki Bibi anaungua ndani tukafanya jitihada kumuokoa bibi yetu Allah kamnusuru na Umauti lakini kaungua Bibi yetu...
nahisi uchungu. akiendelea kusimulia.
Vitu vyote vimeungua kosa lao ndani ya nchi yao hawaliju. pole nikiendelea kumsikiliza.
Nani wa kuwasaidia? majirani wema wanaendelea kumsaidia Bibi yao yupo Mnazi Mmoja kwa matibabu.