Alizaliwa kwenye familia ya kitajiri,akiwa na miaka 8 akafundishwa biashara.Akasoma chuo kikuu kisha akapewa mkopo na mjomba wake akaanza kufanya biashara.Baba wa watoto 3,aliyeoa mara mbili ila ndoa zikavunjika,tajiri namba moja Afrika,Aliko Dangote anazidi kuwa tajiri kila siku
Miradi ya uwekezaji anayofanya Aliko Dangote ambaye pia ni mtu mweusi tajiri zaidi duniani ni mikubwa mnoo.Kiwanda chake cha Sukari ndicho kinachozalisha zaidi Sukari bara la Afrika na cha 3 kwa uzalishaji duniani kote.Dangote anasomesha na ameajiri wengi,pia anatoa misaada sana.
Aliko Dangote ambaye pia ni miongoni mwa watu 200 tajiri zaidi duniani.Alipoulizwa Kwanini haachi kuzidi kutanua biashara alisema “kama huna malengo,haupaswi kuwa unaishi”. Dangote anapenda football na amesema ataichukua timu ya Arsenal baada ya mradi wake wa mafuta kukamilika.
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Akiwa na miaka 27 alifanya mapinduzi akawa rais.Akainua uchumi wa nchi yake kupitia biashara ya mafuta,akaandika kitabu ambacho ilikuwa ni lazima wanafunzi wakisome “Green Book”.Miaka 42 ya kuitawala Libya Gaddafi akajiita Mfalme wa wafalme,kiongozi wa mapinduzi.Mwisho akauawa.
Gaddafi alipiga marufuku biashara ya pombe na lugha ya kiingereza kutumika nchini kwake.Pia akafunga kumbi za starehe na bar.Vile vile alifanikiwa kuweka makubaliano na Makumpuni ya mafuta yaliyoiwezesha Libya kupata Pesa nyingi.Akajenga shule,hospitali na miundombinu yakutosha.
Rais Ronald Reagan wa Marekani alipoingia madarakani alimuita Gaddafi “Mbwa Kichaa”1986 akaamuru ndege za kivita kushambulia makazi ya Gaddafi,Kwa bahati hakuwepo hivyo akanusurika. USA chini ya Reagan ikakataa mafuta ya Libya na kumuwekea vikwazo lukuki.Gaddafi hakurudi nyuma.