Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu tumefarijika sana na Hotuba iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali wa juu serikalini. Tunatoa taarifa kwa Umma juu ya maswala machache yaliyoangaziwa katika hotuba hiyo ambayo ni pamoja na
Uhuru wa Habari
Kwa miaka kadhaa sasa kumekuwa na malalamiko yenye mashiko kuhusu uhuru wa Habari nchini Tanzania na ambayo kwa kiwango kikubwa ilikiuka katiba ya nchi katika Ibara ya 18. Kipekee kabisa tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa maelekezo
Tunaisihi serikali kuharakisha mabadiliko ya sheria na kuondoa viunzi vya sheria zinazotoa mianya kwa mamlaka za mawasiliano, na idara zingine za serikali kuminya uhuru wa habari kinyume na Katiba ya Nchi
Haki elimu
Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha Elimu nchini na kipekee kwa watoto wa kike kupata elimu. Tunatoa rai kwa serikali kuendelea kushughulikia swala la watoto wa kike wanaopata ujauzito bila ridhaa yao kuendelea kupata elimu kwenye shule za umma ama
kuanzishwa mpango maalum katika ngazi ya wilaya ambapo watapata fursa ya kuendelea na elimu katika mfumo rasmi.
Mifumo ya Kodi
Kwa muda sasa, kumekuwa na malalamiko ya wafanyabiashara na wananchi juu ya mifumo ya kodi nchini. Malalamiko haya yalipata nguvu katika Bunge la Tanzania kwamba Mamlaka ya Kodi Tanzania inakusanya kodi kupitia kikosi maalum ambao hawafuati misingi ya sheria na
hivyo kuminya haki za wawekezaji na watanzania. Kituo cha sheria na Haki za Binadamu kinafarijika na wito wa Rais kwa mamlaka za Kodi kuzingatia sheria lakini Wakati huohuo kuangalia uhalisia na kupunguza matumizi ya mabavu.
Tunatoa wito kufanyika kwa mabadiliko ya sheria ya kodi ili kuondoa uwezekano wa watu kubambikiziwa kodi kubwa ama kesi za uhujumu uchumi kama alivyosema Rais.
Ugonjwa wa COVID-19
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu inaungana na serikali hatua madhubuti za kisayansi zichukuliwe ili kuwakinga watanzania na janga la Corona. Tunaisihi serikali kutangaza hatua zaidi za kujikinga wakati Mh Rais akiunda Tume itakayomshauri kuhusu hatua
sahihi za kisayansi za kuchukua ikiwemo haja ya kufikiria kuhusu chanjo kwa wananchi.
Haki ya kuishi na makazi, Ngorongoro
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinatambua historia ya Haki za Binadamu Ngorongoro ambayo imekuwa na changamoto nyingi ndani ya takriban miaka sitini ya uwepo wake. Tunatambua maslahi ya kiuchumi kwa nchi, maslahi ya kimataifa kama sehemu
ya urithi wa Dunia lakini kwa Umuhimu mkubwa tunatambua maslahi na Haki za wenyeji wa eneo la Ngorongoro na jukumu lao kufanya eneo la Ngorongoro kuwa na umuhimu iliyonayo.
Tunatambua hali ya Haki za Binadamu katika eneo la Ngorongoro limekuwa likipigiwa kelele kwa muda mrefu sana. Tunatambua mchakato unaoendelea katika hifadhi ya Ngorongoro ikiwemo mapitio ya sera ya ardhi mseto ambayo imelalamikiwa na wananchi wa Ngorongoro kuwa haikuwa sherikishi
Tunaisihi Serikali kuzingatia misingi ya Haki za Binadamu na Haki za kiraia za wenyeji wa enel la Ngorongoro na historia ya miongo sita ambayo haki zao za maendeleo zimebinywa na sera na sheria za mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro katika mchakato huo
Uwajibikiaji
Maendeleo ya taifa lolote inategemea viwango vya ubora wa uwajibikaji iliyonayo, tunaunga mkono maelekezo ya Rais kwa viongozi kuwajibika kutatua kero za wananchi bila kusubiri viongozi wa juu kufika maeneo yao ili kuwasilisha kero hizo. Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu kinaiomba serikali na Mahakama kuifanyia marekebisho makubwa mifumo ya Haki nchini kwani ndio njia pekee na yenye tija ambayo wananchi wengi wanaweza kupata haki zao kwa wakati bila kujali aina ya viongozi wanaowaongoza
Matumizi ya mabavu kwa Uwekezaji

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaamini katika utawala wa sheria, uwajibikaji wa watu na taasisi mbalimbali kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Kituo kinamshukuru Rais kwa kuelekeza viongozi wa serikali wasitumie mabavu kutekeleza
sera na sheria za nchi. Kituo kinaishauri serikali kufanya marekebisho katika sheria ili kuondoa uwezekano wa matumizi mabaya ya madaraka @johnadamtz

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Joseph Moses Oleshangay

Joseph Moses Oleshangay Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Oleshangay

7 Apr
@bawazir67 @SuluhuSamia Asante. Kwa uchache, Jana Rais Samia katika hotuba yake ambayo kwa sehemu kubwa ilikuwa nzuri alisungumzia kuhusu eneo la hifadhi ya Ngorongoro ambayo ipo kwenye wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Katika hotuba aliashiria kuwa hatua zifanyike kwa kile alichosema NCAA inakufa
@bawazir67 @SuluhuSamia Kwa imani yangu naamini maneno yake yanatokana na taarifa ya kamati ya Ardhi Mseto (ambayo haikuwa yenyewe na uwakilishi mseto) iliyoundwa na wizara miaka minne iliyopita. Kwa sababu nimeona sehemu ya draft ya kamati, ninaweza kusema haiwakikishi ukweli kuhusu Ngorongoro
@bawazir67 @SuluhuSamia Rais @SuluhuSamia anasema watu wamezidi kutoka 8000 mwaka 1959 mpaka 90000 mwaka 2021. Tanganyika wakati inapata uhuru ilikuwa na 11m leo ni 60m. Binadamu ni lazima waongezeke lakini hakuna madhara yeyote yanayohusu ikolojia kusema sasa kwa maelfu yao waondolewe
Read 8 tweets
7 Apr
President @SuluhuSamia is saying Ngorongoro is in danger of extinction because of pastoralism in the area with their number rising from 8000/9000 to allegedly 90000 in six decades. Am certainly sure, she acted on tainted report from MLUM biased committee
that worked on unilateral directive of @visitngorongoro chief conservator without involvement of the direct victims of both the historical injustice in the place and the potential victims of any decision to be made out of these misinformation
That Ngorongoro cannot accommodate 100000 pastoral people? @visitngorongoro is four times @Zanzibar, it’s six times bigger than @dar and the proposed fake report will grab the land more than 1/2 of @rwanda from the so called 100000 pastoral people
Read 17 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!